Watanzania tujiulize: Ikiwa sisi ndiyo wenye mali, nini kinatukimbiza nje kutafuta wa kuja kuzila (eti kuwekeza)?

Duu kazi ipo ..
Mkuu unahisi umeandika vitu gani apo.
Upo sawa kabisa hujatumia kilevi chchte.
 
Kuwa na shukrani mkuu. Tambua mchango wake wa kupigania uhuru na kuijenga Tanzania yenye umoja wa kitaifa.

Hakuwa Mr.Perfect ila toa walau appreciation ya mazuri aliyofanya.
Wapo walopigania uhuru wakamwaga damu zao, yeye alikaribishwa tu....
 
Huna mbadala uliotoa hapo, kwani mafundi sonara sio wafanyabiashara? popote walipo, unataka kuniambia hao wawekezaji (kama vile mafundi sonara wahindi) sio wawekezaji? Ondoa utindio wa mawazo.
Ni nani kati yangu na wewe mwenye utindio wa mawazo?

Hivi ulisoma na kuelewa nilichoandika?

Hivi kwa akili yako unaweza kuyatumia madini yote yaliyopo nchi hii kwa kutengeneza vito vya thamani ambavyo huwezi kuuza kokote zaidi ya Tanzania?

Na hata ikitokea hivyo, unaelewa hata lile neno Vito vya Thamani litakuwa halina maana tena kwa sababu 1kg of gold inaweza kuuzwa hata kwa Sh 100K?

Na kama 1kg ya gold inaweza kuuzwa kwa bei rahisi kwa sababu haina soko, ni nani basi atawekeza billions kwenye uzalishaji wa bidhaa isiyo na thamani?!

Acha kukurupuka na kukimbilia ku-comment... anza kwanza kuelewa hoja ili nawe ujibu kwa hoja badala ya viroja!
 
xx
Hili la "kususia" limetoka wapi, kama si kuchanganya na kuvuruga mada ambayo iko wazi kabisa inachozungumzia.
Man,

Soma kwa makini kisha digest! Hakuna nilichochanganya hapo unless kama ulitaka niongee moja kwa moja bila kutoa changamoto ya watu kutafakari nilichosema!

Mleta mada anasema:-
Sikubaliani kabisa viongozi kuzunguka dunia nzima kuomba pesa na uwekezaji. Tunajidhalilisha!
Like serious?!

Canada ni Developed Country lakini kwa miaka sasa Canada wana-issue Investor Visa. Ukiwa na minimum of $200K, Canada wanakupa ama status ya PR au hata uraia kabisa.

Na sio Canada tu... karibu nchi zote duniani, maskini kwa tajiri, zinafukuzia FDI.

Yaani nchi zenye higher purchasing power and larger consumer markets bado zinatafuta foreign investors ije kuwa ka-nchi maskini kama Tanzania?

Nchi kama China inaweza isihangaike sana kutafuta Wawekezaji kwa sababu soko lake kubwa ambalo ni la medium income tayari ni kivutio tosha kwa mwekezaji yeyote kwenda China kuwekeza!

What about you? Hivi cha maana hasa mlichonacho ni kipi? Madini yaliyokuwepo ardhini? NImetoa mfano wa madini kwa sababu ndio yanatupa kiburi sana Watanzania kwa kujiona ni matajiri sana wakati madini katika dunia ya leo si lolote si chochote!

Au gas iliyopo more 100KM kutoka ufukweni huku gesi yenyewe ikiwa more than 1KM below the sea level?

Hivi huo utajiri unaowapa kiburi cha kudhani watu watakuwa wanawafuta tu ni utajiri upi hasa?!

Wale nyumbu wasiojua hata kwamba maji ni hatari kwa maisha yao?!

Your utajiri is nothing unless you know how to convert it into money!! And you can't convert it into money unless you've enough capital, required skills, and the market!!

Niwakumbushe tu kwamba gharama za LNG Processing Plant peke yake pale Lindi ni $30 Billion. Bajeti ya nchi yetu tajiri ambayo inaingia hasa kwenye mipango ni less than $15 Billion kwa mwaka!!

Hiyo ndo nchi tajiri ambayo watu wake hawaoni umuhimu wa kutafuta wawekezaji!!

Na ndo hao leo hii nawauliza, assume madini yetu na bidhaa zake vinakataliwa duniani kote... je, dhahabu ile Tanzania Tajiri tutaifanyia nini?! Ile Tanzanite matajiri sisi tutaifanyia nini!!

Jibu la madini hayo yatafanyiwa ndipo utakapoona umuhimu wa wawekezaji kutoka nje!
 
Hata we tofautisha kuzila na kuwekza. Wakiwekeza we ndo unakula na wao pia. Na inafanyika hivyo kwa sababu huna uwezo wa kuwekeza. Mpaka hapo ulipo sidhani hata laki Kama unayo
mimi nina elfu 86 kwenye akaunti
 
Contents za subject matter unayojaribu kuadress ni bayana,lakini"Approach" yetu Ina kizungumkuti. Bado nasisitiza"Tujipime" tukae tupange tunachohitaji kama nchi,kabla ya"kufukuzia" kama ulivyosema fursa za wawekezaji na uwekezaji. Haraka ya nini? Tumepata Uhuru miaka 60 plus iliyopota,hatukujua population ya watu inaongezeka,leo tukurupuke hatuna madawati au madarasa? Na je,tutakopea vingapi endapo hata chaki ya mwalimu ni ya mkopo?
Juzi hapa,Mama yetu kaleta fedha za madarasa na madawati,umeona ilivyotumika nguvu kubwa kutetea hoja yake kwa wananchi! Wananchi wanasema nchi imejaa misitu kedekede ya kutengeneza madawati,leo wanaingizwa madeni kwa kofia ya Covid-19bila sababu za msingi!!!.
Unapomleta mwekezaji wa nje kwenye nchi,unatengeneza ajira 10,unavuruga 100 na za kudumu endapo kazi hiyo ingefanywa na sie wenyewe. Hilo liko wazi na mifano ipo!! Sera zetu za fedha hasa za mikopo ya nje haziko bayana!! Kila kiongozi anatumia "approach" tofauti hasa kujikwezea na kuunda"minorities" wa kumsemea , hapa Ina walakini. Mara nyingi imeonekana kwa nchi nyingi manufaa yake hayawezi kukuza uchumi ndani ya muda muafaka,pale mkopo unapolenga huduma za kijamii,. Kwani muda wa kurejeshwa tungeacha haraka,kwa nguvu za wananchi na "rasilimali "zilizopo hiyo kazi ingekuwa imeisha bila kuiminya jamii kufaidisha wageni.
Nina maono makubwa na Nchi yangu,tusijione wanyonge,na tusijidekeze,tunaweza. Kumchukua Mwarabu Oman kuja kuwekeza kilimo cha Zabibu ni fedheha kwa Taifa!
Nimetumia lugha nyepesi nieleweke.
 
Bandiko bora kabisa lkn kwasababu kuna watu wamejitoa ufahamu kwasababu ya njaa ya matumbo watakuja na hoja za kukosoa badala wajiulize na kachangia hoja
 
Hakuna wa kulaumiwa zaidi ya wewe unayelaumu.
 
Huna haja ya ku panic mkuu. Kunywa maji upunguze jazba.
 
Bondo,
Ili kurahisisha, naomba uweke maana ya mwekezaji, sonara, na mfanyabiashara.
Tukiweza kujulishana hapo tutaendelea.
Hapo juu unadai Tunaongelea, wewe na nani? nimechanganyikiwa nina kujibu wewe, wewe umenijibu mimi? sielewi.
Sijui kama umesoma lizungumwalo katika mada hii na kama ndio vivyo basi sote tumetoka katika mada, turudi kwa kurahisisha, maana ya mwekezaji,sonara, na mfanyabiashara. Pia, Je

Watanzania tujiulize: Ikiwa sisi ndiyo wenye mali, nini kinatukimbiza nje kutafuta wa kuja kuzila (eti kuwekeza)​

 
Kwanza Tanzania hatuna rasilimali za thamani kama tunavyoaminishana utasikia eti tuna mito, mabwawa, ardhi, madini, wanyama pori, maziwa ni rasilimali sawa ila hazina thamani kama tunavyoaminishana.
Daah ! Ungefafanua vizuri ingependeza. Kwamba madini ya Tanzania hayama thamani kushinda ya Congo au Ghana ? Wanyama pori wa TZ hawana thamani kushinda wa Kenya ? Maziwa, mito na vingine ni hivohivo ? Tafsiri yako ya thamani ni ipi ?
 
Amini usiamini Chige hata mimi huwa napata utindio wa mawazo.


Nilikusoma, na nilivyoelewa nikuwa haukuwa na mbadala pale juu.

Kwahili ninanukuu "

Hivi kwa akili yako unaweza kuyatumia madini yote yaliyopo nchi hii kwa kutengeneza vito vya thamani ambavyo huwezi kuuza kokote zaidi ya Tanzania?"

Hapo juu sijakuelewa. Ni uhakika kuwa katika mada hii jambo kuu ni wawekezaji, sasa kama maana yake ni kuchimba madini peke yake basi tuelimishane. Hata jembe laweza kuchimba.

Viroja gani hivyo, punguza jazba.
 
Hivi kumbe kuna watu walikuwa wanaamini yale maneno ya Jiwe
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Wewe ulitaka tuamini maneno ya nani?.kama hukuweza kuamini maneno JPM hata maneno anayotoa Rais wa sasa hutaamini pia
 
Uzi murwaaa lakini naona watu wanamshambulia mtoa mada

Ova
 
Daah ! Ungefafanua vizuri ingependeza. Kwamba madini ya Tanzania hayama thamani kushinda ya Congo au Ghana ? Wanyama pori wa TZ hawana thamani kushinda wa Kenya ? Maziwa, mito na vingine ni hivohivo ? Tafsiri yako ya thamani ni ipi ?
Mfano madini yapo ila ni kwa uchache sana huwezi kuendesha serikali ya Tanzania kupitia rasilimali zake hata kwa nusu tu. Kuna inchi zina rasilimali kiasi hata haziitaji kodi kujiendesha.
 
Mkuu 'Chige', sishangai hata kidogo juu ya 'mentality' yako hii potofu, kwa sababu nilishakusoma vya kutosha tokea enzi za Bagamoyo.

Kididimo hajakataa uwekezaji, na sijaona popote mtu yeyote akikataa uwekezaji Tanzania. Lakini uwekezaji hauwezi kuwa ndio mbadala wa juhudi za wananchi na serikali yao kujiletea maendeleo yao. Hakuna nchi yoyote iliyopata maendeleo eti kwa sababu wawekezaji wengi toka nje ndio wameleta maendeleo hayo.

Serikali, na viongozi hawa wana wajibu mkubwa sana kuwaelewesha watu kama wewe wasilaze akili zao kwa kudhani kwamba tutaendelea kwa vile tumejiuza sana kwa wawekezaji, kujiuza hata kunakodhalilisha utu wetu!

Inashangaza kidogo hata kutoweza kutambua kwako kwamba uwekezaji si wa kutoka nje ya nchi pekee. Wananchi wetu hata kama hawana uwezo wa hayo mabilioni ya kuweka kwenye gesi, lakini kwa juhudi zetu tunao uwezo mkubwa sana wa kubadilisha maisha yetu wenyewe bila hata hiyo gesi au madini; na kwa kufanya hivyo hao hao wawekezaji unaowalilia wataona soko la uhakika hapa nchini na kuleta uwekezaji wao.

Serikali na viongozi hawa hawawezi kudumaza akili za wananchi wetu kuamini kwamba hatuwezi kuchangia kwa kiasi kikubwa zaidi katika kubadilisha maisha yetu, eti lilobaki ni kusubiri uwekezaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…