Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

H
Ni Bora kumlipa mshahara mrefu ceo WA kukodi au wataalamu wa kuongeza ufanisi kuliko kuikabidhi bandari Kwa waarabu.

Mali asili zote zitasombwa na kupelekwa kwao na ninyi mtabaki kuwa mbwa Kwa kupewa mifupa na minofu na vizawadi vya ist vitaimaliza nchi wapenzi muje muone.
 
Bandiko safi sana Paskali,
Chanzo cha haya matatizo, ni mifumo.
1. Mifumo ya Elimu, haimwandai mwanafunzi kukabili matatizo yake, bali humwandaa aajiriwe.
Mifumo ya elimu erekebishwe iweze kuandaa watu wanaoweza kujitawala kutengeneza ajira.

Kama intake zote za madarasa kuanzia kipindi cha uhuru 1961 kinaandaa watu wa kuajiriwa na si wa kutengeneza ajira, unategemea nani atengeneze hizo ajira?

Na ndiyo maana hata mambo madogo kama bandari tunakosa pumzi ya kuiendesha, kwa sababu elimu yetu haikutuandaa kujiongoza, imetuandaa kuongozwa.

viongozi na serikali ni zao la elimu inayofundisha kuajiriwa, hivyo ni ngumu sana wao kuweza kuwa na ujuzi wa kuendesha mambo zaidi ya ku-opt kuendeshewa.
 
Laana ya wizi wa kura haiwezi kuiacha nchi salama hata kidogo. Siku tukipata utawala unaotokana na matakwa na ridhaa ya wananchi laana hii itaondoka. Watawala wetu wanapata kibri kwa vile wameshajiwekea mfumo ambao hata wakivurunda sisi wananchi hatuna cha kuwafanya. Watawala wanaotokana na kura(ridhaa) ya wananchi huwa wanajihadhari na matendo ya hovyo kwani wanajua kuwa wananchi wanayo fimbo ya kuwapigia yaani kuwakataa kwenye sanduku la kura,lakini CCM wameshajiwekea mfumo ambao sanduku la kura halina maana yoyote. Na hapa ndiyo umuhimu wa Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi unaonekana.
 
Ni wananchi wangapi wanaijua katiba iliyopo? idadi ya wenye uelewa wa katiba ikifikia idadi wa mashabiki wa Diamond na Zuchu, hapo itawezekana kufanya mabadiliko.

Tuhamasishane kuwa Serious na mambo ya msingi yanayohusu taifa, huu utakuwa mwanzo mzuri sana.
 
MASHIRIKA ya muhimu tumeyaua wenyewe,,, Sasa mbona Bandari mnaishikilia bango sana 😂😂😂.. Nayo iuzwe tu Wapiga Dili na Wapeana Ajira watafute Chaka lingine..
 
Sisi hatukatai kusaidiwa, yaani ubia wa tupate wote tukose wote. Yaani ni sawa na jamaa kundoka na bakuli zima la mboga, kuna kula ugali hapo ndugu zangu.
 
nauliza tu hivi kuna sehemu au siku Pascal keshawahi kutoa uzi wa kuikosoa Serikali?
 
Operesheni +255 inaifanya kazi hii, tuunganishe nguvu katika hili vinginevyo watawala hawa wataendelea kutuchezea
 
Mjumbe Paskali una stayili ya mishmash, inachanganya mazuri na mabaya, chuya na pumba, kenge na nyoka, halafu unaweka conclusion moja. Azorygwanda aliuliwa na UAMSHO kwa kutumiwa na magazeti ya Kenya kupata breakingnews, Ben alitekwana kuuliwa na squad toka Mara wamesema Dr. Slaa na Dr. Mollel. Yale mengine ni sawa, kina Kabunda, Mwanahalisi, na ugaidi wa UAMSHO na wa Mbowe, hayo ni sawa.
 
Mradi wa mabus ya mwendokasi wamechelewa sana ilitakiwa hata Jana
 
Waarabu baada ya kuona hawawezi kuisimamia miradi Yao ya kiuchumi Kama waafrika wakaona ni afadhari wawaachie wazungu waendeshe shuguli za uchumi Leo wapo bandari
 
...Unauma na kupuliza....umeshauri sio vibaya kuomba msaada ukishindwa ila hujaafiki msaada wa nje kabla ya kuanzia ndani.....au nimekuelewa vibaya ?.…🤔🤔
 
Ni kweli watanganyika hatuwezi kumuua mtu mmoja tu anayetaka tuwe bandariless
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…