Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 24,523
- 30,084
Nikufahamishe tu, chombo chochote cha umeme kisipopata kiwango sahihi cha umeme unaotakiwa ujue kitakuongezea gharama ya umeme na kukutia hasara, na hii hata hayo majiko ya mfumo wa kisasa.Ukichafuka mikono unatafuta sabuni na kunawa sio kununua gloves ili watu wasione huo uchafu..., Issue ya umeme mdogo inabidi TANESCO warekebishe usiwe mdogo...
Issue ya wengi kutokupikia ni mambo mawili, majiko ya zamani ya coils na plate ni kweli hayana ufanisi kwahio ukitumia sasa hivi yanakula umeme sana..., ila haa hayo kabla ya umeme kupanda bei mfululizo mithili ya mtu anayefukuzwa na Hussein Bolt watu walikuwa watumia hayo majiko ya umeme tena mengine yalikuwa assembled hapa hapa Bongo (DM Investments kiwanda cha Diallo hapo Mwanza) kipindi hicho hicho watu walikuwa na taa za zamani ambazo zilikuwa heater kuliko taa (hadi wanafugia kuku) Taa 100 watts ambapo kwa watts hizo hizo unaweza kutumia slow cooker kuivisha mboga / nyama kwa masaa saba (hizi taa zilikuwa mtu anazo hata nne au nane nje na zinawaka usiku kucha)
Kipindi hicho watu wanaogopa gesi kulipuka umeme ndio ulikuwa mpango mzima.....
Kwahio hapo utaona common denominator ni kwamba Serikali haitaki kupunguzia watu mzigo na hili ni sababu wanaoweza ku lobby ndio wenye biashara za gesi (kwahio ukweli hausemwi)
Hujambo?Hiki kingereza ni cha gesi au umeme?
SijamboHujambo?
Wewe watumia gesi au umeme?Sijambo
Kwakweli hii elimu ya Xi Jinping sikuwa nayo, natumia gesi.Wewe watumia gesi au umeme?
Hiyo gharama ya umeme ameandika haina uhalisia.Umeongea ukweli mtupu ngoja nikanunue jiko la umeme niachane na gesi, niwakomeshe wapangaji wenzangu.
Siyo wajinga! Hakujawa na awareness ya maana tu. Watu bado tumekariri ilivyokuwa zamani majiko yalikuwa yanakula sana umeme. Kikubwa watu waelimishwe tu kuhusu gharama za kutumia umeme. Matumizi ya mkaa mjini yanaweza kukoma kama watu watapata elimu. Pia serikali inatakiwa ipunguze bei ya umemeGas ikiisha unasikia Watanzania wajinga wakisema "sijui kwa nini gesi lazima iishe usiku."
Sawa gas imeisha usiku kwa nini usingekuwa na backup ya jiko la umeme?
Utamsikia Mtanzania anakwambia jiko la umeme linatumia umeme mwingi, ok well mbona ndani una vyombo vingi sana vya umeme na haulalamiki?
Kwani jiko la umeme unalitumia siku nzima?
Mtu ana flat screen ya milioni lakini jiko la umeme hata la plate 2 linamshinda.
Kuna ujinga mwingi sana kwenye jamii ya Watanzania, pesa ya kufanya au kununua vitu vya kijinga wanazo ila kuongeza units za umeme awe anatumia jiko la umeme hana.
Kuna majiko ya single burner yana 1000 watt
1000 watt ni sawa na 1kWh kwa saa
Tuseme kwa kadirio la juu unatumia jiko kwa masaa 2 kila siku yaani 2kWh
Kwa siku 30 za mwezi utakuwa umetumia 60kWh
Kwa sasa Tanesco wanachaji 1kWh kwa Tshs 100-250 kwa wateja wa kawaida
60kWh×Tshs 250 unapata 15,000/=
Kwa mwezi unaweza kutumia gesi ya shilingi ngapi?
Sasa we ushaona Wtz wana akili?Hizi hesabu Watanzania hawajawahi kupiga
Tanesco nao jau unapika mala fyaaa wameubeba umeme wao.Na siku hizi majiko ya umeme simple na ambayo matumizi yake ya umeme sio makubwa yako mengi tu. Bei iko reasonable
Watanzania wanathamini sana flat screens sijui wamerogwa
Tuwekee mchanganuo wa hizo gharama kwa elimu zaidiHiyo gharama ya umeme ameandika haina uhalisia.
Uhalisia gharama ipo juu kuliko alicho andika.
Hizo nyumba wamehesabu na zile za keko, vingunguti?Mtoa mada ni mpumbavu. Tanzania pamoja na kuwa na idadi ya watu inayokaribia milion 70 ina nyumba za makazi ambazo hasizidi milion 11 . Hii inamaana zaidi ya asilimia 90 ya watanzania wanashea nyumba na umeme, umeme wa kushea kidesturi haufai katika matumizi makubwa kwan ni chanzo cha migogoro
Nafikri mleta mada anasema mtu unakuwa na back up. Unakuwa na gesi kwa ajili ya back up!Mkuu tatizo umeme siyo reliable kwa hapa TZ ,umeme kila siku unakatika ,ni bora jiko la gesi lina meter unajua gesi ikiaribia kuisha.
Majiko ya umeme hakuna kitu inaitwa burner.Kuna majiko ya single burner yana 1000 watt
Ntalifany back up pale gesi ikiishaHiyo gharama ya umeme ameandika haina uhalisia.
Uhalisia gharama ipo juu kuliko alicho andika.
Umemjibu vyema huyu machina wa Mkundugeni ....Pesa zetu, upange cha kuzinunulia wewe!!
Tena na unatutukana kabisa. Mnunulie mama yako na ndugu zako wqnatosha.
Ule umeme wa units 75 kwa TZS. 9,150 kwa mjini ulishafutwa! Sasa hivi wote tumerundikwa kwenye group moja. Nchi yetu hovyo sana!Nimeona umeweka bei ila hizo sio bei halisi tunazoziona kwenye receipt...weka gharama halisi, hakuna unit ya tsh 292 kwa watumiaji wa zaidi ya 75kWh, wala tsh 350 unless useme hiyo ndo bei kabla serikali haijatia mkono, ambapo sio halisi sasa!