Watanzania wengi ni wanafiki sana

Hatutaki viongozi mafisadi wala madikteta. Uchaguzi si lazima uwe kati ya aina hizo mbili tu. Na hawa wote kiuhalisia huwa mafisadi kwa mitindo tofauti tu.

CCM ndiyo imetengeneza mazingira hayo baada ya kuamua kutumia vyombo vya dola na hazina ya taifa kupora haki ya wananchi kuchagua viongozi wanaowataka kupitia sanduku la kura.

Kwanza dikteta anaingiaje kwenye uongozi wa nchi? Kwa kuchaguliwa na wananchi? Kwa katiba? Hakuna kitu kama hicho. Ni ujinga unaoendelea nchini ndio unafanya nchi iendeshwe kihuni na wahuni wanaopokezana zamu baada ya kuvunja nguvu za wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.

Vilio vitaendelea nchi hii hadi siku akili zitakapowarejea wengi hasa machawa wa madikteta na mafisadi wa CCM. Watakapoelewa kuwa subservience kwa wahuni haina tija kwa taifa, hatimaye.
 
... TIMING WALIIKOSEA! ... yaani kama wangepambana na Mzee Magu kama Raila alivyolianzisha na Ruto tungeona KWELI! ... HIT THE IRON WHILE STILL RED HOT!
'NA HII NI KWELI KABISA'! πŸ˜…
Tanzania haya ndo maandamano ya kwanza kurusiwa na serekali tokea mfumo wa vyama vingi kuanza mwaka 1992

Bado wananchi hawakushiriki sababu ya hofu
 
Nilishawahi kusema huko Nyuma, hakuna Watu Wapumbavu na Wanafiki kama Watanzania, kwa Africa hii tunashika namba moja...!

Ukitoka nje ya Tanzania, hata hapa hapa Africa, ukatembelea nchi 2 ama 3, ndo utagundua Uzuzu wa Watanzania.
 
Hayo maandamano si yalikuwa ya wanasiasa , hamna hata sehem mmoja kulikuwa na mambo ya kulalamikia sukari , na kupanda kwa bidhaa , bali ni kupata tume huru itakayowafanya waendele kupata vyeo

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Chadema walichokosea ni kuchomekea mambo ya tume ya uchaguzi, hapo ndio watu wakashtuka, wanaandamana kwa ajili ya maslahi yao binafsi . Usifikiri watu ni wajinga, hiyo ya ugumu wa maisha ni kuzuga tu,
 
Unaf
iki husababishwa na Ujinga !
Mtu mwerevu hawezi kuwa mnafiki !!
 
H
Chadema walichokosea ni kuchomekea mambo ya tume ya uchaguzi, hapo ndio watu wakashtuka, wanaandamana kwa ajili ya maslahi yao binafsi . Usifikiri watu ni wajinga, hiyo ya ugumu wa maisha ni kuzuga tu,
Watu wengi walikuwa wanaamini maandamano yasingekuwepo na wengine walidhani kutakuwepo na vurugu !!
Naamini maandamano mengine yatakapoitishwa utaona tofauti kubwa sana !!
Kwa Dar es salaam maandamano yanafaa miezi ya baridi baridi kuanzi june mpaka September maana miezi mingine ni jua kali sana πŸ˜…πŸ˜…πŸ™
 
Kabisa !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…