DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
Bashite kama Bashite
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanzoni ulimquote chagu nikabaki nashangaa tu.Sawa, apakatwe tu kama alivyozoea kupakatwa labda toka utotoni lakini kura za raia huru wenye akili huyo shetani hapati ng'o! Mtu mzima unapakatwa kama kitoto kichanga, hiyo ni aibu kubwa. Halafu alivyo mhuni, anaweza akawanyea waliompakata halafu kazi ya kuzoa uharo wanaachiwa akina chagu wa malunde🤣
Atasema vita ya madawa haijawahi kumuacha mtu salamaJamani tuelewane
Makonda hata akipitishwa asubuhi hii na kamati bado haiondoi furaha yetu ya yeye kutokushinda kwenye kura za Jana.
Kuanzia Jana na kuendelea lolote litalotokea iwe jina lake kuteuliwa kuwania ubunge au kuja kuwa mbunge wa kuteuliwa ni sawa na ANABEBWA TU
Makonda achukue matokeo ya Jana Kama funzo, ajijue kwamba yeye si muhimu kiasi alichojifikiria wala Hana ushawishi mkubwa aliojiwekea kichwani kuwa anao.
Ajitafakari kwanini watu wengi wamefurahia anguko lake japo tunajua kwenye maisha binadamu huwezi kukosa maadui na wasiopenda mafanikio ya mtu, aangalie mbona kwake waliofurahi ni wengi zaidi.
Makonda ajifunze kuishi vizuri na watu na ubabe auweke kando
Ana mazuri mengi Sana kayafanya, Ila mabaya makubwa machache mno yaliyojaa kebehi, ubabe na majivuno ndio yamemfikisha hapo.
Amevuna alichopanda.
Mwuaji mkubwa Bashite..Kuangushwa katika kura za maoni za CCM, katika jimbo la Kigamboni, kwa Paul Makonda na Faustine Ndugulile, kumepokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wa nchi nzima
Hivi hali hiyo inaweza ikawa inaashiria nini?
Hivi inawezekanaje kwa mkuu wa mkoa, ambaye mara kwa Mara amekuwa akisifiwa hadharani na Rais Magufuli aliyemteua na kumtaja kuwa ndiye mkuu wa mkoa bora kabisa hapa nchini na wakuu wa mikoa wengine, wanapaswa waige mfano wa uchapaji kazi wa huyo Paul Makonda, wanaccm wa Kigamboni waamue kumnyima kura?
Licha ya malalamiko mengi sana ya wananchi kuwa Mkuu huyo wa mkoa hafai na kumwomba Rais Magufuli atengue uteuzi wake................
Hata hivyo Rais Magufuli amekuwa akiweka pamba masikioni na kutotaka kabisa kusikiliza maoni hayo ya wananchi, hadi wakati fulani aliwahi sikika Rais Magufuli akimwambia Mkuu huyo wa mkoa aendelee kuchapa kazi na asisikilize hizo shutuma zinazotolewa na wananchi walio wengi na akaendelea kumsifia kuwa yeye Makonda ndiye RC bora kabisa hapa nchini, ambapo maRC wengine wanapaswa wamuige yeye Makonda kwa.uchapaji kazi wake!
Je ni kiburi hicho alichopewa na Mheshimiwa Rais, ndicho kilichompa kichwa hadi kuwadharau watanzania wote hadi wakuu wake wa kazi?
Bila shaka wananchi bado hawajasahau lile sakata la namna mkuu huyo wa mkoa, Paul Makonda, alivyoweza kutunushiana "msuli" na waziri wa Fedha, Mheshimiwa Philipo Mpango, kuhusu yale makontena yake ya "fanicha" aliyotaka kuyaingiiza nchini bila ya kuyalipia ushuru, hadi pale Mheshimiwa Rais alipoingilia kati na "kumwamuru" mkuu hiyo wa mkoa ayalipie ushuru stahiki makontena hayo
Kutokana na kiburi chake kilichopitiliza wananchi walifikia hatua ya kumbatiza cheo kisichokuwepo cha "Naibu Rais" wa Tanzania!
Hata hivyo wananchi wote wa nchi nzima, hatuna budi kuwapa pongezi wajumbe wa mkutano wa kutoa mapendekezo kwa Jimbo la Kigamboni kwa kufanya kazi iliyotukuka ya "kulikata" jina la Paul Makonda!
Ni matumaini ya wananchi wote kuwa kwenye vikao vilivyosalia vya juu zaidi vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, vitatia "tiki" uamuzi wa wanakigamboni na kutolirejesha jina la Paul Makonda kuwa ndiye mpeperusha bendera za ubunge kwa tiketi ya CCM na kuunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na wanaccm wa Kigamboni kuwa Faustine Ndugulile ndiye apeperushe bendera ya CCM kugombea ubunge huo baadaye mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapa nchini
Mungu ibariki Tanzania
Umemjibu mtoa mada kijinga na kishabiki tuu. Point yake haikuelemea kushindwa kwake bali mapokeo ya matokeo sio kwa Kigamboni tuu bali kwa nchi nzima.
Nadhani Rais Magufuli hana fikra kama zako zilizo lala hivyo anaona reaction ya Watanzania kuhusu mapokeo yao kwa kupigwa chini maoni ya awali kwa "RC bora nchini" kama alivyokuwa anamnadi.
Pengine anajiuliza jee Makonda alikuwa amenishika kwa nguvu za Giza hadi sioni asivyokubalika?
Maana sasa sio siri kama unatumia akili kujua kuwa mama Samia hamkubali, Majaliwa na Bashiru hawamuungi mkono na hata mawaziri na viongozi wenza mkoani walikuwa hawaendi sambamba naye.
Kuna somo ambalo hata yeye Rais atakuwa amejifunza, watanzania waweza kuwa wamekuchoka lakini wanakushangilia jukwaani ila ukibwagwa na kama ulikuwa na kiburi watakuzodoa hadi waweza kukonda kwa siku mbili tuu.
Mtu yeyote hata wewe unaweza kuwa kiongozi ila kiongozi mzuri ni yule mwenye maono, mbunifu na mwenye uthubutu hasa wa mambo ambayo yamekuwa yakiwashinda wengine na hizi sifa ndizo alizonazo Makonda.WEWE itakuwa ndio Bashite mwenyewe...ulichopatia kuhusu makonda ni kuwa anapenda kujaribu na kila muda huwa anajaribu
Hakika hiyo ndiyo picha ambayo hao wanakigamboni wameitoa kwa niaba ya wakazi wote wa Jiji la Dar kuwa almost wakazi wote wa Dar hawamtaki!
Mbunifu na mwenye uthubutu kwenye;Mtu yeyote hata wewe unaweza kuwa kiongozi ila kiongozi mzuri ni yule mwenye maono, mbunifu na mwenye uthubutu hasa wa mambo ambayo yamekuwa yakiwashinda wengine na hizi sifa ndizo alizonazo Makonda.
Ni kweli alukuwa na uthubutu. Kama aluweza kumtandika kibao Mzee Warioba nn angeshindwa?Kura za maoni zisikupumbaze mimi naamini Makonda ndio mkuu wa mkoa bora kabisa kuwahi kutokea, ni kiongozi mwenye uthubutu na mwenye maono na anayependa kujaribu. Naamini kama Makonda akifanikiwa kuingia kwenye baraza la mawaziri na akapewa wizara ya kilimo ambayo imeajiri watu wengi basi kutakuwa na mapinduzi makubwa sana ya kilimo wakulima watanufaika sana
Nilichokigundua mimi ni kwamba kuna nguvu kubwa sana ya media hasa mitandao ya kijamii inatumika kuaminisha uma kuwa Makonda ni kiongozi mbaya, na hii ni kutokana na ujasiri wale uliochangia kuokoa vijana wengi wa Tanzania waliokuwa wakiteketea, sasa wanufaika wote wakahakikisha wanaelekeza nguvu zao kuhakikisha wanamchafua. Kiongozi mzuri hawezi pimwa kwa wingi wa kura pekee yawezekena wake wajumbe waliopiga kura za maoni wakawa sio wafuasi wake, lakini ikumbukwe wananchi hawapigi kura kwa kuangalia ufuasi, wao huangalia ni kipi kiongozi alichowafanyia au atachowafanyia, na kama hivi ndivyo ilivyo naamini Makonda anaweza shinda jimbo lolote lile ndani ya Tanzania kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ya kuokoa kizazi chetu hasa vijana . Ni binadamu wachache sana wenye uthubutu hapa duniani na hawa huwa ni tunu.
Kama ni hivyo kwanini ameangukia pua kwenye kura za maoni? Huyo watu walikua wanamsujudu kutokana na nafasi aliyokuwepo lakini kiuhalisia wengi walikua hawakubaliani naye kabisa. Shughuli imeisha huyo.Kura za maoni zisikupumbaze mimi naamini Makonda ndio mkuu wa mkoa bora kabisa kuwahi kutokea, ni kiongozi mwenye uthubutu na mwenye maono na anayependa kujaribu. Naamini kama Makonda akifanikiwa kuingia kwenye baraza la mawaziri na akapewa wizara ya kilimo ambayo imeajiri watu wengi basi kutakuwa na mapinduzi makubwa sana ya kilimo wakulima watanufaika sana
Nilichokigundua mimi ni kwamba kuna nguvu kubwa sana ya media hasa mitandao ya kijamii inatumika kuaminisha uma kuwa Makonda ni kiongozi mbaya, na hii ni kutokana na ujasiri wale uliochangia kuokoa vijana wengi wa Tanzania waliokuwa wakiteketea, sasa wanufaika wote wakahakikisha wanaelekeza nguvu zao kuhakikisha wanamchafua. Kiongozi mzuri hawezi pimwa kwa wingi wa kura pekee yawezekena wake wajumbe waliopiga kura za maoni wakawa sio wafuasi wake, lakini ikumbukwe wananchi hawapigi kura kwa kuangalia ufuasi, wao huangalia ni kipi kiongozi alichowafanyia au atachowafanyia, na kama hivi ndivyo ilivyo naamini Makonda anaweza shinda jimbo lolote lile ndani ya Tanzania kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ya kuokoa kizazi chetu hasa vijana . Ni binadamu wachache sana wenye uthubutu hapa duniani na hawa huwa ni tunu.
Pompeo alishamaliza kazi " Bashite ananyima watu haki ya kuishi' ( YAAANI NI MUUWAJI) Over and outKuangushwa katika kura za maoni za CCM, katika jimbo la Kigamboni, kwa Paul Makonda na Faustine Ndugulile, kumepokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wa nchi nzima