Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
- #81
Suala la watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha na wengine kutekwa na kukutwa wamekufa kama ilivyotokea kwa Mzee Ally Kibao ni mambo makubwa yanayogusa hisia za watu wote na yanayopaswa kukomeshwa mara moja na wahusika kukamatwa na kufikishwa mahakamani. Lakini sote ni mashuhuda wa namna Rais wetu alivyoguswa na kukemea vikali sana na kuagiza uchunguzi wa kina ufanyike juu ya matukio hayo.Lucas, jitafakari sana, na ujiulize kama upo kwenye upeo wako halisia. Yaani watu kutekwa, kupotezwa na kuuawa kwa sababu tu ya ukosoaji, unasema ni changamoto ndogo ndogo? Kama kupotea kwa maisha ya watu ni mambo madogo madogp, kwako mambo makubwa ni nini?
Mimi sifikirii muda huu ni wa kumwondoa Rais madarakani, na sidhani kama kuna anayelidhamiria hilo. Lakini kwa sababu jukumu la msingi kuliko yote kwa serikali yoyote Funiani ni usalama wa raia, na kwa vile Rais Samia ameshi dwa kwenye hili la msingi, tumpe muda amalizie muda wake wa Urais wa kikatiba, mwaka 2025 tumshukuru alipotufikisha, aende akapumzike. Lakini ni muhimu zaidi, katika kumpata Rais mwingine, tuwe makini sana, isije ikawa huu ushetani wa sasa ukaendelea au ukawa mbaya zaidi ya huu wa sasa. Rais ni mtu mmoja tu, lakini kwa katiba yetu hii mbaya, Rais anaweza kuwafanya muishi kama binadamu, au muishi kama nyumbu katikati ya simba, kama ilivyo sasa.
Hata upande wa chama changu yaani CCM nacho kimekemee vikali sana na kuonyesha kuumizwa na kukasirishwa sana na matukio hayo. Kwa hiyo ndugu yangu Bams napenda kusema kuwa Masuala ya utekwaji na kupotea kwa watu hakuungwi mkono ndani ya chama na ndani ya serikali