Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Kwani ibada ni lazima kanisani? Mimi mbona huku nilipo hakuna kanisa langu la ELCT,lakini huu ni mwaka wa 3 sasa nasali zangu ndani,nina app ya tv za bongo,nafuatilia na kushiriki ibada kwenye tv yangu safi kabisa.
Kesho Mh. anaweza kuamua kujisalia zake home tu,na hakuna haja ya kuhoji ni kwa nini.
 
Utabiri sio ishu maana yawezatokea ama laa.

Codes inakuja hivi upo nyumbani halafu mkutano unawakilishwa wew umeenda kuchunga au unaumwa!!.

Ngoja usiku wa manani ufike tuchungulie kitaalam.
 
Shubamiti anavyowadhalilisha watu tena hadharani na kuwafukuzisha kazi hajui kama wanafamilia na watoto ebu lile tukio la kumtukana Enjinia famila yake imejisikiaje .
Kwa maana hii laana juju za waathirika wa Amri zake ndivyo vimemnasa mtukufu?
 
Kwani ibada ni lazima kanisani? Mimi mbona huku nilipo hakuna kanisa langu la ELCT,lakini huu ni mwaka wa 3 sasa nasali zangu ndani,nina app ya tv za bongo,nafuatilia na kushiriki ibada kwenye tv yangu safi kabisa.
Kesho Mh. anaweza kuamua kujisalia zake home tu,na hakuna haja ya kuhoji ni kwa nini.
Kumbe typo dhehebu moja
 
Nilipata Ghadhabu sana, nikiwa kama mdau wa Demokrasia na haki za binadamu kuona kuna kiongoz anathubutu kuwaita Watanzania wenzake "wadudu " tena mbele ya kadamnasi na mbele ya media

Niliona hii ni dalili nyingine ya vijana walio aminiwa na Mh Rais JPM, lakin wanajimwambafy na kujivika mamlaka wasio kuwa nayo

Ila leo nimeamini jamaa hakukosea sana, nafuta kauli zangu za kejeli nilizotoa kwake siku ile,

Na inawezekana neno wadudu lilikuwa ni understatement

Nimeelewa kuwa

1)Ni Wadudu tu, wanaoweza kushinda mitandaoni wakifurahia jambo na wakifurahia au kusubiri kwa hamu ujio wa taarifa mbaya za mwanadamu mwenzao, tena kiongoz wao. Na tena wadudu hao sio jamii ya Nyuki, Siafu au jamii nyingine ya wadudu wenye akili, siafu, Nyuki na baadhi ya wadudu wana upendo, Ushirika, uzalendo kwa makundi na vichuguu vyao kuliko wapinzani wa Tz, wanaheshimu viongozi wao balaa, nawaza labda wadudu jamii ya nzi,mende na wengineo ambao hawana ustaarabu wa kuishi kijamii ndo watakuwa na sifa za wapinzani tulio nao Tz.

2) Ni wadudu tu ndo ambao kila kitu hupiga kelele ,liwe jema au baya, Mchukulie nzi, kutwa kucha yeye ni nzeee, nzeee, nzeee, anapiga kelele, anacholilia hukion, hujui kuwa anafurahia au anahuzunika, na mbaya zaid ni kuwa anapiga kelele bila kufanya hatua yoyote, Nzi hang'ati,
Ni aheri kama nyuki, akitulia anatengeneza asali, ukimzingua anapiga yowe kidogo, huelewi anang'ata. Sasa kuwalinganisha wapinzani wa Tz na wadudu aina ya Nyuki sio sawa, hawa hawang'ati ,na wala hawatengenezi asali ,kazi kupiga domo tu, yee yee yee ,hawa ni wadudu jamii ya nzi na mende

3)Ni wadudu tu ambao watakuwa na usahaulifu kama walio nao wapinzani wa Tz

Juzi juzi tu mtu wanae muona leo ni hero kwa kuwaletea habar za uzushi, alikuwa ameweka kambi la mashambulizi kwa mwenyekiti wao,

Mwenyekiti wao hajajibu hata hoja moja, na wala halijawa tatizo, leo hii mtu huyo kazusha ya kuzusha, Msigwa ameendelea na majukumu yake ya kutangaza teuzi, wanabak wanalalama, mbona tuhuma hazijawekwa sawa? Wadudu mbona mnakuwa wasahaulifu? Tuhuma za mwenyekiti mliweka lini sawa? Na imagine tuhuma za mwenyekiti zilikuw zinahusu majukumu yake ya kazi, tuhuma hiz za leo ni binafsi (afya ni mambo binafsi) .

Au ndo muendelezo wa yale yale ya double standards, chama mnataka kitawaliwe kidikteta, miaka nenda rud,mwenyekiti ni huyo huyo, et hakuna mwingine mwenye vigezo, ila mkiambiwa na sisi kama nchi hatuoni mwenye vigezo vya kumpokea JPM tunataka aendelee, mnaanza kung'aka kuwa haiwezekani ktk watanzani m50 akosekane mwenye vigezo, wadudu mbona mnashindwa kutumia logic ndogo tu?

Hivyo kwa heshima na taadhima, naomba nimtake radhi yule mheshimiwa alie waita wapinzani wa Tz kuwa ni wadudu, sababu siku ile nilimlaani vikali kwa kutumia maneno yasiyo na staha kwa watanzania wenzake

Ila kwa yanayoendelea leo, yamenifanya nitafakari, na kugundua kuwa jamaa alikuwa anajua kitu cha ziada ambacho mimi sikuwa na najua kwa wakati ule

Hivyo namtaka na kumtia moyo, ajitokeze aongezee na kutolea ufafanuzi kwa msisitizo kuwa wapinzani wa Tanzania ni wadudu wa jamii ya nzi Na mende, sio wadudu wa jamii zinazojielewa kama Siafu wanaopiga kazi balaa(hapa kazi tu), nyuki wanaotengeneza asali (wanaunga mkono serikali ya viwanda) Vipepeo wanaoruka na kusaidia ktk pollination (kama Bombadier zetu tu)Na wadudu wengine wa aina hii.

Viva JPM, Viva Tanzania.
Hawa wa sasa hawako sawa kusherekea tetesi, na unaowatetea nao hawako sawa hata kidogo kwa kuwaumiza nafsi wenzao kwa muda mrefu. Unapoamua kuwafungulia viongozi wote wa chama kesi za kubambikiza unajengea roho gani kwa wafuasi wao ?!. Unapoamua kufanya siasa wewe na chama chako huku wapinzani wako hawatakiwi kukusanyika hata watu watatu unajenga roho gani kwa wafuasi wa upande wa pili ?!.

Tuwe wakweli haya yameletwa na watawala zaidi kuliko wapinzani wao
 
Hii ni story ya kweli na huu niushauri kwa wale wenye madaraka na pesa kuto jisahau nakuchunga midomo yao pindi wanaongea.

Siku moja kiongoz wa taasisi fulani alimkuta ofisa wa daraja la chini akitoa maoni yake kwenye kikao fulani sasa yale maoni yakawa kama yanamgusa na kwa hasira akamtafuta yule kijana nakumwambia atamshusha daraja na kumkaripia sana yule boss alikuwa nikama daraja la nne kutoka yule ofisa. Yule ofisa hakujibu sana zaid yakumsikiliza Boss wake nakusubiria any time kushushwa daraja lakin kilichotokea yule boss akawa ndie anashushwa daraja miaka nane sasa yule bwana kila akifika nafas fulan anashushwa anakaa mwingine.

Hii inamanisha nini hasa? Wanadam ni viumbe hatari sana kunawanadam sio wakawaida. Hivi sijuwi kama umewahi sikia habari ya mtu mmoja alikuwa akimshauri kijana na yule kijana akamwambia ujana wangu ale nani? Haikupita muda yule kijana akafa kifo cha ajabu sana.

Ndugu zangu kuna watu niwakawaida sana ila waogope sana na hawa tupo nao maofisin na majumbani usiwachukue poa. Kuna kiongoz mkubwa sana amekutana na mambo mazito sana ila angalia watu walio simama nakumshughulikia lile kundi wengi wamepumzika na hiyo ni picha halisi ya hatari ya kiumbe mwanadam.

Nani anamkumbuka kiongoz fulan wa upinzani alie kuwa akiwasemea wanakijiji wa kijijifulan kusini alafu akasimama mbunge wa lule jimbo nakumnyooshea kidole yule kiongoz wa upinzan baadae alipata ajali na ule ule mkono alio mnyooshea ukakatika. Hayo ndio maajabu ya kiumbe mwanadam na hatari zake.
Wapo watu ni hatari kuliko sumu ya koboko. Kuna watu akikuangalia au akiumia moyoni na wewe unaumia kama alivyo umia. Jambo linaweza kuwa baya sana.

Usimdharau mtu kwa maisha yake au nafasi yake kuna watu ni zaid ya hatari. Mkurugenz fulan akiwa ktk kikao alikutana na swal kutoka kwa kujana ambaye kwa nafasi yale nikama mtu wa certificate sasa yule mkurugenz hakupenda swal lile alichokifanya nikumpa transfer kwenda mbal kabisa na mkoa wa Dsm sasa kilichotokea yule kijana aka pangua alafu akaomba kuonana na Mkurugenz na alikuwa ananeno moja tu kumuuliza je amewauliza HR file lake kama analo? Mkurugenz kwa kiburi akamuagiza Mkuu wa HR kijana akiendelea ku pangua transf afukuzwe... Tobaa kumbe anajifukuza. Basi jamaa kwel akafukuzwa na alipo pat baruwa akaomba tena kwenda kwa mkuu nakumshukuru mwaka mmoja baadae yule yule alie mfukuza akaja na dispatch kutoka ikulu ya baruwa kutoka kwa Rais kwamba hana kazi. Ndugu zangu sijuwi niseme nin mnielewe juu ya utisho wa mwanadamu na vile yatupasa kuchunga midomo na action zetu.

Kun vijana wameheshimiwa nakupewa madaraka ila uwenda miaka yao imekuwa mifupi kwa kulewa madaraka wamewaambia watu wataona na hawajuwi same people wanatoa taarifa zao na uchafu wao bila chenga na siku zao zinasoma kama mshale wa saa.

Mkuu mmoja wa mkoa miakafulan akaweza kujuwa aina ya hawa watu na ktk kujiham akawa anawapiga majungu nakuwanyanyasa sana siku anatenguliwa mmoja ya wale aliwanyanyasa ndio alikuwa mkuu wa mkoa. Na aliondoshwa usiku wala sio mchana. Cheo nidhamana waheshim watu na funga mdomo.

Naogopa mdomo naogopa madaraka yakiwa yanakuongoza bila kuyaongoza. Kitisho cha Goliati kilimfanya Mungu kushuka nakumuondoa kupitia kijana mdogo sana hili nifundisho kwamba alie kupa wewe ndie kamnyima yule be humble person.
Mimi nimeelewa FULANI FULANI FULANI FULANI
Mwaka Fulani
Kiongozi Fulani
Mkoa Fulani
Kikao Filani.
Ajali Fulani.
 
Hizi nyuzi zimekuwa nyingi na kwa bahati mbaya kwa kiasi kikubwa ni pumba zinazosababishwa na ushabiki.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom