Mnaosema nchi ina chuki,hivi chuki mnayosema itakapofika nadhani watu tutaftana,nadhani mnaotamka kuhusu chuki,mnaitaka,kwani mlinenalo ndilo mnalopewa.
Chuki zipo nchi za Somalia,DRC Congo,Libya na nyinginezo ambazo kila kukicha kunasikika milio ya risasi na mabomu,hivyo raia hawawezi hata kupata usingizi.
Wewe ambaye unauhakika wakulala bila wasiwasi,ukaenda mahali popote ukarudi nyumbani usiku wa manane kwa usalama kabisa bado unasema nchi ina chuki kweli umefikiri sawasawa?
Nchi ipo salama kabisaa
Wewe unadhani huko ulikoku - pinpoint kuwa ndiko kwenye chuki ulidhani ilianzaje?
Mimi ni mkristo na kila linalotokea ktk jamii siku zote hulitazama kwa mtazamo wa kiimani zaidi kwa kusikiliza Mungu anasemaje juu ya jambo hilo....
Kwa hiyo, naomba nikujibu kwa kunukuu maandiko toka Biblia takatifu:
Yakobo1:14,15
"....14 lakini MTU hujaribiwa na anapovutwa na kunaswa na TAMAA zake mbaya. 15 Tamaa ikiiva,huzaa dhambi nayo DHAMBI ikikomaa huzaa KIFO....." (BHN)
Sisi sote ni WATU na kwa hiyo andiko hili linatuhusu.
Lakini hebu tulitazame kwa muktadha wa kuuangalia uongozi wa nchi yetu chini ya TANU/CCM tangu 1961 hadi leo takribani miaka 68 sasa...
Viongozi hawa ni watu. Na mtu mkuu anayetuongoza leo kama RAIS anaitwa, Bw John Pombe Magufuli wa TANU/CCM...
Hoja muhimu sana ambazo huwa zinajadiliwa mara kwa mara na kutopata majibu na wakati mwingine ya kejeli ni hizi;
å Hivi ni kweli na hakika kabisa kuanzia serikali ya awamu ya 1, 2, 3, 4 na hii ya 5 chini ya TANU/CCM ziliongoza na kutawala nchi hii kwa HAKI ama kinyume chake?
å Mimi naamini hii iliyopo chini ya CCM na Rais Magufuli na zote zilizotangulia hazikutawala/ongoza nchi hii kwa HAKI kuanzia ktk michakato ya kuingia/kuchaguliwa na hata ktk ku - implement sera na mipango yake dhidi ya watu wa Mungu.....
å Kama ndivyo, maana yake ni kwamba kumbe ni TAMAA tu ya kundi dogo la watu (waliojipachika jina la "viongozi") ndiyo inayoweza kuchachua donge yaani nchi nzima....
Nchi hizo ulizozi pinpoint, hawakujikuta tu siku moja wako vile walivyo yaani kwenye machafuko kama ilivyo leo....
Mambo yalianza hivihivi kama mzaha kwa watu kuziamini kauli za ajabu ajabu za viongozi wenye UCHU na TAMAA zao mbaya za kutaka na kutaka tu zaidi na zaidi....
Kwa kuvutwa na kunaswa na TAMAA hizi, mwisho wa siku TAMAA hizo ziliiva/zilikomaa....
Baada ya TAMAA kuiva/kukomaa, then, DHAMBI (kuua, dhuluma, ujivuni, kujilimbikizia mali kwa kuibia masikini, utekaji, husuda nk nk) ikazaliwa....
Matokeo ya DHAMBI siku zote ni KIFO/MAUTI.....
Kwa sababu dhambi ilishakomaa na kisha ikazaa MAUTI/KIFO, basi ni wazi kabisa watu lazima watakufa sana kwa sababu ya MAKOSA ya viongozi hawa waliojazwa na kushiba TAMAA zao mbaya....
That's what is happening ni DR Congo, Somalia, Syria, and other parts of the Universe....
We, Tanzanians are not safe at all if we continue keeping quite by not telling our leaders to do and stand for JUSTICE....
Hapa TUNASEMA kama njia ya kuonya HATARI iliyopo mbele yetu kama hatutachukua hatua sasa....
Hatusemi tu kwa sababu eti tunayataka na kuyaita mabaya yatupate, la hasha....sivyo....
Hayo ni mawazo yako na kwa kweli ni dhana potofu tu....
The devil is always a liar.....!!