Watanzania wengi wapo slow karibu kwa kila kitu



Madhara ya kuishi ulaya halafu uje bongo uuuiiiii.

Kujuana ndio usiombee, kwenye ajira serikalini nenda mawizarani huko. Mwendo wanagamilia.

Kuna jamaa angu class mate college pamoja yaani amepayata wizara flan, kabla ya happy aliwekwa TPA amehamia wizarani anataka aondoke kisa hakuna masurufu. Unategemea huyu mtumishi atajali mteja??
 
Ni kweli kabisa watanzania hatupendi kwenda na muda hata ukija kwenye upande wa usafiri bado ni changamoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu yupo kuhutubiq anaanza, Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama yetu Dr. Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Dr. Philip Isdori Mpango, Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa...... hao ni watu watatu tu wa.etambulishwa, amalize utambulisho tayari dk5 zimepita.

Tatizo hili ni kubwa sana...hatuna haraka kwa lolote!
 
Kwanini ufikirie kuwa mgeni wa fulani? Hayo ni mawazo tegemezi.

Siku zote fikiri kujitegemea / kutegemewa siyo kutegemea.

Wazungu inahusu nini?
Ndo maana nikasema utamaduni. Utamaduni wa wazungu wa kujitenga hatuuwezi Wao wana Kila kitu siyo bongo.

Unaacha kusalimia watu baada ya siku mbili linakukuta la kukuta utajuta kuzaliwa
 
Nilikaa CRDB Mbagala kuanzia saa nne asubuhi mpka saa kumi na moja kisa kufungua account tu
 
Kuna duka la jumla nilienda kununua bidhaa, aisee sijawahi ona watu wako slow kama wale. Duka lina wafanyakazi kama 8 hivi na sio kubwa sana, ila haoo utasimama mpaka uwahimize wakufanyie upesi.

Kila mwenye jukumu anajivuta mno kama una haraka zako hata hizo bidhaa unahairisha kuchukua.
 

Hapo karibu wote wameajiriwa. Wajitume Duka la Baba Yao, ndio watakujibu hivyo
 
Na hata kutembea barabarani utakuta mtu njia yote kakaba yeye anetembea pole pole utafikiri bank ana milioni 100 kumbe balance ni negative.
Hii ni kero sana hasa miji kama Dar. Si ajabu tunaburuza kwenye maendeleo kwa sababu watu hawafiki waendako kwa wakati. Unapita barabarani saa 3 nanusu asubuhi bado trafiki imekamata. Mi nachukua shortcuts kukwepa magoigoi. Huu uzi wenyewe sana
 
Hizo hotuba tu za viongozi maamkizi na pongezi kurasa 2 mtu anapoteza muda dakika 3 anasalimia tu kabla ya hotuba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…