Jana kulikua na maandamano ya chadema yalikuwa yanalenga kuaddress kero tofauti tofauti na ilikua ni hiyari na sio lazima.
Mimi binafsi sikuandamana sababu watanzania ni wanafki na kumpigania mtu mpumbavu kama Mtanzania ni kupoteza muda na nguvuila ila kamwe siwezi wabeza waliondomana kwa namna yeyote ile.
Ila ajabu kuna watu wanawabeza chadema mara hawakua na watu wengi walikua wachache, bodaboda walikua wachache na maneno mengine ya kashfa.
Ila watu hao hao wanaobeza maandamano ya jana utawakuata kwenye nyuzi nyingine hapa hapa jamiiforum wanailalamikia serekali
- Kukatika umeme ovyo
- Bidhaa zinapanda bei hovyo,
- mara huduma kwenye ofisi za serekali zimekua mbovu,
- mara kuna upendeleo wa ajira kwenye baadhi ya taasisi za serekali.
- Ubovu wa miundombinu
Ajabu ikitokea mtu anapaza sauti anambeza alafu mda huo huo analalamika ugumu wa maisha hii inaonyesha ni jinsi gani alivyokua mnafki na hii ndo tabia ya watanzania wengi.
Hata kwenye maisha ya kawaida unaweza ukawa unampigania sana mtu ila akienda upande wa pili anakuponda vibaya mno.
Ndo katika yale matatizo matatu ya nyerere aliyoyasema ujinga, umaskini na maradhi inatakiwa liongezeke la nne unafki