Akilindogosana
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 4,303
- 12,679
Heri ya mwaka mpya 2023.
Moja kwa moja kwenye mada
Mwaka jana 2022, kama majobless wengine niliendelea kuhudhuria interview mbalimbali za utumishi na sehemu nyingine nyingi sana. Kitu nilichoona naona majobless wanaongezeka sana sio kama zamani nilivyokuwa nikiwaona. Yaani naona makutano na mafuriko ya watu wakiendelea kuomba kazi.
Wengine ni wadogo zangu kabisa 😂😂😂 napiga nao pepa. Sasa kuna kitu nimekiona nimeona nitoe wazo. Kwenye interview huwa nakutana na masela zangu wa zamani na wenyewe wapo kwenye mpambano wa kutafuta kazi. Wengine ni wachovu kama mimi 😂😂😂.
Ila nashangaa nakutana pia na wengine ambao kwao mambo safi na wenyewe wapo kwenye interview. Huwa nawauliza. Hivi ninyi kwenu si wakusuport uanzishe kitu? Unajua kimasiharamasihara unaeza kufika miaka 50 bado unatafuta kazi au unajitolea?
Unakuta mwingine kwao mzazi anamuweka ndani tu. Ila nje kuna magari makali, harrier, vanguard, prado e.t.c unakuta mzee wake anacheo kwenye serikali au sekta binafsi pia anazonyumba kadhaa za wapangaji ila dogo yupo ndani hawamsuport. Wanampa hela ya kwenda kwenye interview tu na miaka inaenda. Au anajitolea kwerikweri 😂😂😂😂😂.
Wengine unakuta wazee wake wapo vizuri ila wana misimamo ya kizee kwamba ajira ndio kila kitu. Kila siku wanamuuliza dogo, mbona hautafuti ajira? Hao wazee huwa ni wakishamba sana wanadhani miaka hii ajira inapatikana kirahisi kama enzi zao, ukimaliza form four tayari una ajira 😂😂😂😂.
Pia kuna wengine wazee wao wanataka dogo asome zaidi ili apate kazi, unakuta mzee anamlazimisha dogo asome masters na PhD eti ndio itamsaida 😂😂😂😂😂.
Kwa niaba ya majobless wengine naomba kuwaambia wazee wote wenye itikadi hizo. Ajira sio rahisi kama enzi zenu za miaka ya 60,70,80,90. Siku hizi watu ni mafuriko. Masters ni nyingi sana na ajira ni ngumu kwerikweri 😂😂😂😂😂.
Suluhisho ni sisi waTanzania tuanzishe utaratibu mpya wa kumaliza tatizo la ajira kwa ngazi ya familia.
Utaratibu ni kuchanga hela angalau mtoto apate mtaji au afanye partneship aanzishe mradi anaoona unafaa. Kama mnachanga mamilioni kwa ajili ya harusi, sendoff, kitchen party kwanini usimsaidie mwanao? Kama unahela za kujenga majumba ya wapangaji kwa mamilioni halafu unaambulia vilaki 3 kwa mwezi kwanini usimsaidie mwanao?
Kama unahela za kununua magari, kluger, harrier, vanguard, kwanini usimsaidie mwanao?
Kama upo tayari kumsomesha mwanao masters na PhD kwa mamilioni halafu akose ajira, kwanini usimsaidie mwanao mtaji?
Muda umefika ninyi wenye angalau uwezo msaidie watoto wenu angalau mtoto apate mtaji wa kujiajiri au pawe na ushirikiano wa kifamilia kusaidia watoto majobless. Msipofanya hivyo mtashtukia mtoto anafikisha miaka 50 hana ajira wala chanzo chochote cha mapato 😂😂😂 wala bila familia.
Natoa siri hii ila usimwambie mtu "VIJANA WENGI WA KIUME HAWAOI SIKUHIZI, KWASABABU HAWANA AJIRA WALA VYANZO VYA MAPATO VYA KUELEWEKA" na "MTOTO HALI CHETI".
Naomba viongozi wa dini msaidie kufikisha ujumbe huu, misikitini na makanisani. Suluhisho la ukosefu wa ajira sio maombezi pekee. Masheikh, Maustadh, Mapadri, Maaskofu, Mitume, Manabii, Wachungaji na watumishi wa Mungu naomba mfikishe ujumbe na Mungu atawabariki.
NB:
1. Huu ujumbe uko dedicated kwa wazee ambao pesa wanayo ila hawana connection ya kuwasaidia watoto majobless. Sisi tunaotokea maisha ya kuungaunga tunakutana ajiraportal 😂😂😂.
2. Mtoto atakayepewa mtaji lazima afanyiwe due diligence mapema mwenendo wa tabia yake asije akahonga hela yote 😂😂😂.
3. Utafiti wa kina wa gharama na makadirio halisi wa mradi lazima ufanyike kwa kina bila papara.
Wengine mtaboresha zaidi.
Samahani kama kuna mtu atakwazika kwa maoni yangu.
Nawatakia mwaka 2023 wenye mafanikio.
Forward huu ujumbe kwa wazazi wote mnaowajua. Au hata kwenye magroup yoyote. Ujumbe ufike. Hasahasa mzazi mweye mtoto jobless au anayejitolea.