Watanzania tujiulize: Ikiwa sisi ndiyo wenye mali, nini kinatukimbiza nje kutafuta wa kuja kuzila (eti kuwekeza)?

Watanzania tujiulize: Ikiwa sisi ndiyo wenye mali, nini kinatukimbiza nje kutafuta wa kuja kuzila (eti kuwekeza)?

Kwanza Tanzania hatuna rasilimali za thamani kama tunavyoaminishana utasikia eti tuna mito, mabwawa, ardhi, madini, wanyama pori, maziwa ni rasilimali sawa ila hazina thamani kama tunavyoaminishana.

Kabisa mkuu, raslimali zipo ila thamani yake ni ndogo sana.
 
Hata new genaration ikiingia kwa Tz bado shida ipo palepale maana hiyo new generation yenye kuingia kwenye system ni watoto na wajukuu wa walewale walioshindwa.wana mind set zilezile za baba zao na babu zao.wazungu wezetu wanaangalia capacity ya m2 kuliletea Taifa maendeleo ndo maana akiba Obama wameweza kuwa Rais marekani m2 mwenye asili ya kenya ila Afrika vitu kama hivi haviwezi kutokea wanaangalia mtoto wa nani? Baba yake au babu yake aligombania uhuru?.JPM alipoingia na watu wake wakaambiwa sio ccm halisi na wengine kuitwa makokoro ndo utagundua hawaangalii perfomance ya m2 wanaangalia mtoto wa nani?.kwahiyo usitegemee kuona mabadiliko chanya kwa hiyo new generation.
Umenielewa.
 
na maana ya "maneno" na "blaa blaa" unajua??!!
Nilifikiri una hoja, wake up man!
HaIwezekani kama Kiongozi utuoni wote tuna akili kama za ndugu zako uliowateua kisa ulaji,never on earth! Tanzania tuna watu competent kuwekeza au kuzalisha Ajira kuliko unavyofikiri !??
Inakuwaje leo u amuuzia mtu Kitalu cha kuzalisha mifugo, keshokutwa anaanza kuuza mifugo nje,ilhali wewe kwa miaka 40 ulishindwa? Hiyo nayo inahitaji Mzungu?.
Tujipime.
 
Hao wabunge watoe kabisa hapo kwenye list,tusiwategemee hao kabisa kabisa.
 
Tulimtumia nani hapa nchini kupata hizo options? CCM?,Bunge? Vyama?, Vyuo vikuu na wasomi wao? Je, na wao wanatumia kina Nani kuziona hizo option tena nchi sio yap? We are wrong somewhere.
Sema hata hapa hapa.... huwezi jua nani anaona.
 
Inasikitisha sana ati leo hii tunatafuta hadi wawekezaji wa sekta ya KILIMO...kweli kweli watanzania..?
yaani miaka 60 ya uhuru wetu hata kilimo nacho tunatafuta watu wa kuja kutufundisha...we're not serious aisee !!

Haya ngoja waje wachukue mapori yote ya akiba tubakie mjini kuuziana soksi.
 
Watanzania wenzangu, kuna kitu hakiko sawa!

Tutachanganyiwa lugha zote kuwa tunafungua nchi kumbe kuna hila ndani yake.

Sikubaliani kabisa viongozi kuzunguka dunia nzima kuomba pesa na uwekezaji.
Tunajidhalilisha!

Tuna bunge, Mawaziri, Wasomi, Wanasiasa, Wafanyabiashara maarufu nk,tumeshindwa kutulia na kukipanga hata iwe miaka 100 ijayo tukaijenga nchi yetu wenyewe? Hiyo haraka ni ya nini?

Wazee wetu kina Warioba, Msekwa, Malecela, Msuya nk niwaulize, mmekubali wajukuu zenu na elimu zao kuwa manamba wa Wazungu? Ndivyo hivyo Mwl. Nyerere aliwausia? Vijana,wajukuu zenu serikali iliwasomesha hadi vyuo vikuu ili wawe ombaomba duniani? Au waendesha bodaboda tuu na siyo kusimamia rasilimali zetu?

Ni kwa nini kila Rais aingiapo tunaruhusu alete mambo yake mapya na siyo kuendeleza ya mtangulizi au yaliyoasisiwa na nyie wazee wetu?

Mwl. Nyerere alituachia rasilimali tuzitumie kujiletea maendeleo au kuzinadia duniani?

Tujitizame.
Unapoteza muda kwa kupiga siasa, dada na kaka zako wanatafuta kazi kupitia hayo makampuni ya wawekezaji.Achana na hizi fikra za kurithishwa na wanasiasa, ubongo wako na usimame wenyewe.
 
Tumezuia "Vipaji" tunaenda kuvitafuta nje, hivyo siyo vyetu!!!! Tusijidanganye. Viongozi wanaokotezana kindugu wanadanganyana kutafuta" mjomba feki" kuwa atawasaidia, huyo mjomba ni mjinga? Hatusomi Historia? China,Vietnam,Indonesia,Malaysia,Brazil kwa uchache waliwezaje? Vijana wenye uelewa wapo, tujenge maono ya mbele tuwawezeshe kwanza Hawa. " The time is coming when all stupid minds will be uprooted,and the facts open " Haiwezekani Wazazi wetu watuachie mali tutapanye kwa kukosa maarifa! Hilo nalikataa.
Pengine kabla hujazaliwa wewe wazee wetu kina Nyerere walihubiri kujitegemea kinadharia lakini kivitendo walishindwa.

Ni dunia ya kutegemea, punguza maumivu ya kichwa yasiyo na sababu.
 
Tz tunazalisha Tanzanite,makaa ya mawe,gas,Dhahabu,Alumas,Rubi na madini yakutengenezea jipsum marumaru na makighafi za miti huku Iringa zote hizi zinaenda nje kama hujuwi.Enzi za awamu ya nne zilikopa hela zatengenezea kiwanda cha mbolea Lindi kila kikawa tayari hela zikaliwa na kiwanda hamna hadi leo.JPM aliwahi kulisema hili kwenye hutuba zake.hakuna uwekezaji hapo wanatafuta watu wajusimamia mambo yao na biashara zao kwa kivuli za uwekezaji.Mkapa na kikwete waliimba na kuzunguka uwekezaji hakuna impact yoyote tuliona.Bora JPM aliyejimbanunua kwa dhana yakujitegemea na tuliona impact kwa nchi alifanya mambo mengi mazuri.
Mkuu usimfananishe Samia na JPM, kila rais anayo haki ya kupita njia anazoona zinaifaa Tanzania. Kipaji alichokuwa nacho JPM Samia hana.

Kipaji alichonacho Samia JPM hana, hivyo msitake kulazimisha hisia zenu za kumpenda JPM ndizo hizo hizo zimeongoze Samia, mnatwanga maji kwenye kinu, mnapoteza muda.
 
Watanzania wenzangu, kuna kitu hakiko sawa!

Tutachanganyiwa lugha zote kuwa tunafungua nchi kumbe kuna hila ndani yake.

Sikubaliani kabisa viongozi kuzunguka dunia nzima kuomba pesa na uwekezaji.
Tunajidhalilisha!

Tuna bunge, Mawaziri, Wasomi, Wanasiasa, Wafanyabiashara maarufu nk,tumeshindwa kutulia na kukipanga hata iwe miaka 100 ijayo tukaijenga nchi yetu wenyewe? Hiyo haraka ni ya nini?

Wazee wetu kina Warioba, Msekwa, Malecela, Msuya nk niwaulize, mmekubali wajukuu zenu na elimu zao kuwa manamba wa Wazungu? Ndivyo hivyo Mwl. Nyerere aliwausia? Vijana,wajukuu zenu serikali iliwasomesha hadi vyuo vikuu ili wawe ombaomba duniani? Au waendesha bodaboda tuu na siyo kusimamia rasilimali zetu?

Ni kwa nini kila Rais aingiapo tunaruhusu alete mambo yake mapya na siyo kuendeleza ya mtangulizi au yaliyoasisiwa na nyie wazee wetu?

Mwl. Nyerere alituachia rasilimali tuzitumie kujiletea maendeleo au kuzinadia duniani?

Tujitizame.
Kutokuwajibika kwa waliojipa uongozi pasina malengo mapana na wasio wabunifu.Badala ya kutafuta njia shirikishi ili kuzitumia raslimali zetu.Tangia awamu ya 5 iingie madarakani kimagumashi ndipo teuzi nyingi zilipoegemea kwa maDR na maProfesor,lakini kwa kukosa kwa ubunifu tukashuhudia deni la Taifa likipaa kwa kiwango karibia au sawa na deni la awamu zote zilizotangulia.
CCM hata ingeongozwa na malaika anaweza kufanya mabaya kuliko shetani mwenyewe.Tunavutia wawekezaji kutokea enzi za Mzee wa Lupaso lakini nchi ndiyo inazidi kudidimia.
Tatizo la Tanzania ni aina ya viongozi wabovu wanaopatikana kwa njia ovu na wenye tamaa za kujineemesha wao na ndugu/jamaa zao kwa miaka yote nasi wananchi kukosa njia mbadala ya kuwaondoa.Sheria na Katiba mbovu ni kikwazo kikubwa.
Tusipobadilika na kupigania mabadiliko sisi wenyewe,tusitarajie mapya.
 
Brains... (lack of)

Brainwashed (kuthamani vingine / vya nje)

Not being serious (kutengeneza / kufanya vitu vyenye mediocre quality)

Investing on wrong things (wakati wengine walitumia nguvu sana ku-invest kwenye research, development na kuwezesha watu wao) sisi tunawekeza kwenye kujaza ujinga...

Marginalization na Developed Countries kuzibana nchi kama zetu ili tuendelee kuwa wazalishaji wa malighafi na watumiaji wa their junks products...
 
Mkuu usimfananishe Samia na JPM, kila rais anayo haki ya kupita njia anazoona zinaifaa Tanzania. Kipaji alichokuwa nacho JPM Samia hana.

Kipaji alichonacho Samia JPM hana, hivyo msitake kulazimisha hisia zenu za kumpenda JPM ndizo hizo hizo zimeongoze Samia, mnatwanga maji kwenye kinu, mnapoteza muda.
Hapo ndio kosa la sisi kuwa hapa tulipo...., No one is clever / bright than all of us...., Kumpa mamlaka mtu mmoja ndio achague nini cha kufanya au njia gani za kupita ni matumizi mabaya ya Human Resources..., Wadau na Wataalamu inabidi wachague njia Rais ni kusimamia tu....
 
Hizi ndio akili za waafrika, anaamini hawezi kuwekaza na wala hawa hawezi pata mtaji, hivi akili wao walitoa wapi hao wazungu mnaoenda kuomba,? Kama ni technology hawakuiokota, walisoma, maanake elimu Bora ndio umewasaidia kupata technology, nyie elimu yenu ikoje? Yani huwa hatuwezi kuona mambo zaidi ya urefu wa pua.

Basi someni historia ya nchi zingine waliwezaje? Singapore waliwezaje na ni kisiwa? Ndio nchi yenye watu wenye IQ kubwa duniani,
Watu wanakufa kwa njaa hata chai ya asubuhi shida. Sasa immediate rescue imekuja utafikilia hayo yote!!!
 
Tunakimbizana na maisha bwashee. Inawezekana we umesukumwa na ubinafsi tu kuandika haya lakini kumbuka watanzania Ni wengi maskini wanatafuta ajira. Laiti ajira au serikali ingekuwa na uwezo wa ku accommodate watanzani wote hakuna haja ya uwekezaji kutoka nje lakini ujue hata marekani ndani kwao Kuna wawekezaji wengi kutoka china, urusi n.k. Hivyo siku nyingine ficha ujinga wako
Mtoa mada yupo sahihi kuuliza hilo alilohoji.Nchi hii ina mipango ya zimamoto na umaskini wa fikra.Tuna madini,bahari,maziwa,mito yenye kutiririsha maji,ardhi yenye rutuba,watu wenye nguvu nk ambapo kasoro kubwa zipo katika uongozi bora.Kubali kataa ila huo ndiyo ukweli.
 
Watanzania wenzangu, kuna kitu hakiko sawa!

Tutachanganyiwa lugha zote kuwa tunafungua nchi kumbe kuna hila ndani yake.

Sikubaliani kabisa viongozi kuzunguka dunia nzima kuomba pesa na uwekezaji.
Tunajidhalilisha!

Tuna bunge, Mawaziri, Wasomi, Wanasiasa, Wafanyabiashara maarufu nk,tumeshindwa kutulia na kukipanga hata iwe miaka 100 ijayo tukaijenga nchi yetu wenyewe? Hiyo haraka ni ya nini?

Wazee wetu kina Warioba, Msekwa, Malecela, Msuya nk niwaulize, mmekubali wajukuu zenu na elimu zao kuwa manamba wa Wazungu? Ndivyo hivyo Mwl. Nyerere aliwausia? Vijana,wajukuu zenu serikali iliwasomesha hadi vyuo vikuu ili wawe ombaomba duniani? Au waendesha bodaboda tuu na siyo kusimamia rasilimali zetu?

Ni kwa nini kila Rais aingiapo tunaruhusu alete mambo yake mapya na siyo kuendeleza ya mtangulizi au yaliyoasisiwa na nyie wazee wetu?

Mwl. Nyerere alituachia rasilimali tuzitumie kujiletea maendeleo au kuzinadia duniani?

Tujitizame.

"uomba pesa na uwekezaji" Unapotosha pesa za uwekezaji haziombwi kwasababu sio za serikali. Serikali inahimiza uwekezaji na hii inatokea kila mahali. Huku nje mfano hapa USA hata miji na majimbo yanafanya hivyo hapa Texas Governor wetu anaenda California kujaribu kuwashawishi wawekezaji waje hapa.
 
Back
Top Bottom