Uchaguzi 2020 Watanzania sio wajinga, hawatachagua chama ambacho wafuasi, viongozi na wanachama wake sio wazalendo

Uzalendo ni itikadi ya kuweka maslahi ya taifa lako mbele ili liweze kufanikiwa kwa kila namna. Lakini inatia aibu sana CHADEMA na wanachama wake pamoja na wafuasi wake hawana uzalendo kabisa na hawalitakii mema taifa letu.

Kwa mwananchi mzalendo ambae unalitakia mema taifa lako huwezi kubeza mambo ambayo CCM imelifanyia taifa hili tangu tunapata uhuru mpaka sasa. Serikali ya CCM inaimarisha sekta ya afya kwa kujenga vituo vya afya na hospital, mnasema eti ni maendeleo ya vitu. Kwani hawatakuja kutibiwa watu?

Serikali ya CCM inajenga mradi wa JNHPP ili taifa lipate umeme mwingi na wa uhakika. Mnasema eti ni Mega structures na hazina manufaa kwa watu. Kwani huo umeme nyie wanaChadema hamtautumia? Tena kwa bei rahisi! Mradi wa Sgr mnasema ni maendeleo ya vitu sio watu. Kwa hiyo hiyo treni hamtaipanda? Hamtasafirishia mizigo yenu?

Kwa ujumla watanzania wameshawajua ninyi ni wapiga dili na chama chenu kipo kimaslahi binafsi. Sio kuwaletea watanzania maendeleo kwa maslahi mapana ya taifa letu.

Natoa ushauri tu Oktoba msijaribu kugombea nafasi yoyote maana watanzania hawawataki tena.

Siasa sio chuki na uadui.

Mtegemee polisi ndo watakuchagueni, Hakuna mwenye akili timamu atachagua njaa again watz wanataka shibe na sio majengo.
 
Acha kupotosha watu. Tunaijua historia ya nchi yetu. Chadema subirini kugawana meza na viti.
Apo umeongea comrade,natamani tutumie njia ya NAZI dhidi ya NDP au FASCISM ...kukubali nchi kua chini ya watu wa Demokrasia, Haki ,Uhuru na Utawala wa Sheria ni kurudi nyuma kimaendeleo.
 
Usifananishe Ccm na Nazi social party. Ccm ni chama kinachofuata misingi ya demokrasia. Na umeshudia siku mbili zilizopita Dodoma. Ungekuwa na aibu ungejionea huruma maana haiwezekani chama kiwe na mwenyekiti mmoja kwa zaidi ya miaka 20.Kisa tu chama ni cha baba yake,alafu wewe nae ni kamanda wa chama kama hicho.
 
Nazi na Fascism walitumia jeshi,polisi na Gestapo kubaki madarakani na kuimarisha mamlaka zao...hivyo huku CCM tunatumia dola,polisi,jeshi kubaki madarakani ...tusipingane na Dr.Bashiru maana alituma elimu hii ya bure.Pia hao sijui Mbowe na wenzie inawezekana ndiyo makubaliano yao.Mwenyekiti wetu amepata 100% ila sijui mpinzani wake amepata ngapi?
 
Mpinzani gani unaemzungumzia ? Ccm wana desturi ya kumuachia aliyefanya vizuri amalize ngwe yake.
Kuhusu kutumia dola,polisi na jeshi sio kweli. Hamna mwananchi anayeshikiwa bunduki kuchagua Ccm.
 
Duuh kumbe ni utamaduni wetu basi na hao CHADEMA wana utamaduni wao.
Kwahiyo Katibu Bashiru alikua na maana gani kusema kua lazma CCM itumie dola tubaki madarakani?
 
Alifafanua vizuri ukampata. Nini matumizi mazuri ya dola kwa maslahi ya taifa. Utamaduni wa Chadema kumuachia mwenyekiti chama hata kama amefeli!
 
Huu UPUUZI uliouandika INGEKUWA ni UKWELI basi dikteta na chama chake wasingeiogopa TUME HURU wasingeogopa MUONGOZO wa Sheikh Ponda ili kuhakikisha Uchaguzi ni HURU na wa HAKI.

2455082_ERFcWLLW4AIVOAq.jpg

Back
Top Bottom