Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Mi nafikir tuanze na Rais.ABINAFSISHWE.
Hana afanyalo tukajivunia ukiachilia mbali kudandia cheap popularity ya Yanga ili tujue yupo. Zaid ya hapo hana ajuacho zaid ya kukopa kopa tu na kuzidi kulitia taifa hili kwenye matatizo mazito ya madeni mbele ya safar.
Matatizo wanayopitia Kenya sasa hiv hayakuanza ghafla tuu, ni kwa style hii hii ya kopa hapa..kopa palee na mwisho wa siku pesa zinaliwa na wajinga wachache aliowachomeka kwenye idara za wizara mbali mbali ..na pia anawapa maelekezo kabisaa kwamba WALE KWA UREFU WA KAMBA ZAO kiasi kwamba leo hii mkurugenzi wa halmashauri ya Mkuranga mkoani pwani anawaamuru wafanyakazi woote chini ya halmashauri hiyo walipe 70,000 kwa ajili ya kugharamia send-off party yake
 
Mkuu sana Pascal Mayalla hiki ulichokiandika kinawezekana sana na sababu kubwa ni inferiority complex ambayo ilipandikizwa na wazungu wakituaminisha kuwa nchi yetu ni masikini, na sisi uwezo wetu wa kufikiri ni mdogo. Hii dhana ni potofu kabisa. Nchi hii imejaa watalaamu wa kila aina. Yaani fikiria unampeleka Mbunge Msukuma kwenda kujifunza ili aje ashauri mkataba wa ubia badala ya kuchukua wasomi vyuoni wa aina zote.
 
Hatuwezi kukubali ya kwamba kuna Jambo hatuliwezi Karne ya 21 huo ni udhahifu mkubwa nchi yenye watu 67 milioni , kuhusu kusaidiwa hatukatai lakini iwe Kwa uwazi na muda mchache kisha tulisongeshe wenyewe , hao watawala hata wakodishe TRA Kwa mwekezaji Sisi powah tu Kwa maana Hata hiyo TPA faida yake iko wapi zaidi ya kuwa mzigo Kwa maendeleo ya Taifa na kichaka chao.
TAIFA LITAKUWA LA HOVYO HILI HII SIYO KARNE YA KUSHINDWA KILA JAMBO NI KUTHUBUTU TU.
 
Mbona tusiweze? Siku wanasiasa wakiondolewa majukumu ya kuteua CEOs wa Taasisi na badala yake vetting system ikatumika tutaweza! We angalia utashi wa Rais unavyofanya disruption ya routes za Air Tanzania kila siku! Sasa sijui customers' satisfaction and loyalty itatoka wapi?
 
Kama una copy ya huo mkataba tuwekee hapa tuone unasemaje kwanza.
Halafu ajabu nyingine ni hii akili ya kuamini kuwa Watanzania hawawezi ila Waarabu wanaweza!!!
 
Kwa maana hiyo umeconclude kuwa kwa vile sisi hatuwezi pia kizazi chetu kwa miaka 100 ijayo nacho hakitaweza ....!!

Yah right. This is Tanzania .....!!
 
Kaka kushindwa kwa serikali hiii wajiuzuru. Kwanini awamu ya Tano waweze awamu ya Sita wanashindwa. Watanzania tunaburuzwa si kwamba hatuwezi. Si kwamba wakiwekwa watu wengine Bandari haitaleta Tija. Ni kwamba wameshindwa waondoke.
 
Mzee pascal Kwa nini hatusomeshi watu wetu kwenye hiyo Nyanja ?
 
braza jifunze kujipambania mwenyewe na kutomtegemea mtu ipo siku utasaidiwa mpka kwa mkeo amini maneno yangu
 
Paskali.

Mimi naliona kwenye angle tofauti. Haya maamuzi mazito mno yafanywe na serikali ya Tanganyika kama ilivyo kwa Zanzibar.

Waziri na Rais ni Wazanzibar. Iko namna hili limgesubiri katiba mpya ili kuwe na serikali ya Tanganyika.

Zanzibar watajenga bandari kubwa. Please read between the lines if you understand what I am insinuating.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…