Pre GE2025 ‘Watanzania wanyonge’ wataka Paul Makonda agombee na kupewa Urais 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna upinzani nchi hii zaidi ya kuwa na magenge ya wasaka tonge wanaohangaikia matumbo yao tu.
 
Hakuna upinzani nchi hii zaidi ya kuwa na magenge ya wasaka tonge wanaohangaikia matumbo yao tu.
Usingekuwepo hata hiyo sentensi uliyotoa usingeitoa,ungekua umekaa baharini unapunga upepo bila stress

Upo hapa full stressed coz unajua upinzani upo well and alive!
 
Naunga mkono hoja, tena mimi nimempangia 2025 Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... hili litawezekana tuu, endapo sauti HII
ni ya kweli ya kwake YEYE!.
P
 
Yaani tuko kwenye dunia ya ubepari, halafu wewe na ndugu yako Bashite bado mnaongelea habari za unyonge/wanyonge!! Nyinyi kweli hamna akili.
 
MLETA UZI ANA JUHUDI.....
ANAJITAHIDI SANA KUKIDHI MATAKWA...
 
Nilitaka nishangae,,,,bashite apige tu mamikutano yote yale bila kuwa agenda zake flani flani za siri za kuwalipa watu wampigie chapuo chini chini ili achukue form mwakani, ningeshangaa sana
 
Nilitaka nishangae,,,,bashite apige tu mamikutano yote yale bila kuwa agenda zake flani flani za siri za kuwalipa watu wampigie chapuo chini chini ili achukue form mwakani, ningeshangaa sana
Mheshimiwa Makonda halipo watu wala kutoa pesa kwa ajili ya kufanya chochote kile kwa ajili yake .bali ni kutokana na kazi njema na uchapa kazi wake uliotukuka ndio umegusa mioyo ya mamilioni ya watanzania mpaka sasa kuwa na kiu ya kutaka kuongozwa na yeye kama Rais wetu mwaka 2030. Mheshimiwa Makonda amekonga na kugusa mioyo ya watanzania wanyonge ambao wanamuona Mheshimiwa kama mtetezi na sauti yao
 
Yaani tuko kwenye dunia ya ubepari, halafu wewe na ndugu yako Bashite bado mnaongelea habari za unyonge/wanyonge!! Nyinyi kweli hamna akili.
Kasome katiba yetu ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kurasa za mwanzo kabisa ufahamu inafuata mfumo upi .
 
Huo utafiti wa hao watu mamilioni uliufanyia wapi na kwa muda gani? Acha kuandika kishabiki boss. Kama ni hisia zako binafsi na una hoja za msingi za kwa nin unataka makonda agombee uraisi basi ziweke hapa na sisi tuzisome na tuzipime....kama zina mashiko basi tuta kuunga mkono,

Ila sio kuja tu mbio mbio eti mamilioni "wanataka", .....kaka humu ndani kuna watu wanajielewa na wana uelewa wa mambo. Nenda kwa step basi.
 
Kasome katiba yetu ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kurasa za mwanzo kabisa ufahamu inafuata mfumo upi .
Hivi kumbe kuna Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!! Mimi siku zote ninachofahamu kama nchi, tuna Katiba ya CCM ya mwaka 1977!

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilitakiwa iwe ni ile tuliyoipendekeza sisi wananchi mwanzoni mwaka 2010! Na kufanikiwa kupata Rasimu yake, ambayo kwa makusudi kabisa mkaamua kuifanyia uhuni. Na siyo hiyo takataka iliyoandaliwa na makada wachache wa chama chenu, halafu mnaiita eti ni Katiba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…