Pre GE2025 Watanzania wengi wameanza kumfikiria Dr.Emmanuel Nchimbi kwa nafasi ya juu ya uongozi wa nchi tanzania baada ya Dr.Samia, kulikoni?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huu utafiti umeufanya lini? Tunaomba data.
 
Ndio, zile siasa tu hakuna jipya.
Aristotle aliwahi kusema ikiwa unajiona wewe ni bora zaidi wengine na ukaamua kujitenga na kupuuzia masuala ya uongozi wa kisiasa...,

usije kulaumu kutawaliwa na wapumbavu...

kwasabb wao wataungana na kushiriki masuala ya kisiasa na uongozi na watakua na nguvu ya kuunda serikali na watakuongoza bila mbambamba yoyote huku wewe ukibaki na ubora wako πŸ’
 
Hivi huyu ndo yule Nchimbi ambae hakutokea kwenye mahojiano ya Odemba hadi Odemba akaangusha kilio mbele ya kadamnasi?
kwenye ule ushirikina aloandaliwa sio gentleman? πŸ’
 
Ana busara
 
Unataka kumwingiza mwenzako kwenye vita ambavyo havina macho...Mwache afanye kazi yake ya Sasa Kwa ufanisi...
gentleman,
Roho za vita na mafarakano ni muhimu vikaachiwa kwa Hamas, Ukraine na Russia pekee ,

vinginevyo ushirikina si muhimu kwenye siasa za kistaarabu za Tanzania πŸ’
 
elezea kwa kina kifupi kidogo kwa faida ya wadau πŸ’
Kwetu wananchi wa Kawaida, rangi ya Shati au mlango anakotokea si hoja. Akiwa na dhamira na ushupavu kama yeye alivyo na msimamo usioyumba kwa mambo anayoamini, anaweza kufaa na kutosha kwenye Viatu Kuna watu ndani ya hicho Kikundi ambao wametoka humo na wakawa Viongozi wazuri tu na wazalendo. Mimi kwangu Sifa ya kwanza ni Uzalendo na Ujasiri regardless anatokea mlango up au rangi gani ya Vazi lake. Tatizo la uongozi mbovu hutokana na mwenye kushikilia Usukani siyo Chama wala rangi ya vazi lake. Mungu akipenda 2030 amuongoze afikie Ndoto hiyo. Kuna mengi tunaweza kubadilisha yale ambayo tayari yanaonekana kuharibika , ingawa Mzee yule hajaona kama tumefikia hapo. Katiba ya JMT inatoa nafasi kwa Kila Mtanzania Kuchagua na Kuchaguliwa !
 
Ndani ya CCM presidential materials wapo zaidi ya Mia, 2030 Samia akistaafu kila mwanaccm ataruhusiwa kuomba akiwemo nchimbi pia.
uko sahihi gentleman,
jinsi waTanzania walivyompokea nchimbi, maoni na mitazamo yao yamenipa msukumo wa kuandika bandiko hili muhimu sana kwa maslahi mapana ya waTanzania baada ya Dr Samia Suluhu Hassan kumaliza ngwe yake ya pili uongozini 2030πŸ’
 
CCM wengi kabla ya kushika madaraka huwa waungwana ila akishaapa sio yule tena angalia hata Mama kizimkazi alikuaje angalia na sasa hivi.
 
Unamaanisha SSH HATOGOMBEA 2025?
ni muhimu sana kwenye mabandiko ya kitaalamu na ya kibobevu kama haya,

ukajitahidi kuweka pembeni uvivu wa kusoma vizuri na kwakweli kurudia kusoma na kujiridhisha kabla ya kukurupuka kuuliza chochote, kwasabb ndani yake kuna jibu la swali lako gentleman πŸ’
 
CCM wengi kabla ya kushika madaraka huwa waungwana ila akishaapa sio yule tena angalia hata Mama kizimkazi alikuaje angalia na sasa hivi.
Mambo mengi huwa yanatokana na uwezo au udhaifu wa muhusika as an individual maana anakuwa na Power zote anazohitaji ktekeleza agenda anazoamini kuwa ni sahihi na zitafikisha Taifa kule anakotamani. Kama hana Vision ya nini anataka na wapi twende, basi hapo ndipo tunaona kuwa Chama husika ni kibovu. Katiba na Ilani za Vyama vingi ukizisoma huwa ni nzuri na zinaonyesha mwelekeo mzuri kama ungekuwa unatekelezwa. Tatizo ni Yule anayekuwa amevishwa Kofia . Wengine hawashauriki au wakishashika Nafasi husika hudhania wao wanajua Kila kitu na ni best brain than everybody. Na hapo ndipo tunajikuta katika hali tusiyotarajia na kukatishwa tamaa. Siyo kila mmoja anaweza kuvaa Viatu hivyo, lazima tuwe wa kweli. Greater Leaders are Born Leaders, not made.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…