xx
Hili la "kususia" limetoka wapi, kama si kuchanganya na kuvuruga mada ambayo iko wazi kabisa inachozungumzia.
Man,
Soma kwa makini kisha digest! Hakuna nilichochanganya hapo unless kama ulitaka niongee moja kwa moja bila kutoa changamoto ya watu kutafakari nilichosema!
Mleta mada anasema:-
Sikubaliani kabisa viongozi kuzunguka dunia nzima kuomba pesa na uwekezaji. Tunajidhalilisha!
Like serious?!
Canada ni Developed Country lakini kwa miaka sasa Canada wana-issue Investor Visa. Ukiwa na minimum of $200K, Canada wanakupa ama status ya PR au hata uraia kabisa.
Na sio Canada tu... karibu nchi zote duniani, maskini kwa tajiri, zinafukuzia FDI.
Yaani nchi zenye higher purchasing power and larger consumer markets bado zinatafuta foreign investors ije kuwa ka-nchi maskini kama Tanzania?
Nchi kama China inaweza isihangaike sana kutafuta Wawekezaji kwa sababu soko lake kubwa ambalo ni la medium income tayari ni kivutio tosha kwa mwekezaji yeyote kwenda China kuwekeza!
What about you? Hivi cha maana hasa mlichonacho ni kipi? Madini yaliyokuwepo ardhini? NImetoa mfano wa madini kwa sababu ndio yanatupa kiburi sana Watanzania kwa kujiona ni matajiri sana wakati madini katika dunia ya leo si lolote si chochote!
Au gas iliyopo more 100KM kutoka ufukweni huku gesi yenyewe ikiwa more than 1KM below the sea level?
Hivi huo utajiri unaowapa kiburi cha kudhani watu watakuwa wanawafuta tu ni utajiri upi hasa?!
Wale nyumbu wasiojua hata kwamba maji ni hatari kwa maisha yao?!
Your utajiri is nothing unless you know how to convert it into money!! And you can't convert it into money unless you've enough capital, required skills, and the market!!
Niwakumbushe tu kwamba gharama za LNG Processing Plant peke yake pale Lindi ni $30 Billion. Bajeti ya nchi yetu tajiri ambayo inaingia hasa kwenye mipango ni less than $15 Billion kwa mwaka!!
Hiyo ndo nchi tajiri ambayo watu wake hawaoni umuhimu wa kutafuta wawekezaji!!
Na ndo hao leo hii nawauliza, assume madini yetu na bidhaa zake vinakataliwa duniani kote... je, dhahabu ile Tanzania Tajiri tutaifanyia nini?! Ile Tanzanite matajiri sisi tutaifanyia nini!!
Jibu la madini hayo yatafanyiwa ndipo utakapoona umuhimu wa wawekezaji kutoka nje!