Iwapo leo Jumapili tarehe 20-Oct-19 hatutahabarishwa Mhe. Rais wetu Mpendwa amesali kanisa gani kama tulivyozoeshwa na bwana Gerson Msigwa, ninawaomba Mlioko Chato mtuambie ni nini kinaendelea ikiwa ni pamojana kutujuza kama Kipenzi cha wengi,Rais wetu JPM yupo huko Likizo.
Hatujamsikia siku tatu au nne sasa na kwa style yake ya kutaka kuadress mambo kupitia live streaming pamoja na live coverage ya radios na television inatupa mashaka iwapo Mhe. yupo Chato kapumzika au vipi.
Kwa tunaomfahamu,Mhe. anaipenda Chato vibaya mno. Ameifanyia makubwa chato na mara zote huenda Chato mapumzikoni.
Kwa kuwa tumezoea kila mahali anakokuwepo lazima kishindo hasa cha wana usalama kiwepo inawezekana safari hii kaamua kwenda kimya kimya na kama mkuu wa nchi halazimiki kila anakokwenda itolewe taarifa. Lakini pilika pilika zisizo za kawaida pamoja na ulinzi wa kishindo vitadhihirika. Mlioko Chato tuambieni, Mhe yupo huko? Pale kwake kuna pilikapilika zipi? Ni Kipi kinaendelea huko?
Kama Mhe. yupo mapumzikoni namtakia mapumziko Mema, Mungu azidi kumpa nguvu, arejee kwenye majukumu yake kwa kasi na ari mpya.
Sent from my SM-J410F using
JamiiForums mobile app