Watanzania tuchutame, Uchaguzi Mkuu nchini Kenya umetuacha uchi

Watanzania tuchutame, Uchaguzi Mkuu nchini Kenya umetuacha uchi

Najuta kwanini nilizaliwa hapa kwenye nchi ya makondoo.
Uh - Oh!
Hii ni kali. Ni baadhi ya maneno yanayosemwa wakati wa akili inaporuka, na baadae hujutiwa.

Naomba uniwie radhi juu ya swali langu hili: "Nchi ya makondoo", mwelevu atashindwa vipi kuyamudu na ukondoo wao?

Simama kidete uyachunge vizuri haya makondoo.
 


Sina la kusema, nimepigwa butwaa. Najiuliza kama ule nilioushuhudia nchini Tanzania mwaka 2020 ulikuwa ni uchaguzi kweli.

Tukubali tusikubali, huu uchaguzi nchini Kenya umetuvua nguo na kutuacha uchi wa mnyama na kama bado tunazo tuchutame.

Nafuatilia matokeo yanavyotiririka kwenye TV na kushuhudiwa na dunia nzima , bila kusubiri ruhusa

Eti siri katika kuhesabu kura, really? Kura zikishapigwa kuna siri gani tena? Si ni kutangaza tu matokeo? Huu ujinga aliuanzisha nani hapa Tanzania?

Bado tu misukule ya Nyerere haijaamka, laiti wangekua active kama wanavyogombea kununua jezi tungekua mbali kuliko Kenya.

Kwa ufupi 2020 hakukua na uchaguzi ila uzuri qliyejifanya jeuri na mwamba hakufanikiwa kufaidi matunda ya uhayawani wake.
 
JamiiForums1140732688.jpg
 
Bwana Mkubwa Haki inachukuliwa ikibidi hata kwa nguvu,CCM pamoja na ukichaa wao sidhani &siamini kama wamefika hatua ya kukata tawi walilokalia
 
Back
Top Bottom