Watanzania wengi wapo slow karibu kwa kila kitu

Watanzania wengi wapo slow karibu kwa kila kitu

Ni kweli wabongo tupo very slow kwenye utoaji wa huduma, utaona mhudumu anaacha foleni anaenda kula badala ahudumie haraka amalize ndo aende.
• majiono na majigambo ya watoa huduma wanajiona wao ni tabaka jingine hapa duniani, dharau kwa wateja aisee! Ni janga kwakweli

Kula sio tatizo, tatizo linakuja anakula Kwa muda gani. Hapo ndipo shughuli ilipo.
Mtu anafika ofisini labda saa mbili Asubuhi, aanze kujizungusha weee! Kazi aanze saa tatu kasorobo kisha akihudumia tena mara atoketoke mara aingie Mfanyakazi mwenzake wajadili ishu za jana usiku, wewe imekaa tuu.
Saa nne imefika huyo kunywa chai, atakaa dakika 40 hiyo ni saa tano, kisha lunch ni saa Saba unusu saa nane.

Noma Sana.
 
Kuna Baadhi ya Mapadre na Maaskofu ni wabovu kwenye kutunza muda , unakuta wanatangaza misa itafanyika saa nne wao wanafika eneo la tukio saa sita !

Mtu akizidisha dakika kumi za makubaliano naondoka hiyo sehemu.

😂😂😂
 
watanzania wengi hawapendi kujishughulisha wanataka kubembelezwa tu na kuomba misaada wkt nchi ina raslimali nyingi

Wabongo kiboko Yao ni Wahindi. Hao ndio kiboko Yao.
Wahindi wapo Makini kwenye ishu ya muda, sasa wabongo Kwa vile Hawana nidhamu ya muda wakisimamiwa wanasema wanaoelekeshwa😂😂.

Mbongo anataka kazi ya dakika tano afanye Nusu saa.
Mpe fundi nguo kazi mwambie lini itakamilika, alafu nenda hiyo siku uone mtakavyozungushana, sio ajabu ukamaliza mwezi mzima kufuatilia hiyo nguo
 
Ukijaribu kufanya utafiti mzuri yote uliyoandika ni sawa na ukichunguza zaidi watu wanaishi na matatizo ya akili yaani unaweza kushangaa asilimia 50 watumishi wa umma wana matatizo ya akili hapo ndio utajua kwa nini hakuna maendeleo, hawajiulizi kwa nini sekta binafsi au mashirika binafsi yanaendelea na kudeliver vizuri lakini kwenye mashirika ya umma hakuna jipya
 
Nchi ambayo wakijenga shimo la choo cha soko, wanamshukuru Mungu na wanamshukuru rais kuwapelekea pesa hawajui kama ni kodi zao hao unadhani wana akili timamu

😀😀😀
Elimu bado ni muhimu.
Na sio Elimu tuu Hii ya darasani ambayo Dada FaizaFoxy anasema tumeenda kusomea ujinga. Bali ni Elimu ya kujitambua na kujitegemea ambayo mara nyingi hutolewa na Wazazi Kwa Mtoto.
 
Nilifika Rita pale makao makuu kufuatilia cheti cha mwanangu.
Mapokezi wakanambia nifike floor namba x kisha nimuulizie mtu kwa jina x.
Kufika palw nikamkuta mzee mmoja kanuna nuna.
Nikamuulizia mlengwa.
Mimi: shkamoo mzee, namuulizia flan
Mzee: simjui (huku kanuna na hajaikia salamu yangu)
Mimi: nimeambiwa yuko ofisi hii
Mzee: mpigie simu (kafyumu kinoma)

(hapa sasa nikawa nishakereka maana naona dingi kakaa kisharishari tuu na mimi nina haraka zangu ikabidi niweke heshima pembeni kabisaa niwe na mimi jeuri maana hawa wazee wa siku hiz wengi washenzi)

Mimi: sasa mimi nampigiaje mtu simu na simjui.Nipe namba zake basi mbona umekaa kijeuri jeuri hivyo mzee wangu??? (Hapo niliongea kijeuri haswaa)

Mzee: unasemaje wewe?

Mimi: umesikia nilichisema .nipe namba yake nimtafute.

Mzee: unajua mimi ni nani?

Mimi: sina mpango wa kujua wewe nani maana hunisaidii kwa lolote lililonileta hapa.
Mimi siko hapa kwasababu yako ila wewe uko hapa kwasababu yangu mimi hivyo jifunze kuwa na adabu kwa wateja.Usitake kunyenyekewa kwa vitu ambavyo ni wajibu wako.

Yule mzee akanichekiii kisha akatoa namba.

Nikamaliza ishu zangu nikasepa
 
Ukijaribu kufanya utafiti mzuri yote uliyoandika ni sawa na ukichunguza zaidi watu wanaishi na matatizo ya akili yaani unaweza kushangaa asilimia 50 watumishi wa umma wana matatizo ya akili hapo ndio utajua kwa nini hakuna maendeleo, hawajiulizi kwa nini sekta binafsi au mashirika binafsi yanaendelea na kudeliver vizuri lakini kwenye mashirika ya umma hakuna jipya

Mashirika binafsi yanawasimamizi wasiotaka mchezo, kwani Ile kwao ni biashara.

Mbongo anaweza lialia anataka Ajira utadhani ukimpa hiyo Ajira kuna kitu cha maana atafanya(sio wote lakini).
Mpe Ajira, utashangaa anawasumbua Wananchi anaowahudumia Wakati wale ndio wanafanya alipwe Mshahara.

Yaani badala awaheshimu na kuwahudumia Kwa Moyo WA upendo, Yeye analeta dharau, ndio maana mbongo kujiajiri ni kazi Kwa sababu kuanzia akili na mfumo wa Maisha haum- support kufanya hivyo.
Customer care Zero
 
mimi wa kwanza
ukweli nimekosa mambo mengi mazuri kwa ajili ya kuwa slow.

nimesha tia hasara napo fanyia kazi kwa ajili ya kuwa slow.

tunahitaji kubadirika, yaani unakuta una kikao sa 4 unaanza jiandaa sa 3 na dk 50 hadi sa 4 bado unaenda kikaoni sa 4 na nusu unakuta hata kikako hakijaanza (nao ni wale wale wako slow)
 
Nilifika Rita pale makao makuu kufuatilia cheti cha mwanangu.
Mapokezi wakanambia nifike floor namba x kisha nimuulizie mtu kwa jina x.
Kufika palw nikamkuta mzee mmoja kanuna nuna.
Nikamuulizia mlengwa.
Mimi: shkamoo mzee, namuulizia flan
Mzee: simjui (huku kanuna na hajaikia salamu yangu)
Mimi: nimeambiwa yuko ofisi hii
Mzee: mpigie simu (kafyumu kinoma)

(hapa sasa nikawa nishakereka maana naona dingi kakaa kisharishari tuu na mimi nina haraka zangu ikabidi niweke heshima pembeni kabisaa niwe na mimi jeuri maana hawa wazee wa siku hiz wengi washenzi)

Mimi: sasa mimi nampigiaje mtu simu na simjui.Nipe namba zake basi mbona umekaa kijeuri jeuri hivyo mzee wangu??? (Hapo niliongea kijeuri haswaa)

Mzee: unasemaje wewe?

Mimi: umesikia nilichisema .nipe namba yake nimtafute.

Mzee: unajua mimi ni nani?

Mimi: sina mpango wa kujua wewe nani maana hunisaidii kwa lolote lililonileta hapa.
Mimi siko hapa kwasababu yako ila wewe uko hapa kwasababub yangu mimi hivyo jifunze kuwa na asabu kwa wateja.Usitake kunyenyekewa kwa vitu ambavyo ni wajibu wako.

Yule mzee akanichekiii kisha akatoa namba.

Nikamaliza ishu zangu nikasepa

Kazi nzuri Sana.
Jitu kama hilo hiyo ndio Dawa yake,
Wanapenda KUABUDIWA sijui Kwa nini?
 
Hili ni tatizo sugu kabisa hata pale UDSM wako very slow.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
Pale mambo kuwa slow ni pamoja na ukweli kuwa watumishi,(supporting staff) hawathaminiwi.

Kasi ya watumishi kuomba kuhama kwenda taasis nyingine ni kubwa sana, lakin mbaya zaidi wanazuiliwa kuondoka, hali hii inafifisha utendaji kazi.

Case ya UDSM inahitaji wizara ya mambo ya utumishi kuingilia kati, maana hali ni tete, watu wanalalamiki shughuli haziendi, lakin deep down tatizo ni watumishi kufanyiwa ndivyo sivyo.

Huwezi kumzuia mtu kuhama alafu utegemee matokeo chanya kutoka kwake, sio rahisi!

UDSM kwa sasa ndio imekuwa ikijifunza kwa Vyuo kama UDOM na SUA, ambapo watumishi wanafurahia kufanya kazi kwenye mazingira bora.

Utumishi wana kitu cha kufanya ili kupunguza rate ya watu kukimbia pale, ingawa wengi wanazuiliwa, na kuzuiliwa huku ndio kunapelekea utendaji mbovu na kuchelewa kwa mambo meengi.
 
Si unajua tena.ukipata kazi serikalini basi ndio mkataba wa maisha huo

Ni kweli Kabisa. Watu wafundishwe maadili.
Utashangaa kijana amesota miaka nenda Rudi, Kwa bahati hizi Ajira za tamisemi kaomba alafu kapata, nenda kamfuatilie Huko kazini uone anachokifanya, miezi sita mingi utashangaa ujingaujinga tuu!

Watu Hawana Upendo Kwa wengine ndio maana haya yanatokea.
 
Back
Top Bottom