Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Hakuna aliye na hakika juu ya uvumi huu lakini so jambo la kawaida kwa serikali kuwa kimya mpaka mudaa huu , ni kwa asilimia nyingi yawezekana kweli mh hayupo katika hali yake ya kawaida
Na Kama ikiwa ni hivyo tunavyo dhani ndivyo basi tukio na utu pia kuguswa kwa namna moja au nyingine tumuuombee M/Mungu amnusuru na kila baya

Ameni
 
Je kama sio jirani yako!
Mimi kama binadamu siwezi muombea mwenzangu afe au aumwe tu siwezi kamwe ila nikiona mwenzangu/jirani yangu haonekani na sijui aliko lazima nitaulizia kujua anaendeleaje maana uzima au ugonjwa wake ni wa kwetu sote hakuna anaeijua kesho yake na hayo yote sio SIRI

Si Anasemaga Mabeberu Hawapendi Maendeleo Anayoyaleta Ndio Maana Wanawatumia Watu (Vibaraka Wa Mabeberu) Kukwamisha Juhudi Zake? Sasa Mbona Kaenda Kutibiwa Hukohuko Kwa Mabeberu? Kama Kweli Mabeberu Wanakwamisha Juhudi Zake Haogopi Kwamba Wanaweza Pia Kukwamisha Na Uhai Wake?
 
Kama mnasubiri avute basi naomba kuwa taarifu Milango yakuzimu kamwe haitomuweza Rais wa jamuhuri Ya muungano wa Tanzania.

Atatikiswa ila hawawezi kuigusa roho yake. Nikweli nimkali ila ni kiongoz shupavu alie na maono ya kweli kwa taifa letu.
Chuki na hasira sio za wananchi ila kundi lawapumbavu na n vilaza fulani. Ndugu zangu kama vile jina lilivyopita ndivyo usalama wake utakuwa naye. Wanyonge wengi sana wamepata haki zao utawala huu na sishangai chuki hii nikwa kaz nzuri anafanya.

Rais amkuwa na ratiba ambayo sio yakawaida nauwenda imemchosha. Kiufupi uwenda sasa atafuwata ratiba nakupunguza kazi. Pia ningeshauri wafanyakaz wa Ikulu wampeleke watoto acheze nao huwa ni wazuri sana kupunguza stress.

Naiman baada ya mapumziko rais wetu atarud kulitumikia taifa lake.
Mungu ibariki tanzania na watu wake na Viongoz wake. Amen
 
Ni siku ya tatu leo kumekuwa na taarifa zinazotolewa na baadhi ya watuamiaji wa mitandao ya kijamii kuhusu afya ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania alipokuwa ktk ziara mikoa ya kusini.

Na wengine kufika mbali kabisa kwa kuzusha kabisa taarifa za kifo kitu ambacho baadhi ya wapinzani wa kasi ya awamu ya tano wamekuwa wakifurahi na kushangilia katika mitandao na kuleta taharuki majumbani na mitaani kiasi watu wengi kuuliza Nini kinaendelea.

Taarifa hizi zimekuwa zikitolewa na watz ndani na nje ya nchi wakati Ikulu haijatoa taarifa yoyote kuhusu kuwa Rais ni mgonjwa.

Nadhani tuna sheria na kanuni kuhusu kutoa taarifa hasa zinazohusu usalama wa nchi Sasa hawa wanaotoa taarifa za kuzusha tu toka katika chanzo ambacho hakijulikani na kuleta taharuki wanatakiwa kufanywa Nini na mamlaka husika kisheria.

Nadhani mamlaka husika Kuna haja ya kutoa mtu mmoja kama mfano ili liwe fundisho kwa wengine wenye nia kama hii.

Ukisoma mitandao ya kijamii ndiyo utajua Nini kinasambazwa na kuleta maneno chini kwa chini na taharuki mpaka makanisani watumishi wameanza maombi ya kukemea kinachoendelea.

Kama huna taarifa acha kuzusha taarifa na kama una taarifa sahihi basi jitoe muhanga kwa kutoa taarifa kamili inayoeleweka sio kutoa taarifa za kuwachanganya watz.

Watz wengi wanaelewa sana nia mbaya za watu kwa serikali hi na kama ndiyo kutafuta mtaji wa kura ktk uchaguzi wa November basi hapo mmepata zero kabisa.

Watu wa Cyber happy mna kazi ya kufanya kuondoa uchafu kama huu katika nchi yetu.

Ni muhimu kuwa na taarifa za kweli kuliko uzushi.....tena wakome wote wenye nia mbovu na Serikali.

Umesema ukweli tupu, ila siungi mkono mtu kutolewa kafara ili iwe mfano kwa wengine
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom