Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Watanzania baada ya uhuru hatukujiandaa na mambo makubwa kama haya.

Mwalimu Nyerere alikuwa na maono lakini alikosa wale waendelezaji baada ya yeye. Nchi zote ziloendelea wamefanya hivyo hutayarisha vizazi vijavyo kuja kuendeleza yale yanojengwa.

Hadi leo tuwashindwa kuendeleza masoko makubwa kama soko la Kariakoo je, tutaweza vipi kuendeleza miradi mikubwa khasa ile ya kimkakati?

Hii miradi yote yahitaji akili kubwa na mipango sahihi ya kuhakikisha ni endelevu hata kama itaendeshwa na wabia.

Barani Afrika kuna nchi ambazo zina watu wa ajabu sana si viongozi wala wale wanoongozwa.

Hata mtu akipelekwa kusoma nje kujifunza akirudi huwa ndo mzigo zaidi na akili yote huiweka kapuni.

Wenzetu wachina na waarabu wakipelekwa kusoma huko nje hurudi na ari ya kutaka kuonyesha ujuzi wao waloupata huko nje, wakati mtanzania akirudi nyumbani huanza mipango ya upigaji.

Ipo mifano kama Waziri Kindamba je amesomea nini huko nje? na leo atumika kwenye eneo gani ili kutia ujuzi wake?

Na si yeye tu wapo wengine ambao leo hii wameamua kuweka akili zao kapuni badala ya kuzitumia.
 
Bora kuwapa wageni pengine tija itapatikana. Watanzania wengi ni mafisadi na hawaridhiki. Mtu hata alipwe milioni 15 kwa mwezi bado anafikiria kuiba tu! Hatuwezi kuwasapoti watu wetu kisa tu ni wenzetu ilhali ni mafisadi na wezi wakubwa. Tena ikibidi na mashirika mengine wapewe hata ikibidi na TRA.
 
Kushindwa kwetu kunaanzia kwenye dhana hii ya kulalamika badala ya kutafuta suluhisho.
Kila tatizo linalotokea badala ya kutafakakari, kulichambua na kisha kulitatua tunakimbilia kutafuta visingizio.

Mtu aliyezaliwa siku tuliyopata uhuru, huu ni mwaka wa pili tangu astaafu.

Tuache kulalamika.
 
Hoja zako zina maslahi kwa taifa japo we Kinyonga, lakini viongozi wetu hawapo kwa maslahi ya taifa, wanajali zaidi maslahi ya familia zao.
 
Huku Mwendo wa kupeana vyeo tu ,huo ufanisi utatoka wapi?
 

Attachments

  • Screenshot_20230607_161949_Twitter.jpg
    95.2 KB · Views: 4
Tukisema bora mkoloni mweupe angebaki for a while tunaambiwa tuna akili mgando na za kikoloni!! Tatizo wabongo hatupend kuambiwa ukwel kwa failure zetu, but kabla ya yote tungepata utawala tofaut na CCM ili tupime. Then tukifail bas tujue kua mfumo wetu usha fail na tunahitaj tena wakolon warud!!
 
Wewe always siyo critical, balanced and sophisticated thinker. You are always quick to start bullshit threads in support of whatever stupid decisions by the government, however nefarious the consequences might be. Unakuja na hoja zisizo na mantiki. Hiyo ya Bandari ya Rotterdam inakuja wapi wakati DP World kupewa uendeshaj wa Dar Port ni wapi kulikuwa na Open Tender?
 
Even I have wondered if there is no tender announced, which means this contract is shrouded in great secrecy without transparency.
 
Paskali, nakubaliana nawe. Serikali hii ya kwetu haiwezi kufanya jambo lolote ambalo mafanikio yake hyamliwa na ufanisi.

Sisi tunachoweza sana ni porojo na majungu lakini kwenye mipango inayohitaji weledi, hakuna hata moja inayoliweza.

ATCL, SGR, BANDARI, TANESCO, na HOSPIRALI YA TAIFA MUHIMBILI, kama taasisi hizi zitaendelea kumilikiwa na kuendeshwa na Serikali, tena Serikali hii hii ya CCM, kamwe haitakuja kutokea hata mara moja kuwa na ufanisi wala kuja kutengeneza faida.

SGR inakula pesa nyingi, itakamilika, lakini itakapokuja kuanza kufanya kazi, kwa ukiritimba na upeo mdogo wa waendeshaji chini ya Serikali, watu wataendelea kusafiri kwa mabasi,na mizigo itaendelea kusafirishwa na malori.

ATCL itaendelea kutengeneza hasara milele, TANESCO itaendelea kutoa huduma kwa ugoigoi kama ilivyo sasa, haitatengeneza faida, haitakuja kutoa huduma kwa ufanisi, na milele itaendeshwa kwa ruzuku za walipa kodi.

Hizi taasisi zote ni aheri kuzikabidhi kwa sekta binafsi au kuajiri menejimenti ya kutoka nje ya nchi kama walivyofanya waarabu kwa shirika lao la Emirates ambalo kwa miaka mingi liliendeshwa na wazungu, na sasa wamefanikiwa.
 
Mengi nakubaliana nawe lakini natofautiana nawe kwenye statement yako kuwa eti nchi tumebarikiwa sana. Mimi naona nchi hii tjmelaanika sana maana mengi ya yanayofanyika yanaashiria upungufu wa uwezo wa akili, na ukikosa akili, hata ukasogezewa kila kitu mpaka miguuni, bado hutaweza kufanya chochote. Na ndicho kinachotokea kwa nchi yetu.
 
Mkuu sio laana, viongozi wetu wanachokifanya wanajua, maslahi yao kwanza na familia zao, sisi wananchi ndio tumelala kwa kukosa akili ya kuchukua hatua.
 
Kwa sisi wanainchi sawa ila kwa viongozi wetu wanajua wanachokifanya ni kwa maslahi yao na familia zao ila sisi wanainchi ndio hatuna akili kwa kushindwa kuchukua hatua.
 
Mkuu sio laana, viongozi wetu wanachokifanya wanajua, maslahi yao kwanza na familia zao, sisi wananchi ndio tumelala.
Mzee Bams umeibukia huku? Kwa hiyo unakubaliana na Paskali kwamba Bandari ya Dar wapewe Waarabu wa DP World bila zabuni ya wazi? Hiyo Mou kati ya Serikali na DP World ipo wapi? Kwanini haiwekwi wazi?
 
Asee sikumaliza kusoma,nimeishia pale uliposema hata ATCL na SGR tuingie ubia.

Nasema hivi,kama kuna watu mnaoweza kusababisha risasi kurindima,wewe ni mmoja wapo.

Hii hii ATCL iliyokuwa na wabia wakafilisi ndege zilizokuwepo?

Hii TRC waliyoingia ubia na wahindi wakaua kabisa shirika kabla hawajatimuliwa?


Je kwa nini kujaribu kupima kiasi hiki uvumivu wa watanzania?

Kama kuna ulazima wa kuingia ubia,kwa nini ndege zilinunuliwa kwa pesa ya watanzania tena cash?Halafu aje mtu ale faida atuachie maelezo matupu?
 
Mi namanisha uwepo WA natural resources.
 
u RAIS mtamu sana ila hii dunia hamna cheo na kazi ngumu kama ya RAIS

Huu ni ukweli mchungu sana,RAIS wetu wa sasa ndie RAIS alieonyesha waziwazi

kunyoosha mikono juuu kwamba yamemshinda,nchi haiwezi,nchi imemuelemea

kwa ufupi ni kwamba bado uwezo wa kusimamia vitu vyetu tunao ila shida ni hao wasimamizi

yani hii nchi ukiwa rojo rojo huwezi ongoza kitu kikaenda,Eti unasema "HILI MKALITIZAME" nyooooo

Haina cha kutizama ni hapo hapo Vua watu shanga piga chini,vitu viko wazi kweupe unawambia watu wakalitazame

watizame nini? waangalie nini? kama sio kutengeneza tu mazingira mengine ya watu kujilia pesa,Matokeo ni UOZO.

Bana muarubaini wa haya yote sio kuwapa watu watusaidie,ni Umagufulication mwingine utokeee maisha yaende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…