Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Ni siku ya tatu leo kumekuwa na taarifa zinazotolewa na baadhi ya watuamiaji wa mitandao ya kijamii kuhusu afya ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania alipokuwa ktk ziara mikoa ya kusini.

Na wengine kufika mbali kabisa kwa kuzusha kabisa taarifa za kifo kitu ambacho baadhi ya wapinzani wa kasi ya awamu ya tano wamekuwa wakifurahi na kushangilia katika mitandao na kuleta taharuki majumbani na mitaani kiasi watu wengi kuuliza Nini kinaendelea.

Taarifa hizi zimekuwa zikitolewa na watz ndani na nje ya nchi wakati Ikulu haijatoa taarifa yoyote kuhusu kuwa Rais ni mgonjwa.

Nadhani tuna sheria na kanuni kuhusu kutoa taarifa hasa zinazohusu usalama wa nchi Sasa hawa wanaotoa taarifa za kuzusha tu toka katika chanzo ambacho hakijulikani na kuleta taharuki wanatakiwa kufanywa Nini na mamlaka husika kisheria.

Nadhani mamlaka husika Kuna haja ya kutoa mtu mmoja kama mfano ili liwe fundisho kwa wengine wenye nia kama hii.

Ukisoma mitandao ya kijamii ndiyo utajua Nini kinasambazwa na kuleta maneno chini kwa chini na taharuki mpaka makanisani watumishi wameanza maombi ya kukemea kinachoendelea.

Kama huna taarifa acha kuzusha taarifa na kama una taarifa sahihi basi jitoe muhanga kwa kutoa taarifa kamili inayoeleweka sio kutoa taarifa za kuwachanganya watz.

Watz wengi wanaelewa sana nia mbaya za watu kwa serikali hi na kama ndiyo kutafuta mtaji wa kura ktk uchaguzi wa November basi hapo mmepata zero kabisa.

Watu wa Cyber happy mna kazi ya kufanya kuondoa uchafu kama huu katika nchi yetu.

Ni muhimu kuwa na taarifa za kweli kuliko uzushi.....tena wakome wote wenye nia mbovu na Serikali.
...kwani kuna habari tena?
 
Kuna majinga hayampendi Rais wetu mpendwa na kwa taarifa yao JPM ataongoza hadi 2035
Tena yale ambayo hayajaajiriwa na yako mitaani miaka zaidi ya mi4 Sasa,huku SGR na ununuzi wa ndege ukiendelea.
 
Acheni kupotosha watu tulikuwa tunafuwatilia msafara mwanzo mwisho.

Shida ilianza Masasi na sina uwakika kama watu wanao angalia afya ya Rais waliona lile tukio sisi tulio kuwa mbali tuliona kabisa baada ya pale msafara uliondoka na kwenda kijijifulan baadae ukarud ila Rais aliondoka ktk njia ambayo mpaka sasa no one know wala siwezi kuandika hapa as nimfuwasi wa kuto toa kila siri.

Usiku ule ambao nyie mnauliza yupo wapi Taifa lilikuwa kazini na nina dhani hakuna alie lala.

Ila Taifa letu lina tunu yaaman na upendo huwez amini watu walikuwa wamoja kuliko hii mambo ya mtandao kiukweli natamani kulia ila Wazee wetu amabo ni top secret number one wanampenda sana kijana wao kiukweli sina uwakika kama kuna chama kina unity kama ccm.

Nataman kulia ila navipongeza vyombo vyote vya ulinzi na usalama na top secret ya Rais kiukweli hawa ni mashujaa shime serikali yangu na taifa langu.

Tuache upotoshaji... Japo from now Rais atapunguza Ratiba za kaz nyingi nakupata muda wakupata mapumziko. Pia kam mnkumbuka anamualiko wa German kamamnakumbuka sim ya Angel kwa Rais..
Sasa mbona unarukaruka? Touch the point masasi kulitokea nn?
 
Nadhani ni mwendo wa sisi raia kutayarishwa kisakolojia.
Mwanzoni tuliaminishwa kwamba hakuna lililotokea na kwamba Raisi wetu yupo ofisini kama kawaida yake anatengua na kuchagua!
Sasa wameanza kutuaminisha kwamba ni kweli ameumwa na labda yuko kwenye hatua za kupatiwa huduma ya matibabu na labda ni kweli nje ya nchi!
Hatua itakayoufuata ni kujulishwa kwamba Mheshimiwa wetu ame... na hivyo mambo mengine yatafuatia baadae.
Kwa kumalizia tuwaombe tu waungwana kwamba sisi watanzania sasa tumekuwa wakubwa, sisi ni watu wazima sasa na si wajinga kihivyo mnavyotufikiria! haina haja ya kutupeleka hatua moja moja, I mean for God sake we can handle this!
Leo asubuhi barabara ya kuelekea uwanja wandege walikua wanai clear labda mtu anataka kusafirishwa...
 
Huyu mwandishi wa hili gazeti itakuwa darasa la saba kabisa, haiwezekani unaitaja nchi halafu unaandika "tanzania" huu upuuzi ulopitiliza...
Mada nagoma kuchangia
 
Umeshamlaani tayari kama hujui. Ni YESU KRISTO WA NAZARETH pekee mwenye sifa hiyo ya kushinda mauti na kuzimu.
Yesu Kristo mbona alisha sepa kitambo sana sisi ambao bado tuko hai ndiyo mpaka sasa tumeishinda hiyo milango ya kuzimu!!
 
Hakuna aliye na hakika juu ya uvumi huu lakini so jambo la kawaida kwa serikali kuwa kimya mpaka mudaa huu , ni kwa asilimia nyingi yawezekana kweli mh hayupo katika hali yake ya kawaida
Na Kama ikiwa ni hivyo tunavyo dhani ndivyo basi tukio na utu pia kuguswa kwa namna moja au nyingine tumuuombee M/Mungu amnusuru na kila baya

Ameni
Umeambiwa na chanzo gani
 
Wale mnaomuombea Rais wetu mpendwa mabaya yampate ujumbe wenu huu hapa chini. Tena hasa wale mnaolitumia neno la menemene nk. Pia wale mnaotamani kusikia habari mbaya. Basi zikatokee kwenye familia zenu kwa wapendwa wenu kama Mungu wa Israel aishivyo. Mungu wetu ni MOTO ULAO.

Zaburi 118:13
Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini BWANA akanisaidia.

Zaburi 27:12
Usinitie katika nia ya watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo wamenijia, Nao watoao jeuri kama pumzi.

Jihadhari sana kumuwazia mtu mwingine na kumnenea mabaya kwani yatakurudia mwenyewe ×7!!!

Hebu soma Zaburi hizi hapa chini:-
Zaburi 17; Zaburi 35;
Zaburi 54; Zaburi 63; Zaburi 109

Ujumbe kwako Rais Magufuli. Usivunjike moyo.. Kumbuka maneno ya mtangulizi wako Rais Nyerere juu ya vita uliyoamua kuingia vita hii ya uchumi. Wapo WAPUMBAVU yaani watetezi wa mabeberu na wana kelele nyingi. Mwachie Mungu azime kelele zao.

Fahamu kuwa wapo WENYE HAKI WENGI TU WANAKUOMBEA. Usichoshwe na kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji.

Wafilipi 1:6
Basi, nina hakika kwamba Mungu aliyeanza kazi hii njema ndani yako Rais Magufuli, ataiendeleza mpaka ikamilike katika siku ile ya Kristo Yesu.
Amen.

Queen Esther
Amen
 
Tutawasaka hao kwa kutoa taarifa uzushi iwe mfano kwa wengine
wewe mbona mzushi sana leo? taarifa yako ni ipi sasa
KUKANUSHA HUKANUSHI ila unattishia km vileunajua Akwilina yupo wapi Azori au Ben saanane
Wasemaji wa Serikali wapo Kanisani leo Jumapili kaenda kwanini usiturushie
acha Watanzania wanaojua mema au upendo wamtafute Kiongozi wao hata uvunguni
 
Na sio Tanzania tu, Afrika yote marais wa huko wana kazi gumu, raia wanawataka wawe kama Magufuli hususan kwenye vita dhidi ya ufisadi na mabeberu.
Yeye kapambana na ufisadi UPI hapa donor country?
Nipo api mahakama ya mafisadi?I wapi Katiba ya wananchi ambayo ingemsaidia sana kutengeneza mifumo mafhubuti ya kulinusuru Taiga dhidi ya ufisadi/mafisadi?
Anaonekana kuwa anacheza tayari bado hadi sasa.
Matumaini pekee ni kuhakikisha tunahuisha mchakato wa katiba ya Jaji Warioba.
 
Tutawasaka hao kwa kutoa taarifa uzushi iwe mfano kwa wengine
Ukweli na uongo ni kama mafuta na maji. Huwa havichanganyiki. Na uwongo ukirudiwarudiwa sana pasipo kuweka bayana ukweli halisi ndivyo jinsi uongo unavyoenea kwa kasi na kusadikika. Kama hizi taarifa hazina ukweli, basi wenye mamlaka wajitokeze na kuweka ukweli mezani. Vinginevyo tunatengeneza taharuki isiyo na maana hasa ukizingatia tunaenda kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na leo tupo kwenye Uchaguzi wetu wa ndani. Gumzo kuu ni hilo jambo.
Yapo matukio ambayo tumekuwa tukiwaona wasemaji wa serikali wanajitokeza na kukanusha pindi zinapojitokeza taarifa zenye 'uongo'. Lakini kwa muda wa siku tatu wenye taarifa wapo kimya huku wenye kuzusha ndio wanatawala majukwaa ya habari, ifike mahala huu uzushi ufifishwe kwa kuupatia ukweli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom