Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Kawaida yetu sisi tukiwa kwenye mitandao huwa tunaweza kila kitu lakini tukipewa tunaharibu.

Ni kweli kabisa huwa hatupangi mipango ya muda mrefu hasa kwa investments kubwa kama hizo ulizozisemea.

Hata hiyo JNHPP hatuna mpango wo wote wa muda mrefu, huwa tunajisemea tu tutatumia umeme kwa hivi na vile.....

Tunamuomba Mungu atusaidie kuzidi kutupa hekima.
 
Pascal una mawazo kama yangu, hongera kwa uzi mzuri sana.
Jamani ndugu zangu Watanzania tukubali tu sisi hatuwezi kuleta ufanisi. Tunachoweza ni kuiba tu kufirisi haya mashirika.
Jana nimetoa mfano wa Customs ya Tunduma border Zambia, Lori moja kupita kwenye scanner linatumia mpaka dakika 30, kwa saa 1 ina maana yatapita 4 au 5 tu out of hundreds yaliyopo kwenye foleni. Je tupo serious kweli?
Scanner ya upande wa Zambia ni dakika 5 tu chap Lori limetoka.

CAG Professor Assad aliwahi kusema Watumishi wengi kwenyeTaasisi za Serikali ni incompetent. Mavyeti tu wanayo, ubunifu na uwajibikaji zero. Wanawaza madili tu.
Wawekezaji waje tu sisi hatuwezi.
 
Naungana na hili rais na mawazili tuwape wawekezaji wawe katika ivyo vyeo kwanza
 
Watu wa kulaumiwa kwanza ni mkapa,kikwete,Samia,maghu Hawa ndio waliofanya madudu,serikali imejaa wezi watupu,huko Ttcl,wakurugenzi Wana vikampunicvyao vya kutoa internet,deal hazitaenda serikalini,watajipigia pande TU,Ttcl "iliingiliwa "kimwili ikazaa Airtel,mkapa,kikwete walikuwepo walikuwa wanapiga makofi TU!!
Na kwa watumishi wa umma,wengi ni wezi,hawajuhi kazi,wamepata kazi kimaghumashi,Sasa wanatumia nafssi zao kuiba,boss wao Rais nae nidhaifu,analetewa wezi anashindwa kuchukua hatua,
Kubaki na bandsri mikononi mwa wazawa,wakati wizi ukiendelea na pesa kuingia mifuko binafsi,Bora tuibinafsishe,tupate pesa nyingi zijenge zahanati.
Tulishindwa kuendesha TBL,alikuwepo manager yeye kazi yake ilikuwa kujaza ndugu vilaza watupu!,,ikabidi iuzwe Sasa hv,IPO mbali sana,
Halotel, wa likuja juzi TU lakini wameishaipita TTCL ambayo IPO tangu mkoroni!!
Kwa ufupi,hii miradi mikubwa,atcl,tanesco,dawasa,ni Bora tuwakabidhi watu binafsi waendeshe sio Hawa wabongo wasio na nidhamu ya kazi,
Na ajira ziwe za mkataba
 
Ila "we should not throw a baby and bathtab"
Tusitupe mti na jongoo wake,
Ubovu wa watumishi kwanza wanapatikana kimaghumashi,wapo watz wenye uwezo mkubwa,ila ndio hawana connections,yanapata mavilaza matupu
 
Watanzania ni kama ma ng'ombe yanayo swagwa wala hayajui yanapo pelekwa ni kupelekwa msobe msobe tu.

Uafrika hasa utanzania ni LAANA.

Wale Raia 66 walio ukana utanzania na wengineo wengi waliokimbia hii nchi na hili Bara wamefanya jambo sahihi kabisa la kuvua Laana na kujitakasa kutoka kwenye Laana.
 
Hakuna anayeipenda Tanzania hata ukiweka watanzania ni mwendo wa kuiba mwanzo mwisho hakuna cha maana watakachofanya
Uafrika hasa utanzania ni LAANA.

Wale Raia 66 walio ukana utanzania na wengineo wengi waliokimbia hii nchi na hili bara wako sahihi kabisa kuvua Laana na kujitakasa kutoka kwenye Laana.
 
nothing impossible under the sun the word it self say am possible,ni aibu kubwa kwa taifa kushindwa,hata huyo mwarabu hajawahi kuwa mwema kwa lipi? ni biashara kama zingine tu anategemea faida.

*Ni bora tudeme na wezi wetu(sawa na mwanao akiiba ndani) tutafika tu.
 
Sisi kama nchi tunaweza tena kwa ufanisi mkubwa tuu.
Tatizo ni kwemba akiibuka aliyebarikiwa uwezo wa hali ya juu atachukiwa na kizimwa na kupotezwa kwa namna yoyote iwe kwa risasi,kutekwa na kupigwa hata kulogwa inapobidi. Na hii itaanzia ngazi ya familia,ukoo,jamii na kiserikali.
Akipewa mtu nafasi ataanza kuvimba na kuiba,kunaynyasa wengine na kujifanya Mungu mtu.
Utakosa ushirikiano mpaka utamani kuhama nchi.
So,tatizo lipo kwa wanaadamu wenyewe
 
hebu waambie hawa mazuzu wanaozusha uongo
 
Tunashindwa kwasababu tumechagua kushindwa! Mifumo yetu ya utawala tayali ni collapse huwezi kupata ufanisi kwenye mfumo uliyokufa!

Mkurugenzi wa shirika kubwa kama bandari anachaguliwa na Rais! Na Rais amepatikana kwa kuiba kura!! Mwizi ndio anachagua mtu wa kuongoza bandari!!

Hakuna uwazi uyo mtu amepatikanaje na kwa vigezo gani? Ili mradi tu Rais kamchagua!! Utasikia tiss wamemfanyia vetting! Tiss awa ambao wanaiba kura!? Tena wanaiba kwa mbinu za kiganga za kienyeji!!wala sio za kisayansi!

Tiss ambao hawana exposure yeyote zaidi ya kuchoma nyama mnadani na kununua wanawake malaya, pale chako ni chako bar!! Watu wa dizaini hio watamfanyia vetting ya maana nani? zaidi sana uwa wanaangalia kama mlengwa ana kadi ya kijani tu.

Harafu tunakaa kabisa tunategemea ufanisi kwenye bandari ambako upatikanaji wa mkurugenzi wake umegubikwa na rushwa,ukabila,udini na wizi!! Ni sawa na kusubili meli jangwani.
 
Kwani nchi hii haina what we saw call them wataalam
Tupo karne ya 21 yenye teknlogy ya hali ya juuu
Ni muda wa kuamka kutoka kwenye usingizi wa pono
Kwani kizazi kijacho kitatushangaaa
Ni bora kina mkwawa na wengineo kuliko uongozi wa sasa
 
Serikali haikuwa kunufaika na ubinafsishaji. Mashirika mengi yalikufa kabisa, mengi tukaja kushtuka yapo hoi trc, tanesco, atcl, ttcl
Serikali kwa maana ya watendaji waliokabidhiwa mamlaka kuendesha mashirika, viongozi wa juu Serikalini, wafanyabiashara wakubwa ndio walionufaika kwenye ubinafsishaji uliopita. Ushahidi upo TTCL, kwa miaka mingi tu wafanyakazi wa kampuni ile ya Serikali ndio wanufaika wa ubinafsishaji ule. Takukuru wako kimya tu, hata zile sheria za uhujumu uchumi nadhani hazitumiki kabisa. Nchi inaenda kienyeji kama vilabu vyetu vya mpira na vyama vya ushirika aka ushirikina!.
 
Shida na ujinga wote huu ni matokeo ya mifumo ya kipuuzi ya ujamaa,Huwa haijengi hoja ila inategemea propaganda,hisia na Imani..

Hao hao wajinga na wapuuzi wenye hizo mentality over years wameshindwa kuleta Ufanisi na ndio maana Mwingi na Mkapa waliachna na hayo mawazo ya ujima..

Imagine pamoja na kujaza sijui wanajeshi na Tisa huko bandarini chini ya awamu ya 5 hakuna Ufanisi wowote sana sana wafanyabiashara walimkimbia Bandari Kwa sababu hao hao Watumishi wa Umma na wao wanataka pesa ,na hawawezi kuwa na Ufanisi kama private sector..

Private sector hainaga urasimu Wala Mlmilolongo ya urasimu wa kindezi,ukizingua unakuwa fired ndio maana Kuna Ufanisi..eg Dart pamoja na kuwa na njia zake binafsi ni hasara daily Kwa sababu ni Mali ya Umma shamba la bibi
 
Hii nchi hata kujenga vyoo hatuwezi.

Na hatuwezi sio kwa sababu hatuna uwezo, hatuwezi sababu ya mifumo mibovu ya kiuongozi.

The whole system needs to be rebooted.
 
Acha zako wewe.

Tumeshindwa wapi wakati nafasi za juu kwenye taasisi zote mnaweka watoto wenu wasio na SIFA

Fungueni milango na wekeni uwazi wa mishahara watu waombe hizo nafasi halafu uangalie ufanisi.
Mishahara iliyowaz ni walimu tu laki laki hao vitengo wanakula kwa urefu wa kamba
 
Nimekumbuka ubinafsishwaji wa TANESCO enzi za Mkapa, kumbe ulikuwa ni mpango wa kupiga hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…