Watanzania wawili wakamatwa India kwa usafirishaji wa kilo 1.5 ya dawa za kulevya

Billion 2 mate yananitoka

Sema haya maisha sometimes ni kujilipua tu umafia umafia ukitoboa hapo unaachana kbs na hiyo biashara unanunua zako benz unaenda kujenga kajengo kadogo lushoto..unaanzisha m pesa,kamin supermarket na ka daladala kamoja na ka grocery kamoja chenye kitimoto na duka la nguo..unatulia kimyaaaaa
Kuuza ngada sio umafia. Umafia nikuinfiltrate biashara zingine , kugamble, maswala ya pesa nyingi kuziamisha ndio umafia, elchapo, na wenzake sio ma mafia wale, mafias wako huko italy, wachache mexico na hawapo kwenye cartels.

Turudi kwenye mada, Kupata hela nzuri kwenye Kuuza Unga inahitaji muda mrefu ila sio mrefu sana, unahitaji utrafick walau safari tatu bila kukamatwa. Ukikamatawa hata uachiwe unakua umefanya kazi bure tu. Huridhiki.
 
Billion 2 mate yananitoka

Sema haya maisha sometimes ni kujilipua tu umafia umafia ukitoboa hapo unaachana kbs na hiyo biashara unanunua zako benz unaenda kujenga kajengo kadogo lushoto..unaanzisha m pesa,kamin supermarket na ka daladala kamoja na ka grocery kamoja chenye kitimoto na duka la nguo..unatulia kimyaaaaa
Hizo sio zao, wao ni punda tu, hizo ni hela za mfuga punda
 
Point yako ya msingi ni ipi?
Nadhani anamaanisha kuwa kuna dini zina mafundisho yanayokosa mkazo wa kufanya kazi kwa bidii. Na kwa sababu mahitaji ya mwanadamu hayategemei wewe ni wa imani gani, hawa watu wasio na mafundisho thabiti ya kujituma kufanya kazi, mwishowe hukimbilia njia za mkato ili wapate kuishi.

Hapa nchini, maeneo mengi walioishi waarabu, kama vile Tabora, Tanga au Ujiji, watu wengi siyo watu wa kujituma, hasa kwenye kazi ngumu. Tena kwenye maeneo hayo, utakuta hali hiyo haitegemei imani ya mtu. Hata kuanza kazi asubuhi, hasa kwa wasioajiriwa, huchelewa sana kuanza.

Kuna njia moja ya uhakika ya kumfanya mtu awe na uhakika wa maisha yake, nayo ni kufanya kazi kwa bidii. Mengine yaliyobakia ni kubahatisha kunakoendana na hatari nyingi.
 
View attachment 2786999

Kurugenzi ya Mapato ya Ujasusi nchini India (DRI) imewakamata Raia wawili kutokea nchini Tanzania kwa madai ya kuhusika na usafirishaji wa kilo 1.5 ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine yenye thamani ya kati ya milioni 80 hadi 100 ya India (Tsh Bil 2.4 mpaka Bil 3) kwa kuzificha ndani ya miili yao ikiwa ni tukio la saba ndani ya kipindi cha mwezi mmoja nchini humo.

Taarifa zinasema mwanzoni mwa mwezi October chombo hicho cha ujasusi DRI kilimnasa Mussa Mgonja (62) na Rashid Zamiru (23) ambao waliwasili kutoka Addis Ababa nchini Ethiopia kuelekea jijini Mumbai nchini India.

Ingawa utafutaji wao wa binafsi haukuzaa matunda, kwa mujibu wa ripoti walipopelekwa katika Hospitali ya JJ, Musa alionekana na vidonge 79 ndani ya mwili wake na Rashid akiwa na vidonge 33 kisha uchunguzi zaidi ulibaini kuwa wawili hao walikuwa wabebaji mahiri wa dawa za kulevya ambapo Mussa alisema hiyo ilikuwa ni safari yake ya pili na alikuwa amesafirisha vidonge kufikia 125 vya madawa huko kuelekea jijini Delhi, nchini India.

Ayo updates
Musa na rashidi au sio. Mbuzi wa kafara
 
Shida sio bidii, shida ni tija, wengi wanafanya kazi zisizo na tija ndio maana hukosa morali ya kufanya kazi kwa bidii
 
View attachment 2786999

Kurugenzi ya Mapato ya Ujasusi nchini India (DRI) imewakamata Raia wawili kutokea nchini Tanzania kwa madai ya kuhusika na usafirishaji wa kilo 1.5 ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine yenye thamani ya kati ya milioni 80 hadi 100 ya India (Tsh Bil 2.4 mpaka Bil 3) kwa kuzificha ndani ya miili yao ikiwa ni tukio la saba ndani ya kipindi cha mwezi mmoja nchini humo.

Taarifa zinasema mwanzoni mwa mwezi October chombo hicho cha ujasusi DRI kilimnasa Mussa Mgonja (62) na Rashid Zamiru (23) ambao waliwasili kutoka Addis Ababa nchini Ethiopia kuelekea jijini Mumbai nchini India.

Ingawa utafutaji wao wa binafsi haukuzaa matunda, kwa mujibu wa ripoti walipopelekwa katika Hospitali ya JJ, Musa alionekana na vidonge 79 ndani ya mwili wake na Rashid akiwa na vidonge 33 kisha uchunguzi zaidi ulibaini kuwa wawili hao walikuwa wabebaji mahiri wa dawa za kulevya ambapo Mussa alisema hiyo ilikuwa ni safari yake ya pili na alikuwa amesafirisha vidonge kufikia 125 vya madawa huko kuelekea jijini Delhi, nchini India.

Ayo updates
Kuna Mtanzania alikamatwa huko China akasababisha nchi iingie mikataba ya hovyo ya gesi na Bandari ya Bagamoyo..

Safari hii tunawaokoaje wenzetu? Tugawe nini kwa Wahindi?🤣
 
Nadhani anamaanisha kuwa kuna dini zina mafundisho yanayokosa mkazo wa kufanya kazi kwa bidii. Na kwa sababu mahitaji ya mwanadamu hayategemei wewe ni wa imani gani, hawa watu wasio na mafundisho thabiti ya kujituma kufanya kazi, mwishowe hukimbilia njia za mkato ili wapate kuishi.

Hapa nchini, maeneo mengi walioishi waarabu, kama vile Tabora, Tanga au Ujiji, watu wengi siyo watu wa kujituma, hasa kwenye kazi ngumu. Tena kwenye maeneo hayo, utakuta hali hiyo haitegemei imani ya mtu. Hata kuanza kazi asubuhi, hasa kwa wasioajiriwa, huchelewa sana kuanza.

Kuna njia moja ya uhakika ya kumfanya mtu awe na uhakika wa maisha yake, nayo ni kufanya kazi kwa bidii. Mengine yaliyobakia ni kubahatisha kunakoendana na hatari nyingi.
Sawa.nitajie nchi zinazoongoza kwa kuuza madawa ya kulevya.na unitajie nchi za kiislam japo 3
 
Back
Top Bottom