Watanzania wanawakubali CHADEMA juu ya kutetea rasilimali zao kuliko CCM kwa kipindi hiki fukuto likizidi kufukuta

Watanzania wanawakubali CHADEMA juu ya kutetea rasilimali zao kuliko CCM kwa kipindi hiki fukuto likizidi kufukuta

Ukikaa vijiweni, baa au kwenye maofisi ya umma, mjadala ni namna CHADEMA wanavyopambana kulinda rasilimali za Tanzania.

Utasikia watu wakisema nilikuwa naichukia CHADEMA ila kwa hili...

Nilikuwa namchukia Lissu ila kwa hili...

Mwisho kabisa wanakamilisha mjadala kwa kusema. Mama anatumiwa na ... Kuuza rasilimali za Nchi
Jambo ili sio la chadema! Bora tuwaoigie makofi Sauti ya Watanzania maana wak ndiyo walilivakia njuga kuliko ata Chadema wenyewe.

Mimi binafsi sina card ya chama chochote, na sina interest zozote na Chadema ila nimepinga ili limkataba mpaka kwa njia ya maandishi na kuwasilisha maoni yangu Bungen kuoinga marekebisho ya muswada wa sheria inayotaka ikafanywe ili kuibeba DP World mgongoni.
 
Wewe upite kwenye vijiwe vya wajinga wenzio na kuja kuandika uzi kuwa CHADEMA inakubalika.. una akili kweli wewe? Kwenye suala la DP World bora ungemtaja Dr Slaa, Mwabukusi na TEC ambao sio wanachadema. Nyie ni wazee wa kudandia agenda za watu. Hoja zilizotolewa na CHADEMA zilikuwa hazina mashiko. Nakumbuka ni Mbowe tu aliropoka kuhusu Tanganyika na Zanzibar... hakuna mtu yeyote toka CHADEMA aliyeongea la maana. Kitu pekee mlichoongea ni #freemdude na #freemwabukusi.
Umefuatilia mikutano yao? Hujasikia wakichambua ibara mbovu moja baada ya moja za IGA
 
Ukikaa vijiweni, baa au kwenye maofisi ya umma, mjadala ni namna CHADEMA wanavyopambana kulinda rasilimali za Tanzania.

Utasikia watu wakisema nilikuwa naichukia CHADEMA ila kwa hili...

Nilikuwa namchukia Lissu ila kwa hili...

Mwisho kabisa wanakamilisha mjadala kwa kusema. Mama anatumiwa na ... Kuuza rasilimali za Nchi
Huyu mstaafu!
Ndie aliyeanzisha ufisadi mkubwa katika nchi hii enzi za utawala wake.
ESCROW,RICHMOND,MEREMETA,SYMBION,IPTL .hizi
Zote ni kashfa za enzi zake!

Sasa ameshikilia Remote bila aibu na anatupelekesha na DP-WORLD!
Hataki kuachia remote akiamini kuwa anao ubavu wa kutupelekesha kwa ushirika na "RA".
Fisadi kubuhu ambaye amerudi kwa kasi ya 5G kwenye awamu hii ya mteule wao maushungi!

Je!
Watanzania mnakubali hali hii mpaka lini?

Nchi inaelekea kugawanyishwa kwa makundi mawili yenye maslahi tofauti.

1-Wapinga mkataba mbovu wa DP-WORLD!
Ambao wana maslahi mapana ya upendo kwa nchi yetu Tanganyika.

2-Waliouleta mkataba baada ya kutundikwa picha zao ukutani huko Emirati.
Kwa maslahi mapana ya matumbo yao mapana yasiyotosheka.

Kama Rais mstaafu analipwa mshahara 80% ya Mshahara wa Rais aliyeko madarakani currently.
Pia anaruhusiwa kutibiwa katika hospitali za kimataifa huko ughaibuni.

Anao walinzi na madereva wa serikali muda wote wa maisha yake.
Huku pia akipewa mgao wa gari mpya kila baada ya miaka mitano.
Amejengewa nyumba ya kifahari na serikali.
Na bado anazo nyumba lukuki za serikali alizojimilikisha toka zile zilizokuwa za serikali.

Walizojiuzia kinyemela....
Yoote hiyo haridhiki nazo na bado anataka kuliyumbisha taifa kwa kutaka mali zaidi!
Sasa naanza kuwaelewa wale viongozi wa Mapinduzi wa Niger dhidi ya Rais bilionea muuza Nickel ...Boughum!

Mungu Inusuru Tanzania
 
Ukikaa vijiweni, baa
hawa hawapigagi kura!.
Utasikia watu wakisema nilikuwa naichukia CHADEMA ila kwa hili...

Nilikuwa namchukia Lissu ila kwa hili...

Mwisho kabisa wanakamilisha mjadala kwa kusema. Mama anatumiwa na ... Kuuza rasilimali za Nchi
as long as hakuna hata milimita moja ya JMT inayouzwa, then hakuna ubaya wowote wala hakuna tatizo lolote
P
 
Ukikaa vijiweni, baa au kwenye maofisi ya umma, mjadala ni namna CHADEMA wanavyopambana kulinda rasilimali za Tanzania.

Utasikia watu wakisema nilikuwa naichukia CHADEMA ila kwa hili...

Nilikuwa namchukia Lissu ila kwa hili...

Mwisho kabisa wanakamilisha mjadala kwa kusema. Mama anatumiwa na ... Kuuza rasilimali za Nchi
Pumba
 
Umeambiwa endapo Tume ya uchaguzi ikiwa huru hata kwa 25% tu. Kichwa chako kinafunza ama.
 
hawa hawapigagi kura!.

as long as hakuna hata milimita moja ya JMT inayouzwa, then hakuna ubaya wowote wala hakuna tatizo lolote
P
Vijiwe vya kahawa, maofisini na vya kwenye mabaa vinatoa picha namna gani utawala unakubalika.

Hilo la milimita 1 ya JMT kutokuuzwa wewe unalijua mwenyewe.

Hoja ni namna wananchi wanavyomtathimini rais wao na CCM yenu
 
Vijiwe vya kahawa, maofisini na vya kwenye mabaa vinatoa picha namna gani utawala unakubalika.
Ni kweli wanatoa picha tuu but they doesn't matter!, wanaomatter ni wapiga kura!
Hilo la milimita 1 ya JMT kutokuuzwa wewe unalijua mwenyewe.
Ndio ukweli wenyewe
Hoja ni namna wananchi wanavyomtathimini rais wao na CCM yenu
Tathmini doesn't matter much, what matters ni decision makers!, tathmini ingekuwa ina ratings hapo tungejali.
Maandalizi ya HGA, yanaendelea
P
 
Ni kweli wanatoa picha tuu but they doesn't matter!, wanaomatter ni wapiga kura!

Ndio ukweli wenyewe

Tathmini doesn't matter much, what matters ni decision makers!, tathmini ingekuwa ina ratings hapo tungejali.
Maandalizi ya HGA, yanaendelea
P
Picha namna utawala unavyofeli na kuonekana ni wa kifisadi sio jambo la kupuuzwa.

Nani aanze kufikiria habari za HGA ambayo tayari imeonyesha kuna ufisadi na mkono wa Rostam Azizi?

Hata huko Niger hao wananzengo wa vijiweni walipuuzwa kama unavyo wapuuza wa hapa Tz
 
CHADEMA NEC ikiwa hata huru kwa 25% wanabeba nchi
🤓 Ben, Labda hiyo nchi iwe ya kusadikika.
Hofu ya CCM ni chadema kuungana na vyama vikubwa angalau vi5 tu.
Hapo CCM watatetemeka kwa hofu na baridi kali sana litawakumba kwakweli na jua litafifia.
Vinginevyo ni porojo na ndoto za kimweri kwa chadema au ACT au chama chochote pekeake kuishinda CCM Karne hii.
 
hawa hawapigagi kura!.

as long as hakuna hata milimita moja ya JMT inayouzwa, then hakuna ubaya wowote wala hakuna tatizo lolote
P
Hivi Ngorongoro na Loliondo zimeuzwa?
Pasco, hivi kama nchi tumeshindwa kujifunza kutoka huko?
Au tumeshindwa kujifunza kutoka katika mikataba ya madini?
Mkuu Pasco maisha ya mwanadamu ni mafupi sana, ni vizuri kusimamia ukweli katika maisha haya kama unaamini kuna life after death na tutaishi kulingana na matendo na misimamo yetu katika kipindi hiki cha maisha mafupi.
Ukiwa na kipawa cha kusikilizwa na wengi (kama ulichonacho) kitumie kuusemea ukweli na sio kupotosha kama MacKenzie
 
Mbona hawazunguki tena kuutetea mkataba wamekaa kimya kbs.
Waligundua ni kama vile wanazidisha petrol kwenye kuni!! Walijikuta wanaeneza tu chuki. Kuna mmoja kwenye kundi hilo wanamtema wiki hii
 
Waligundua ni kama vile wanazidisha petrol kwenye kuni!! Walijikuta wanaeneza tu chuki. Kuna mmoja kwenye kundi hilo wanamtema wiki hii
Endeleeni kujifariji!
JamiiForums2026477905.jpg
 
Ukikaa vijiweni, baa au kwenye maofisi ya umma, mjadala ni namna CHADEMA wanavyopambana kulinda rasilimali za Tanzania.

Utasikia watu wakisema nilikuwa naichukia CHADEMA ila kwa hili...

Nilikuwa namchukia Lissu ila kwa hili...

Mwisho kabisa wanakamilisha mjadala kwa kusema. Mama anatumiwa na ... Kuuza rasilimali za Nchi
Sio kipindi hiki tu. Ni tangu zamani in the history of Politics sema wewe ulijizima data tu.
 
Back
Top Bottom