Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Kumchukia, au kufurahia baya lolote linalompata mwingine haimsaidii yeyote zaidi ya kumzidishia roho mbaya.
Je watu wenye roho nzuri walifikiria mazuri 7/9/2017 area c ?!. Kama na wao hawakufikiria usilaumu wengine wakiwaza tofauti
 
Duuh
Kumbe yale mafumbo ya kule Twitter yalimlenga John, lakin leo katumbua watu
"Wiki hii jiwe limepata mtikisiko"??

Kwani haiwezekani labda akawa aliacha Maagizo Siku hata Tatu kabla kuwa hilo Tangazo litolewe leo Ndugu?
 
Kwani Mange Kimambi anasemaje?

MZEE BABA SIKUHIZI HAWA VIJANA WAMEHAMIA KWA YULE JAY ZEE. HUYO JAMAA NDO ANAWALISHA UMBEYA NAO NDO WANAKUJA KUTULETEA HUKU JF
1571517331111.png
 
Tukianza kunyoosheana vidole hakuna atakaeonekana msafi, sio beberu, mzalendo, mpinzani wala yeyote.

Cha msingi ni kuwa na roho ya ubinadam tu na kuweka tofauti zetu pembeni.

Watanzania tuna utamaduni wa kuwa wamoja kwenye mambo ya kijamii, jema tunafurahi wote, baya tunajumuika wote kufarijiana.

Sina uhakika na tetesi zinazoendelea, lakini jambo moja tunaweza kufanya ni kuomba na kusali, ikishindikana kabisa, kunyamaza itakua busara zaidi.
 
mara nyingi nakuaga pande wa upinzani. Lakini hata kama humpedi Magufuli kiasi gani huwezi ukachekelea kuumwa kwake hadharani. Hata kama moyoni kwako unataka iwe hivyo, sio kitu smart kuonyesha hisia hizo kwa umma, ni kosa moja kubwa sana kisiasa.
Ndio maana hata Tundu Lissu alipopigwa risasi Magufuli alitweet kumpa pole, japo naamini serikali yake inahusika, lakini alifanya kinachotakiwa kufanywa na mwanasiasa. Hutakiwi kushangilia ugonjwa wala kifo cha mpinzani wako hadharani.

Walichonishangaza zaidi hawa Wapinzani walikuwa wakichekelea wakati hata mtu mwenyewe haijulikani kama ana afya kweli ama mgonjwa, sasa ukishangilia halafu mtu akajitokeza mzima kabisa utajificha wapi?

Najua ni viongozi wachache wa Upinzani wamefanya hivi, lakini wapinzani wanapaswa kufundishana namna ya ku behave mbele ya public, samaki mmoja akioza watatangaza mmeoza wote, wanaangaliwa na watu wengi, na kila wanachoandika watu wanaki judge.

Hapa wanawafanya CCM kama akina Musiba hivi kuaminika zaidi kuwa Wapinzani wapo kwa ajili ya kumduru magufuli na wanashirikiana na mabeberu kufanya hivyo, yaani wanajipiga risasi ya mguuni kama sio kichwani kabisa.

Wamenisikitisha sana
 
Pamoja na kwamba alikua kiongozi wa nchi pia ni baba na ana familia iliyokua inampenda,muwe mnawafikiria hao hawajawakosea lolote [emoji22]
Shubamiti anavyowadhalilisha watu tena hadharani na kuwafukuzisha kazi hajui kama wanafamilia na watoto ebu lile tukio la kumtukana Enjinia famila yake imejisikiaje .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom