Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme, hivi ni ujinga au ushamba?

Electrical engineer hesabu za kWh anazijua kwa Tz, ndio maana anatumia electric cooker kwa kusave gharama. Kongole kwake.

Na kama alikuwa mfanyakazi wa TANESCO kuna bonus wanayopata
​
Amestaafu miaka 15 iliyo pita Sasa ☺️ 😁 ni kweli na sahihi Sanaa
 
Sawa gas imeisha usiku kwa nini usingekuwa na backup ya jiko la umeme?
Pressure cooker za umeme zimechukua nafasi.
  • Unapika kwa muda mfupi zaidi.
  • Matumizi ya umeme ni kidogo ukilinganisha na jiko la umeme.
Na kwa wengine Gas ndio back up, iwapo itatokea umeme hakuna, (Pressure cooker) inasogezwa pembeni, unaweka jiko lako la Gas, Kupanga ni kuchagua kila mtu na chaguo lake.
 
Ila ukienda kununua flat unaangalia tamthilia, movies au soka husemi mara Tanesko wamefanya yao chap.

Ni nani aliyewaroga?
​
Nimeona umeweka bei ila hizo sio bei halisi tunazoziona kwenye receipt...weka gharama halisi, hakuna unit ya tsh 292 kwa watumiaji wa zaidi ya 75kWh, wala tsh 350 unless useme hiyo ndo bei kabla serikali haijatia mkono, ambapo sio halisi sasa!
 
Ni kutokuwa na uelewa sahihi,kama wahusika kama tanesco wangekuwa wanatoa elimu kama ulivyofanya wewe hapa basi wengi wangebadili mitizamo yao ya kuwa umeme ni ghari kuliko gas.
 
Hivi matumizi ya kupikia jiko la Umeme asubuhi chai, mchana ugali na mboga au wali au ndizi, na usiku INAWEZA KWENDA UNIT NGAPI? KAMPUNI GANI YA JIKO NZURI AMBAYO HAILI UMEME SANA, NA PICHA IKIWEPO ITAKUA VIZURI
 
Mbona unaponunua vifaa vingine vya umeme hausemi kwa umeme hautegemeki

Yaani kwenye jiko la umeme tu ndio mnaanza hesabu za umeme wa Tanesco hautegemeki
​
Mkuu tv,redio, jokofu nk vikizima tuasikitika na kukasirika lakini jiko likizima katikati ya kusonga ugali inakuaje? Hata ukikasirika ndo ugali ushadoda na watu mnabaki na njaa
 
Wewe unasema bila kufanya utafiti halisi, mimi ninayo majiko yote uliyoyataja pamoja na maikrowevu, maikrowevu ikifika jioni haifanyi kazi, umeme mdogo na hii ni kila siku. Jiko la umeme nalo ikifika jioni halipati moto unaohitajika kupikia, birika la umeme nalo jioni linatumia muda mrefu sana kuchemsha lita moja ya maji!
Huko nyuma niliwahi kuandika humu kuhusu tatizo la umeme mdogo maeneo mengi ukiacha katikakatika ya zaidi ya mara sita kwa siku, hata hivyo wewe haukuchangia posti yangu.
Hivi ninavyo ila kuvitumia ni mtihani kutokana na umeme kuwa mdigo, sijui utatusaidiaje wewe mtoa ushauri.
 
Umeandika vyema sana!
Na hayo majiko ya watts 1000 n k yanakufa haraka sana.
Jiko imara ni kuanzia 2.5kWh, na TANESCO wanakusubiri ujichanganye kwenye 18 yao.
Uzoefu ni mwalimu nzuri sana
 
Hivi matumizi ya kupikia jiko la Umeme asubuhi chai, mchana ugali na mboga au wali au ndizi, na usiku INAWEZA KWENDA UNIT NGAPI? KAMPUNI GANI YA JIKO NZURI AMBAYO HAILI UMEME SANA, NA PICHA IKIWEPO ITAKUA VIZURI
Chai kama ni maji tumia Jug Kettle; Kila kitu kigumu kuiva tumia pressure cooker na wali tumia rice cooker....;

Tena kama unaweza toka nyumbani kwako asubuhi badika wali kwenye slow cooker 75 to 100 watts (low power) ukirudi jioni chakula kimeiva na chamoto na safi...

Kila kifaa kina power consumption Watts; Ingawa Jug lina 1500 watts; yaani kwa saa linakula units 1.5 (KWH kwahio unagawa kwa 1000 hizo watts 1500 ili kupata KW ambazo ni 1.5) lakini je kwa mwezi mzima unaliwasha kwa masaa mangapi ? Unaweza kununua jiko lina watts 2000 ila je unapika at maximum power au low power ambayo huenda unatumia 200 watts ?; Tukija kwenye ufanisi yaani kutokupoteza joto wakati wa kupika kuna induction cooker hii ndio balaa (yaani ufanisi wake unaweza ukawa zaidi ya mara tatu ya gesi)...,

Kwa nchi yetu ukiangalia mchakato mzima ni ujuha kutumia gesi ambayo tunaagiza kutoka nje kwa kutumia dola wakati tuna umeme wa ziada unapotea....


Tuungane kama wananchi tuwabane watunga sera wetu hakuna sababu ya unit moja kuwa zaidi ya Tshs 100/= kwa kila mtu ukizingatia kuna kipindi tuliachia maji kule Bwawa la Nyerere bila kufanya kazi eti maji yamezidi..
 
Ukichafuka mikono unatafuta sabuni na kunawa sio kununua gloves ili watu wasione huo uchafu..., Issue ya umeme mdogo inabidi TANESCO warekebishe usiwe mdogo...

Issue ya wengi kutokupikia ni mambo mawili, majiko ya zamani ya coils na plate ni kweli hayana ufanisi kwahio ukitumia sasa hivi yanakula umeme sana..., ila haa hayo kabla ya umeme kupanda bei mfululizo mithili ya mtu anayefukuzwa na Hussein Bolt watu walikuwa watumia hayo majiko ya umeme tena mengine yalikuwa assembled hapa hapa Bongo (DM Investments kiwanda cha Diallo hapo Mwanza) kipindi hicho hicho watu walikuwa na taa za zamani ambazo zilikuwa heater kuliko taa (hadi wanafugia kuku) Taa 100 watts ambapo kwa watts hizo hizo unaweza kutumia slow cooker kuivisha mboga / nyama kwa masaa saba (hizi taa zilikuwa mtu anazo hata nne au nane nje na zinawaka usiku kucha)

Kipindi hicho watu wanaogopa gesi kulipuka umeme ndio ulikuwa mpango mzima.....

Kwahio hapo utaona common denominator ni kwamba Serikali haitaki kupunguzia watu mzigo na hili ni sababu wanaoweza ku lobby ndio wenye biashara za gesi (kwahio ukweli hausemwi)
 
Ushambaaa,pili umeme wa ,magumashi sana
 
Huku sio kukasirika, ni Kufura 🤭
Kuna haya wanaita INFARED COOKER na INDUCTION COOKER yana tofauti gani na jiko la umeme kawaida
 
Mbona hujaongea hayo majiko yako bei gani? Tuwekee na picha. Tatizo mabei yenu ya kausha damu ndo maana mavitu yenu vinawadodea!
 
Umeme wa 10000 unapata kwh 28 unit moja unanunua karubi tsh357 hapa nikuongeza gharama zisizo za lazima
 
Masharti kibao,,,yanashot sana,usipike ukiwa peku utajuta
 
Washing machine ni ya muhimu sana lakin sjui kwann hatununui,tunawatesa watoto wa watu kila siku wanafua marundo ya nguo
Kuna vitu huwa najiuliza sipati majibu, unakuta mtu kajenga nyumaba ya 50-100 M, hana power backup yoyote solar power au fuel generator. Mtaani umeme ukirudi utasikia na yeye ''uoooo...''
Mtu huyo huyo, hana washing machine (mashine ya kufua nguo), utakuta wadada wa kazi vidole vya mikono vimevubaa, kucha zimeharibika.

Nami niunge mkono waliosema kuhusu suala la exposure, ni muhimu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…