Watanzania watu wa ajabu, wanapenda maendeleo lakini hawataki kugharamia hayo maendeleo kwa kodi

Siyo lazima uwekeze ndio ulipe kodi, kodi inalipwa na mlaji. Nikitumia fedha zangu ktk manunuzi ninalipa kodi pia.
Kila mtanzania akiwa na mawazo hayo tusahau maendeleo.
Hayo ni mawazo ya rest easy, kuna mjomba ataleta fwedha kukuendeleza.
 
Njoo huku Stocholm, Sweden na uine wananchi wake wanavyokatwa kodi kwa kila kitu.
Lakini kodi za wenzetu zinatumika vizuri sana.
Wabunhe wanalipa kodi, na hata mawaziri.

Kodi zinatumika kuendeleza afya, usafiri, uendeshaji miji na elimu ni bure.

Wanaspend billion 500+ kununua hayo magari Yao hapo bado hujaongelea kuyamantain
 
Mwalimu anakatwa Kodi mshahara na akinunua kiberiti anakatwa Tena,serikali kujenga shule na hospitali ni wajibu,hela wanatoa wapi!?
 
Watu wako tayari kulipa kodi+tozo
Na serikali wabane matumizi,waache matumizi yasiyokuwa na tija na mambo ya anasa anasa
Twende sawa
Siyo unakamua kule alafu nyie huko mnajiachiaaaa tu

Ova
Watz hupinga kila kitu Cha serikali,hakuna walichounga mkono,walipinga kuhama analogia,walipinga shule za kata,walipinga vitambulisho vya nida, wanapinga,wanapinga mbolea ya ruzuku...hawana jema
 
Mwalimu anakatwa Kodi mshahara na akinunua kiberiti anakatwa Tena,serikali kujenga shule na hospitali ni wajibu,hela wanatoa wapi!?
Unaelewa maana ya direct tax na indirect..direct tax ina maumivu...hio ya kununua kiberiti ni indirect haina athari moja kwa moja kwako wewe...pia anaekuuzia kiberiti amelipa kodi ya mapato(serikali imeshachukua hela yake hapo ya kujengea hospitali, barabara, mashule nk), leseni ya biashara pia ameshalipa, na makorokoro mengine...kwaio akijumlisha gharama zote anakuuzia kiberiti katika namna ya isiokia na maumivu akaitaka akuumize hapo anatakiwa awe anakuchaji bei ya kuulizia bidhaa dukani i.e unapuliza kiberiti sh ngapi,mchele shingapi? Akuandikie kuulizia bei ya bidhaa ya kitu ni sh 500 + kiberiti cha sh 200 = 700tshs ungekubali? Jifunze vitu mbali mbali mkuu usiwe mzembe mzembe...🤣🤣😍
 
Kazi ya serkali ni kubuni vyanzo vya kodi kwa kutumia rasilimali zake

Kazi ya serikali ni kuendesha taasisi zake zote ikiwemo wizara ya Elimu na Afya. Kujenga madarasa na Vituo vya Afya ni wajibu siyo 'favour' wala haiwezi kusemwa ni mafanikio! Ni wajibu wa serikali iliyopo madarakani

Watanzania wanalipa kodi kwa bidhaa zote na huduma wanazotumia.
Kukusanya kodi ni sehemu tu, matumizi ya kodi ni sehemu nyingine

Mafanikio ya kodi yanatokana na mambo mawili, kukusanya na matumizi yake. Katika nchi yetu matumizi ya hovyo yasiyo na ulazima yanagharimu serikali na mzigo huo anautwisha mwananchi kwa jina la TOZO

Waziri Nchemba kasema kuna watu 500 wanalipwa mishahara ya scale ile ile ya kuteuliwa na Rais ingawa hawafanyi kazi hizo. Haya ni matumizi mabaya ya kodi yanayolazimisha ukusanyaji kwa njia ya Tozo

Matumizi ya serikali na taasisi zake ni makubwa sana. Mbunge anajua kituo chake cha kazi ni Dodoma, ana nyumba lakini bado analipwa pesa nyingi kila akikaa Bungeni mbali ya mshahara mnono.

Ukitaka kujua kuna tatizo, piga hesababu za Taasisi ya Bunge kwa siku moja tu halafu zidisha mara vikao
Kwanini mkoa mmoja una RC mmoja, mkoa huo huo una Wabunge 7 etc?

Kama tunahitaji kodi kwanini hatupunguzi vikao vya 'Bunge' kwa siku 20 tu kwa mwaka! piga hesababu

Kwanini maafisa wanunuliwe V8 ? Kwanini wasipewe pesa za nauli na kuwe na gari chache za Idara na Wizara?
Kwanini karani ajilipie nauli ya kazini halafu alipe TOZO ya kununua V8?

Hoja si kodi au TOZO , hoja ni matumizi mabaya ya fedha yanayolazimisha serikali kutoza tu bila kuangalia namna ya kukusanya kutoka vyanzo vingine. Mfano, tuna madini ya HELIUM kule katavi yanayotafutwa duniani, nani anafikiria ni chanzo kizuri cha mapato?

Kama serikali imeishiwa mbinu, kwanini wasiache wengine wenye mawazo tofauti kama Zambia au Kenya waje na mbinu mpya! Hatuwezi kuishi kwa kukinga Bakuli ughaibuni na kuminya wauza mchicha miaka 60 ya Uhuru

JokaKuu Pascal Mayalla Tindo
 
Tofautiisha kati ya kodi na tozo
 
Sikiliza akili kubwa,
Over taxation huua uchumi,
 

Attachments

  • VID-20220919-WA0001.mp4
    6.4 MB
nadhani sio kama wananchi wengi hawapendi kulipa kodi ila swala je serikali ina mshawishi vp wananchi kulipa kodi kwa hiyal ... serikali imetengeneza mazingira yapi kwa wananchi kulipa kodi ...machinga weny mtaji wa Tsh 20000 umemtengenezea mazingira gani ili akupe kodi na asupport kodi & tozo .
 
Tatizo unadhani elimu ya uchumi unayo peke yako
 
Kodi ni kwa ajili ya kuendesha serikali ambayo itatumia raslimali zilizopo duniani au ulimwenguni kuwaletea raia wake maendeleo.
Kama kodi huleta maendeleo moja kwa moja kusingekuwepo utumwa, ukoloni mkongwe na sasa mamboleo.
 
Sio watanzania wote, bali kuna baadhi ambao wanajua faida ya tozo ila kwa maksudi na kwa lengo la kutaka serikali ishindwe ndio wanao payuka
 
Wananchi wengi hawana uelewa kuhusu ulipaji kodi afu pia wajinga ni wengi nchi hii
Watu hawayapendi mavieite ya Polepole na maanasa anasa mengine wanayoyaona na wanayoyasikia !! Sio kwamba hawapendi kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Nchi ! Hapana sio kweli !! Kwanza tuelewe kwamba mlipaji kodi mkuu ni yule mtumiaji au mlaji ambaye sio mfanyabiashara ! Huyo mfanyabiashara huwa anamkopesha mlaji hiyo kodi anayoilipa anaponunua bidhaa zake za dukani kisha anaanza kuchukua kodi aliyoitoa pamoja na faida katika kila bidhaa atakayoiuza kwa hao walaji wa mwisho!! Lakini siku zote huwa anaonekana mlipaji kodi ni mfanyabiashara !! I stand to be corrected !!
 
Sio watanzania wote, bali kuna baadhi ambao wanajua faida ya tozo ila kwa maksudi na kwa lengo la kutaka serikali ishindwe kutekeleza maendeleo ya wananchi ndio wanao payuka.

Lakini watanzania wengi wanataka kuchangia maendeleo yao.

Ninacho kiona, bado watanzania tulitakiwa twende mwendo wa mateka, kama tutaenda kwa kubembelezana kamwe hatuwezi kufika.

Ndio maana hayati JPM alikuwa hasikilizi upumbavu....ilimradi likikuwa kwa masilahi ya watanzania yeye alikuwa hajali mwendo mdundo.

Hata ufanya jambo zuri kiasi gani wapingaji huwa hawakosekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…