Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Hatutaki viongozi mafisadi wala madikteta. Uchaguzi si lazima uwe kati ya aina hizo mbili tu. Na hawa wote kiuhalisia huwa mafisadi kwa mitindo tofauti tu.Wewe unaona sawa familia kama 1000 kuibia Tanzania kwa miaka na miaka. Unafikiri ni kazi rahisi kuwathibiti "kistaraabu".
Wana mirija kila kona, usalama, jeshini, serikalini, polisi, kila sehemu. Hawakubali, hawatakubali kukata, ukate mirija yao, ukiwa "mstaarabu" watakukata wewe. Wanaelewa lugha flani tu. Unafanyaje.
Ustaarabu ni kuchukua kuwasaidia wananchi wengi wa Taifa lako. Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli. Kuzichukua kuna mbinu tofauti na kuna lugha wanayoisikia na kuielewa vizuri, haraka wenyewe kama Mafia, wahuni, majambazi na majangiri waliokubuhu lakini wana uso wa tabasamu na mtandao mzito.
CCM ndiyo imetengeneza mazingira hayo baada ya kuamua kutumia vyombo vya dola na hazina ya taifa kupora haki ya wananchi kuchagua viongozi wanaowataka kupitia sanduku la kura.
Kwanza dikteta anaingiaje kwenye uongozi wa nchi? Kwa kuchaguliwa na wananchi? Kwa katiba? Hakuna kitu kama hicho. Ni ujinga unaoendelea nchini ndio unafanya nchi iendeshwe kihuni na wahuni wanaopokezana zamu baada ya kuvunja nguvu za wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.
Vilio vitaendelea nchi hii hadi siku akili zitakapowarejea wengi hasa machawa wa madikteta na mafisadi wa CCM. Watakapoelewa kuwa subservience kwa wahuni haina tija kwa taifa, hatimaye.