Watanzania watu wa ajabu, wanapenda maendeleo lakini hawataki kugharamia hayo maendeleo kwa kodi


Uko sahihi, je zile raslimali mnazosema tunazo mpaka wazungu watuonea wivu ziko wapi, kwanini zisiuzwe ili kutupatia fedha?

Unashangaa watu kutaka serikali itoe huduma zote, wakati kila hela za kodi zikitolewa na wananchi zinaitwa ni fedha za rais? Kwanini zisiitwe kodi za wananchi ili watu wasione Serekali ndio yenye hizo fedha?

Tozo za nini wakati viongozi wanatumia fedha za wananchi bila huruma? Kama rais alienda huko nje ambako hajapigiwa kura, akapikizwa basi na hakufa, kwanini hapa ambapo amepigiwa kura atembee na misururu mirefu ya magari kwa kisingizio cha kulinda usalama wake?
 
Watz hupinga kila kitu Cha serikali,hakuna walichounga mkono,walipinga kuhama analogia,walipinga shule za kata,walipinga vitambulisho vya nida, wanapinga,wanapinga mbolea ya ruzuku...hawana jema
Wewe ni mrundi?

Watanzania hatupingi kulipa kodi ndio maana umeajiriwa kuendesha gari la 500M lililonunuliwa kwa kodi zetu
 
Umedadavua vizuri sana.

Kwa kuongezea, tusijilinganishe na nchi zilizoendelea kwa historia tofauti kama US na Sweden. Tujilinganishe na wenzetu wenye uchumi wa kiwango kama sisi au ambao hivi karibuni wameweza kupiga hatua kutoka hali inayofanana na sisi na kuweza kuendelea zaidi mfano zile nchi zinazoitwa Tiger economies - Singapore, Taiwan, nk.

Je, hizi tiger economies ziliweza kuendelea kwa misingi ya kujikita kwenye kukamua na kukusanya kodi kwa wanachi wake?
 
Sio Kweli.
 
Tanzania ni nchi ya ajabu VIONGOZI WANAPENDA maendeleo Ila hawataki kupunguza gharama za kila siku katika uendeshaji wa Serikali.
 
Kiufupi ,wanywaji wanywaji wa vileo wantakiwa kupewa tuzo ya ulipaji Kodi bila manunguniko.

Kwa miaka mingi serikali imekua ikiongeza Kodi kwenye vinywaji ,na gharama hizo hubebwa na wanywaji. Cha ajabu hayajawahi kutokea malalamiko kama haya ya Tozo.
 
Hata hiyo kodi kwenye uagizaji magari tulipaswa kuipinga kwa nguvu zote ila basi tu.

Kodi ni sawa au kubwa kuliko bei ya bidhaa yenyewe ushaona wapi?

Siku watu wakiridhika na matumizi ya kodi zao hakuna atayelalamika.

Waziri asiyekuwa na wizara??
 
Cleopa Msuya, alipokuwa Waziri wa Fedha, alisema , kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe.
Wakamchukia.
ukiacha cha Arusha utakua kijana safi. Haiwezekani kabla ya kunipa mshahara unaukata kodi. Kinachobaki unaniwekea bank halafu unavizia ukate tena kodi ninapoichukua hiyo hela toka bank
 

majibu ya mada yako utayapa humu kwanini watanzania hawataki kutoa hao matozo... nchi hii ni ngumu sana.
 
Kodi haileti maendeleo. Kodi ni kwaajili ya posho za watawala na kugharamia maisha yao ya anasa.
 
Watu hawataki kuwekeza hata kwenye frame ya duka, lakini wanataka elimu bure, matibabu bure, na barabara za lami wanataka hadi mlangoni.
Lakini kulipa kodi inakuwa shughuli pevu, na wabunge wenyewe wanaongoza kwa kutolipa kodi.
 
ukiacha cha Arusha utakua kijana safi. Haiwezekani kabla ya kunipa mshahara unaukata kodi. Kinachobaki unaniwekea bank halafu unavizia ukate tena kodi ninapoichukua hiyo hela toka bank
Kwa kulinganisha tu, Magfuli aliitumia TRA kubeba fedha za wafanyabiashara toka kwnye mabenki kwa nguvu, mkashangilia.
Sasa litaka ninyi ndo msiguswe?
 
Mjeledi ni muhimu sana ili tusonge mbele.
tukibembelezana hatuwezi kupiga hatua ya maendeleo.
Malengo ya wapingaji ni kuchelewesha dhamira njema ya Serikali kutuletea maendeleo.......
naishauri Serikali isihangaike na kelele za wachawi.
 
…Serikali makini duniani kote zinatengeneza mazinira ya uwekezaji kwa WANANCHI WAKE ili waweze kupata kodi kutokana na biashara zao. Huo lazima uwe msingi wa nmna ya kupata kodi...

Lawama zako kwa wananchi zinakinzana na ulichokisema kwenye hiyo paragraph. Serikali imeshindwa kutengeneza hayo mazingira, lakini wewe unataka wananchi waunge mkono hizo tozo bila kujali kama wana vyanzo vya pesa ya kulipa hizo tozo au la.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…