Watanzania wengi ni wanafiki sana

Watanzania wengi ni wanafiki sana

Ufalme ni mfumo ambao upo kila mahali, hata nyumbani wababa huzani wao ndio wafalme hakuna wakuwaambia kitu...

Chadema kuongozwa na Mbowe hakuna tofauti ya raisi wa nchi na kuwa mwenyekiti wa chama.
Ushasema "hudhani". Niongeze nini tena?
 
Hao chadomo miaka yote hatujaona wakitatuwa kero hata moja kwenye majimbo yao.

Kero ya ndani ya chama ya kuwa chama cha kifalme haijatatuliwa.
Ustadhi, nakubaliana na wewe hadharani kuwa kero yao ya msingi ili kuonesha kuwa kweli wanaamini wanachosema imewashinda kuitatua!! Demokrasia katika chama ni tofauti kabisa na chama cha kifalme!
 
Wewe ni nani alikufata akakuomba umpiganie?? Watu mnajipa umuhimu aisee, hata mwenyekiti alieanzisha maandamano sidhani kama ana ego kiasi hicho.
 
Hii ndo sababu ya mimi kugoma kuandamana
Kugoma kuandamana sio suluhisho la matatizo yanayoikabili nchi. Ni jukumu lako kuwatoa Hawa wajinga kutoka kwenye ujinga wao ili waweze kuwakabili wale wanaoneemeka na ujinga wao!
Ccm hawataki kuboresha mfumo wa elimu kwasababu utawala wao unashamili kwa nchi kuwa na wajinga wengi!
 
Pamoja na hayo..naamini asilimia 95% ya wapinzani sio good faith actors.case and point angalia hama hama zao...Wana shida zao kama Mimi na ww,at the end of the day they won't care about the collective if their individual needs are met.
Bila shaka wapinzani walio imara pia umewaona. Hao ndio wa kuthaminishwa. Hao ndio huleta mabadiliko - kama kina Mandela, Nkrumah, Lumumba, Nyerere, n.k.

Sio kila anayedai ni mpinzani anayepaswa kutambuliwa hivyo. Wengine ni watu wa fursa tu. Muda huwafunua. Hao sio kielelezo cha “wapinzani” kwa ujumla.
 
Hao chadomo miaka yote hatujaona wakitatuwa kero hata moja kwenye majimbo yao.

Kero ya ndani ya chama ya kuwa chama cha kifalme haijatatuliwa.
Walikusamya kodi? Au ulitaka watatue kero kivipi? Ccm kodi mnapeleka wapi?
Matatizo ya ndani ya Chadema yanasababisha tukose umeme? Yanapandisha bei za bidhaa?
 
Wote, hata wewe ni mnafiki mkubwa. Upo zaidi kwa tumbo lako.

Kikitokea chuma kikaweka mambo yote sawa unayoyalilia leo, sasa hivi utatafuta sababu zingine kumtukana na kumpinga. Kama ni mshamba, mkabila, kiingereza chake anasema front fed, nguo zake, sio dikteka kamili, sio Mtanzania.

Akiwa dikteta kamili. Mtalia huyu ni bonge la dikteta. Mungu tusaidie. Mnatafuta kiongozi gani?
Unaona vyema kutawaliwa na dikteta, chuma? Ndio aina bora ya uongozi? Yaani uchaguzi ni kati ya kutawaliwa na ama kiongozi mstaarabu lakini dhaifu ama dikteta anayedhibiti ufisadi - wa wengine isipokuwa wake tu?

Hatuwezi kupigania tuweze kuchagua kiongozi mstaarabu mwenye uwezo wa kusimamia ufanisi, weledi, na kudhibiti ufisadi kama nchi makini iliyostaarabika?

Kuna mjadala unaendelea mahali mtandaoni kuhusu jinsi ilivyokuwa rahisi kuwapeleka utumwani Waafrika na kuzifanya nchi zao makoloni - tofauti na mataifa mengine. Hoja kuu ni kuwa Waafrika ni wepesi sana kutii, kutumikia na hata “kuabudu” wenye nguvu. Very subservient. Wanaweza kusalitiana kirahisi kufurahisha wakoloni, wanyapara, madikteta!
 
Unaona vyema kutawaliwa na dikteta, chuma? Ndio aina bora ya uongozi? Yaani uchaguzi ni kati ya kutawaliwa na ama kiongozi mstaarabu lakini dhaifu
Hatuwezi kupigania tuweze kuchagua kiongozi mstaarabu mwenye uwezo wa kusimamia ufanisi, weledi, na kudhibiti ufisadi kama nchi makini iliyostaarabika?

Nipe mfano wa huyu kiongozi. Charactertics zake zitakuwaje kupambana na hawa chini?

Huyu fisadi anaiba bilioni wako kama 100 hivi kwenge genge lao. Huyu anazima umeme kuuza majenereta, huyu anauza mbuga, huyu anafisadi pesa za kujenga hospitali, shule, mwingine anawalipa polisi kuwauwa wote wanaopambania maslahi ya Taifa. Mwingine anauza migodi.
 
Drifter nipe mfano wa kiongozi wa aina yako aliyejenga lolote duniani taifa la wahuni kama hili kwa kutumia vigezo vyako, taifa likasimama kwa miaka hata 100.
 
Unaona vyema kutawaliwa na dikteta, chuma? Ndio aina bora ya uongozi? Yaani uchaguzi ni kati ya kutawaliwa na ama kiongozi mstaarabu lakini dhaifu ama dikteta anayedhibiti ufisadi - wa wengine isipokuwa wake tu?

Wewe unaona sawa familia kama 1000 kuibia Tanzania kwa miaka na miaka. Unafikiri ni kazi rahisi kuwathibiti "kistaraabu".

Wana mirija kila kona, usalama, jeshini, serikalini, polisi, kila sehemu. Hawakubali, hawatakubali kukata, ukate mirija yao, ukiwa "mstaarabu" watakukata wewe. Wanaelewa lugha flani tu. Unafanyaje.

Ustaarabu ni kuchukua kuwasaidia wananchi wengi wa Taifa lako. Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli. Kuzichukua kuna mbinu tofauti na kuna lugha wanayoisikia na kuielewa vizuri, haraka wenyewe kama Mafia, wahuni, majambazi na majangiri waliokubuhu lakini wana uso wa tabasamu na mtandao mzito.
 
Wewe ni nani alikufata akakuomba umpiganie??
Watu mnajipa umuhimu aisee, hata mwenyekiti alieanzisha maandamano sidhani kama ana ego kiasi hicho.
... WATU WENGI HUWA HAWAJUI KUWA SIASA NI 'GAME OF CHANCE &TIMING' ... YAANI HUWA WANAFIKIRI NI KITU CHA "KWELI KABISA!"
😅
 
Jana kulikua na maandamano ya chadema yalikuwa yanalenga kuaddress kero tofauti tofauti na ilikua ni hiyari na sio lazima.

Mimi binafsi sikuandamana sababu watanzania ni wanafki na kumpigania mtu mpumbavu kama Mtanzania ni kupoteza muda na nguvu ila ila kamwe siwezi wabeza waliondomana kwa namna yeyote ile.

Ila ajabu kuna watu wanawabeza chadema mara hawakua na watu wengi walikua wachache, bodaboda walikua wachache na maneno mengine ya kashfa.

Ila watu hao hao wanaobeza maandamano ya jana utawakuata kwenye nyuzi nyingine hapa hapa jamiiforums wanailalamikia serekali
  • Kukatika umeme ovyo
  • Bidhaa zinapanda bei hovyo,
  • mara huduma kwenye ofisi za serekali zimekua mbovu,
  • mara kuna upendeleo wa ajira kwenye baadhi ya taasisi za serikali.
  • Ubovu wa miundombinu
Ajabu ikitokea mtu anapaza sauti anambeza halafu muda huo huo analalamika ugumu wa maisha hii inaonyesha ni jinsi gani alivyokua mnafki na hii ndio tabia ya watanzania wengi.

Hata kwenye maisha ya kawaida unaweza ukawa unampigania sana mtu ila akienda upande wa pili anakuponda vibaya mno.

Ndio katika yale matatizo matatu ya Nyerere aliyoyasema ujinga, umaskini na maradhi inatakiwa liongezeke la nne unafki
Ajabu ikitokea mtu anapaza sauti anambeza halafu muda huo huo analalamika ugumu wa maisha hii inaonyesha ni jinsi gani alivyokua mnafki na hii ndio tabia ya watanzania wengi.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Ila watu hao hao wanaobeza maandamano ya jana utawakuata kwenye nyuzi nyingine hapa hapa jamiiforum wanailalamikia serekali
  • Kukatika umeme ovyo
  • Bidhaa zinapanda bei hovyo,
  • mara huduma kwenye ofisi za serekali zimekua mbovu,
  • mara kuna upendeleo wa ajira kwenye baadhi ya taasisi za serekali.
  • Ubovu wa miundombinu
Ajabu ikitokea mtu anapaza sauti juu ya hizo changamoto anambeza alafu mda huo huo analalamika ugumu wa maisha hii inaonyesha ni jinsi gani alivyokua mnafki na hii ndo tabia ya watanzania wengi.
Kimsingi tuna serikali ya hovyo sn
 
Ajabu ikitokea mtu anapaza sauti anambeza halafu muda huo huo analalamika ugumu wa maisha hii inaonyesha ni jinsi gani alivyokua mnafki na hii ndio tabia ya watanzania wengi.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
Na muda mwingine sio unafiki tu ni uwezo mdogo kichwani tu
 
Back
Top Bottom