Watanzania tuchutame, Uchaguzi Mkuu nchini Kenya umetuacha uchi

Watanzania tuchutame, Uchaguzi Mkuu nchini Kenya umetuacha uchi

Wanauana iwapo kura zinachezewa, sio hapa kwetu kwa maiti hai vyombo vya dola vinaagizwa na majizi ya CCM kuhakikisha wao ndio wanatangazwa washindi. Najuta kwanini nilizaliwa hapa kwenye nchi ya makondoo.
Kuna dude linaitwa Tume ya Uchaguzi. Hili dude linalipwa mabilioni ya kodi zetu kwa lengo moja tu ...kuchafua uchaguzi!

Ili walafi walioifilisi nchi hii waendelee kuitafuna! Masikini Tanzania!
 
Tuseme ukweli tu kuwa majirani zetu hawa wametupiga gap kubwa sana, Sahivi wameanza kuhesabu kura kila kituo nchi mzima na zoezi la kuhesabu linafanyika kwa uwazi kabisa na makamera yakimulika na kila kitu kinachoendelea kuonyeshwa live kabisa hatua kwa hatua... Ile habari ya mawakala wa upinzani kufukuzwa kwa mtutu wa bunduki kisha kura feki kuingizwa kwa mabegi meusi huwezi kuyaona kwa wenzetu..
 


Sina la kusema, nimepigwa butwaa. Najiuliza kama ule nilioushuhudia nchini Tanzania mwaka 2020 ulikuwa ni uchaguzi kweli.

Tukubali tusikubali, huu uchaguzi nchini Kenya umetuvua nguo na kutuacha uchi wa mnyama na kama bado tunazo tuchutame.

Nafuatilia matokeo yanavyotiririka kwenye TV na kushuhudiwa na dunia nzima , bila kusubiri ruhusa ya wenye mtindio wa ubongo!

Eti siri katika kuhesabu kura, really? Kura zikishapigwa kuna siri gani tena? Si ni kutangaza tu matokeo? Huu ujinga aliuanzisha nani hapa Tanzania?
CHAGUZI ZA TANZANIA NI KAMA CHAGUZI ZA KAMATI ZA HARUSI
 
Mungu ibariki Kenya. Viwango vya demokrasia kwa nchi ya kenya viko juu sana kwani wana uvumilivu wa kisiasa hakuna umafia kama huku kwetu wa kuwekea wapinzani vikwazo vya kuweza kuwafikia wapiga kura wao na wanafanya kampeni kwa karibu 10 months without interfeared na chombo chochote. Kwa tz it's another story
 
Lile nduli lililokufa ndio liliharibu demokrasia yetu. Wachomaji huko jehanamu waongeze kuni
2020 upinzani ulikuwa unajaribu uchaguzi ukaangukia kwenye kujichafua.

Unashindanaje na mtu aliyenunua madege, anajenga matreni ya umeme, mafuta hayapandi kiajabu, hakuna mifumuko ya bei ya ajabu hadi wali ukawa sio chakula cha anasa tena.

Anajenga mahospitali, miundo kama yote, mashule. Kifupi hatukutakiwa hata kufanya uchaguzi. Ni ubishi tu wa upinzani.
 
Naona Raila Amoro Odinga anamtimulia vumbi William Samoe Rutto huku Mzee wa Ganja akipumulia mashine na mwingine kaishaaga dunia
 
Leta tofauti ya uchaguzi huo na wa kwetu!!!
Ndugu yangu TUJITEGEMEE, hebu chutama kwanza. Pamoja na nyani kutoona kundule, naomba unipe jibu katika swala linaloleta huo utofauti...je kuna siri gani katika kuhesabu kura?

Kwamba kwenye chumba cha kuhesabu kura camera na simu ni marufuku? Kwamba matokeo ya kura kwenye vituo hivyo iwe marufuku kutangazwa hata na vituo vya habari na TV?
 

Eti siri katika kuhesabu kura, really? Kura zikishapigwa kuna siri gani tena? Si ni kutangaza tu matokeo? Huu ujinga aliuanzisha nani hapa Tanzania?
Isaya 50:11
[11]Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Behold, all ye that kindle a fire, that compass yourselves about with sparks: walk in the light of your fire, and in the sparks that ye have kindled. This shall ye have of mine hand; ye shall lie down in sorrow.

1660072582445.png
 


Sina la kusema, nimepigwa butwaa. Najiuliza kama ule nilioushuhudia nchini Tanzania mwaka 2020 ulikuwa ni uchaguzi kweli.

Tukubali tusikubali, huu uchaguzi nchini Kenya umetuvua nguo na kutuacha uchi wa mnyama na kama bado tunazo tuchutame.

Nafuatilia matokeo yanavyotiririka kwenye TV na kushuhudiwa na dunia nzima , bila kusubiri ruhusa

Eti siri katika kuhesabu kura, really? Kura zikishapigwa kuna siri gani tena? Si ni kutangaza tu matokeo? Huu ujinga aliuanzisha nani hapa Tanzania?

Dah, mkuu Mag 3.

Kwanza heshima, lakini kidogo nami leo ninashangaa kwa mtu makini kama wewe kuuita ule uliotokea 2020 uchaguzi!

Lakini pia tukubali, Kenya nao wamepitia kwenye changamoto za ajabu sana hadi leo kufikia hapa.

Nasi tusikate tamaa; tukijua tu mbinu za kuwaondoa CCM mambo yetu nasi yatanyooka vizuri, pengine hata zaidi ya hao Kenya.

Usione safari hii kuwa ilivyokuwa sasa na kuwasifu. Wasipokuwa waangalifu kitanzi chao cha siku zote cha ukabila kitainuka tena huko mbeleni. Safari hii, pengine sifa kubwa zimwendee Uhuru, kwa haya tunayoona Kenya leo.
 
Ni mapema mno kuanza kujifaragua, hao unaowasifia atakayeshindwa LAZIMA atayakataa matokeo pamoja na mapambio yako ya mtiririko.
 
Lakini inanilazimu kutumia fursa ya mada hii nami binafsi niwe mkweli na hali yetu hapa Tanzania.

Kama kweli tutashindwa kurekebisha mifumo yetu iliyonyongwa na CCM wakati huu wa Samia, itabidi kujilaumu sisi wenyewe.

Kushindwa kwetu hakutakuwa kwa sababu ya maguvu aliyonayo Samia na genge lake huko ndani ya CCM; itakuwa kwa sababu ya ujinga wetu wenyewe, hasa kupitia kwa vyama vinavyojitambulisha kuwa ni vya upinzani, pamoja na asasi zinazojitambulisha kusimamia haki katika jamii yetu.

Uwezo alionao Samia safari hii ni ya kutumia ujanja ujanja zaidi ya kutumia mabavu. Kama hatutakuwa makini, na kukubali kualmbishwa asali, hilo litakuwa ni lawama kwetu wenyewe.

Natumaini, baada ya kuona mfano huu wa majirani zetu, nasi tongotongo zitatutoka na kuadhimia kufanya vizuri zaidi.
 
Ni mapema mno kuanza kujifaragua, hao unaowasifia atakayeshindwa LAZIMA atayakataa matokeo pamoja na mapambio yako ya mtiririko.
Lakini si hata Mahakama zao unajua zinafanya kazi, au hujui?

Sahau hayo ya kule nyuma, angalia tukio hili lililopo sasa, kuwa ndilo funzo muhimu.
 
Back
Top Bottom