Watanzania watu wa ajabu, wanapenda maendeleo lakini hawataki kugharamia hayo maendeleo kwa kodi

VAT ni nini?
 
Watu wako tayari kulipa kodi+tozo
Na serikali wabane matumizi,waache matumizi yasiyokuwa na tija na mambo ya anasa anasa
Twende sawa
Siyo unakamua kule alafu nyie huko mnajiachiaaaa tu

Ova
 
Kwanza na wao wakati umefika wakatwe kodi na walipishwe tozo.
Ili twende sawa sawa

Ova
 
Watu wako tayari kulipa kodi+tozo
Na serikali wabane matumizi,waache matumizi yasiyokuwa na tija na mambo ya anasa anasa
Twende sawa
Siyo unakamua kule alafu nyie huko mnajiachiaaaa tu

Ova
Serikali iachane na sula la kuwanunulia mawaziri magari ya kifahari.
Watumie magari yale ya kula mafuta kidogo kama X-Trail.
 
Wasalaam,

Kama jina la uzi linavyosema, nauliza ni kweli kwamba vyanzo vya mapato ni tozo tuu hatuna angle nyingine ambayo inaweza kumpumzisha Mtanzania na kumfanya asijute kuwa Mtanzania?

Kwa nijuavyo mimi kuna Tax revenues na non tax revenues, sasa ni jitihada gani zimefanyika katika kuhakikisha tunapata fedha za kutosha kupitia resources zetu ili kumpimzisha mwananchi na tozo/taxes?

Ni wakati sasa wa nchi hii kuwa na VISION ya kueleweka na sio kila anayeingia analeta mambo yake, nchi hii ina madini ya kutosha na ya kila aina, ina gesi ya kutosha na ina bandari ina mifugo, bahari ya uvuvi, ardhi yenye rutuba vitu ambavyo ni muhimu katika ukanda huu, ni kwa namna gani hivi vitu vinasaidia wananchi.

Viongozi ni wakati sasa muwe wabunifu na kuacha kufikiria kirahisi rahisi, mkumbuke the more you are taxing people the more you rise their awareness, so are you ready to dig your own graves?
 
Mi nahis umeandika ujingaaaaa
 
Haya ndio mawazo mfu ya watu wapenda vya bure.
Mtu anasema kuna madini mengi tu ya bure, uvuvi na ardhi yenye rutuba.
Halafu mtu huyu anategemea hizo rasilmali ztenmee kwa miguu zenyewe kwenda Hazina!!!
Mtu anaongea na kujitoa kutoka kwenye scenario, its them, not me kuleta mapato, mimi ni mnufaika tu!

Hivi tumelogwa na nani kwa kutokuwa na moyo wa uwekezaji sisi wenyewe?
 
Kwa juhudi zako wewe mwenyewe , umewekeza nini?
Au unamsubiri mjombatoka Uarabuni, Ulaya, Uchina -akukatie pori, alete hela zake za mkopo wa uwekezaji, aajiri wafanyakazi na azalishe mali.

Wewe uko ofisini kusubiri kodi!!
Hapo ndipo tulipologwa!
 
Sio wajinga wanasiasa walishawaaminisha nchi hii Ina utajiri wa rasilimali wa kutupa Sasa kwanin uwabebeshe mzigo wa kodi
Rasilimali ambayo bado huja anza kuitumia sio rasilimali.. mfano madini yaliyopo chini ya ardhi ni mengi sana ila kwa vile hayaja anza kutumika hayana faida bado
 
Lengo lako kubwa ni kutibua watu nyongo. Halafu ukae kando uone wanavyochemka...
 
Unafaa kuwa waziri wa fedha, alafu MWINGULU akalime huko milima SEKENKE
 
Kweli leo nimeamini watu wenye akili zao wako uraiani alafu zero brain ndo ziko madarakani, hasa Mwigulu yule [emoji1664]

Big up sana brother.
 
Lengo lako kubwa ni kutibua watu nyongo. Halafu ukae kando uone wanavyochemka...
Njoo huku Stocholm, Sweden na uine wananchi wake wanavyokatwa kodi kwa kila kitu.
Lakini kodi za wenzetu zinatumika vizuri sana.
Wabunhe wanalipa kodi, na hata mawaziri.

Kodi zinatumika kuendeleza afya, usafiri, uendeshaji miji na elimu ni bure.
 
Siyo lazima uwekeze ndio ulipe kodi, kodi inalipwa na mlaji. Nikitumia fedha zangu ktk manunuzi ninalipa kodi pia.
 
Ukifuatilia malalamiko kwa undani, siyo kuwa watu hawaoni umuhimu wa kulipa kodi, la hasha, bali ni uhalisia (fairness) ya kodi/tozo yenyewe. Mfano mimi mwajiriwa nakatwa kodi kwenye mshahara, halafu nikienda benki kuchukua mshahara nakatwa kodi tena kwenye mshahara ule ule. Pili matumizi ya serekali na taasisi zake ni ya kufuru. Chukulia mfano waziri mwenye dhamana anakuja na tozo kwenye mwamala hata wa Tzs 5,000 wakati huo huo ananunua gari la Tzs 500m. Yes tukamuliwe kodi/tozo - na ni wajibu wetu kulipa kodi - lakini siyo fedha zisifujwe na wakubwa.
 
Kwa hiyo njia sahaihi ni kukomalia waziri asitumie vibaya mali ya umma, au alipie matumizi yake yanayoonekana ni anasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…