Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
37(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais
kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu
kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa
kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais
ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi
cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya
40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka
Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na
uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua
asilimia hamsini ya Wabunge wote.
 
Mbwaymbwai tu . Ye so anavunga mbabe . Sasa tunaloga tu mpaka mbabe atajulikana
 
Yaani kuna watu ni wapumbavu sana. Kwani kuna mtu ataishi milele? Siku za kuishi binadamu zinahesabika na hesabu yake ni ya tarakimu mbili tu. Awe Magufuli, uwe wewe zitto, na huyu pacha wako kigogo wote nyie ni tarakimu mbili tu. Kwanza wewe na pacha wako wote mnaishi kwa matumaini. Usitake tuongee hata kule unakochukulia vidonge. Acheni chuki za kijinga.
 
BINADAMU tumekuwa sawa na wanyama.Tunajadili maisha ya Kiongozi Wa Nchi kimzaha mzaha sana badala ya kumwombea (ingawa huu ni uzushi wa mchana kweupe).

Hivi vitu vya kuzusha na kushadidia uzushi siyo kabisa.Hivi mtu ukiambiwa prove beyond reasonable doubt itawezekana kweli?

Jamani tuombeane mema hata kama kwenye siasa tunatofautiana mawazo.

Tusipotoshane.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom