cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
Wamejaa teleeeWengi tu huko chamani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wamejaa teleeeWengi tu huko chamani
Huwa kuna mother tongue gakuna father tongue,lafudhi ya mtoto mara nyingi huegemea upande wamama,kama ningekylia bara au ujombani ,ningeongea kama waoIdara ya uhamiaji izidi kuwa makini Sana kwa hawa watu..
Kosa tunaaloliona Leo Congo DRC.ndio ili ili la kuwapa Hali raia Watutsi..
Mleta mada..Umeandika upo ujombani! Ujui ujombani kwako ni wapi!Malezi yanajifunga na kuelekeza kukulia kwako pwani ni kujulisha Pwani imeiusaidia kujifunza lugha na nasaba yako si Tanzania...
Aisee! Wakati mwingine yatakiwa ujiongeze kwa kuwa na maarifa mbadala kutokana na alama za nyakati.Mimi nina asili ya kitutsi kwa upande wa mama, baba yangu ni mzaliwa wa Msoga.
Nguvu ya nama nikapewa jina la ujombani la kwanza, kosa kubwa..
Wiki mbili zilizopita kulikuwa na zoezi la kuandikisha NiDA wilayani kwetu, wajihi wangu mrefu na hili jina nusura viniponze sema kiswahili changu ni cha mwambao maana nimekulia Pwani ila niko huku kikazi ujombani.
Kuna mwenzangu aliambiwa atamke nne akasema ine, boksi akatamka bokisi, alipigwa pingu pale pale mpaka walipojiridhisha kuwa amezaliwa Ngara.
Kijijini kwa mama asilimia 50 ni wahamiaji wa kitutsi wenye miaka mingi sana sema wanajiita kabila la hapo wilaya walipo.
Sina lengo la kuwapinga Mamlaka ya Vitambulisho maana lazima wajiridhishe na uraia wa wanaovihitaji ila mlijua kutuchangamsha.
Kuanzia Kahama, Nasumbwe, Runzewe, Ushirombo, Ngara, Karagwe, Biharamulo watutsi ni wengi sana ni kama tuko Rwanda tu. Tunaishi nao na tumezaa nao, sijajua miaka 20 ijayo itakuwaje wakiamua watambulike kama kabila rasmi la Tanzania?
Na wewe mdukuzingara23 muhangaza wa murugwanza ngara jirani ya eric david nampesya mtangazaji wa BBC sema ndio hao hao tu,kutoka ngara mpaka rusumo mpakani mwa rwanda au kabanga mpakani nwa burundi unaenda kwa baiskeli tu
Wanasaidia uchumi wa nchi. Hata Zambia na Malawi kuna wanyakyusa wameshika uchumi wa huko.Nashangaa serikali na vyombo vyake hawakuliona hili
Ila we mwamba umetisha,ulipunguza sana miakaAisee! Wakati mwingine yatakiwa ujiongeze kwa kuwa na maarifa mbadala kutokana na alama za nyakati.
Mimi natoka Rulenge wilayani Ngara na mama yangu ni muhangaza wa Kabanga na ni katika haohao wenye muonekano wa kitutsi.
Mwaka 2013 nilikuwa na shida ya kupata hati ya kusafiria (passport) kwenda moja ya nchi za kiarabu kutafuta fursa.
Mwaka huohuo serikali ya JK ilikuwa imetangaza operation Kimbunga iliyokuwa inalenga kusaka wahamiaji haramu na kuwarudisha makwao.
Pale kwetu Rulenge kuna watu nimekuwa nao , kucheza nao na kusoma nao lakini kwa sababu wazazi wao walitokea nchi jirani wakaja kufia Tanzania watoto hao ambao sasa wameishakuwa watu wazima walitakiwa kurudi Rwanda au Burundi japo wao hawajui wazazi hao walikuwa wakiishi maeneo gani ya nchi walizotoka. Msichana alikimbia vita ya wenyewe kwa wenyewe, kufika TZ akaolewa na kijana wa kiTZ, akazaa watoto akazeeka, akafa na kuacha watoto katika ardhi ya TZ.
Mimi nilivyosoma mazingira ya operation ile ya Kimbunga, nilijua kwamba kwa mtu anayetoka katika mkoa unaopakana na nchi jirani hasa sisi wa mikoa ya Kagera na Kigoma tunaopakana na Rwanda, Burundi, Uganda na DRC ingekuwa kazi ngumu sana kupata passport kwani ingebidi hadi wanipeleleze sana na kwa muda mrefu na kujiridhisha kuwa mimi sio mhamiaji haramu.
Baada ya kuona kwamba nikifuata sheria nitalazimika kuchelewa kupata ninachokitaka na mipango yangu kuharibika nililazimika kutumia pesa kupata ninachokitaka ndani ya wakati ninaotaka.
Kwa kutumia pesa nilipata CHETI CHA KUZALIWA kinachoonyesha kuwa nimezaliwa Kigogo kata ya Kinondoni DSM na cheti cha kumaliza elimu ya msingi kinachoonyesha kuwa nimehitimu darasa la saba shule ya msingi misufini, kata ya Kigogo, wilaya ya Kinondoni DSM.
Na kwakuwa shughuli niliyokuwa naenda kuifanya nje ya nchi ilihitaji niwe na umri wa miaka 25 kurudi chini , CHETI CHA KUZALIWA, CHETI CHA ELIMU YA MSINGI NA PASSPORT yenyewe vyote vilionyesha kwamba nimezaliwa mwaka 1993 , japo uhalisia ni kwamba wakati CCM inazaliwa mama yangu alikuwa na ujauzito wa miezi sita.
HIYO NDIYO DAR ES SALAAM ukiwa na pesa unapata kila kitu unachokitaka kwa wakati unaoutaka isipokuwa roho ya binadamu tu!. ,
Sawa.!.Chanyamisa,Nyaishozi,Karagwe
Afisa yeyote aliyeniuliza mbona sura yako na umri wako havifanani ?! Nilimpa maelezo mafupi yaliyosindikizwa na noti moja ya elfu 5 na maswali yakaishia hapo!Ila we mwamba umetisha,ulipunguza sana miaka
Umetaja Rulenge,umenikumbusha nyumbani,kuanzia kabanga nickel,bigombo,npanyura,kashinga,kibirizi ,nawafahamu akina mzee brukadi,mwampamba,byagira,ngeze,na mapadri wote waparokia ya rulenge,niseme tu ile tarafa ya bushubi imejaa wageni toka rwanda au burundi
Wasituletee 'U-M23' tu ?....😂😂😂Muwe makini sasa mkianzisha yale mavalangati yenu ya M23, hatuta wavumilia.
Nilisoma na jamaa mmoja, tulidhani ni mtanzania mwenzetu hata uongozi tukampa, alipomaliza shule tukasikia yuko Rwanda na ni mnyarwanda.Hilo ni kitu huwa najiuliza sana ni kama wapemba na uarabuni,yaani wanyaranda ni wazalendo kwa nchi yao kupitiliza.mimi mwenyewe kuna sumaku inanivuta kuishi huku japo ninezaliwa pwani
Tumedharauliwa sana, wametufanyia ushenzi wa kila aina wautakaoNaamini serikali haijalala,
Kagame amegusa pabaya na kibaya zaidi watu wenye vyeo na wenye asili ya huko anaojidaia ndani ya nchi za jirani zake watapata shida wasizostahili.
Hii itabidi niipe jina la Operation ya KIMYA KIMYA CHINI YA KAPETI.
Hatuwezi kudharauliwa kwa kiasi hicho.
Nakukumbusha tu passport Sio uraia.Aisee! Wakati mwingine yatakiwa ujiongeze kwa kuwa na maarifa mbadala kutokana na alama za nyakati.
Mimi natoka Rulenge wilayani Ngara na mama yangu ni muhangaza wa Kabanga na ni katika haohao wenye muonekano wa kitutsi.
Mwaka 2013 nilikuwa na shida ya kupata hati ya kusafiria (passport) kwenda moja ya nchi za kiarabu kutafuta fursa.
Mwaka huohuo serikali ya JK ilikuwa imetangaza operation Kimbunga iliyokuwa inalenga kusaka wahamiaji haramu na kuwarudisha makwao.
Pale kwetu Rulenge kuna watu nimekuwa nao , kucheza nao na kusoma nao lakini kwa sababu wazazi wao walitokea nchi jirani wakaja kufia Tanzania watoto hao ambao sasa wameishakuwa watu wazima walitakiwa kurudi Rwanda au Burundi japo wao hawajui wazazi hao walikuwa wakiishi maeneo gani ya nchi walizotoka. Msichana alikimbia vita ya wenyewe kwa wenyewe, kufika TZ akaolewa na kijana wa kiTZ, akazaa watoto akazeeka, akafa na kuacha watoto katika ardhi ya TZ.
Mimi nilivyosoma mazingira ya operation ile ya Kimbunga, nilijua kwamba kwa mtu anayetoka katika mkoa unaopakana na nchi jirani hasa sisi wa mikoa ya Kagera na Kigoma tunaopakana na Rwanda, Burundi, Uganda na DRC ingekuwa kazi ngumu sana kupata passport kwani ingebidi hadi wanipeleleze sana na kwa muda mrefu na kujiridhisha kuwa mimi sio mhamiaji haramu.
Baada ya kuona kwamba nikifuata sheria nitalazimika kuchelewa kupata ninachokitaka na mipango yangu kuharibika nililazimika kutumia pesa kupata ninachokitaka ndani ya wakati ninaotaka.
Kwa kutumia pesa nilipata CHETI CHA KUZALIWA kinachoonyesha kuwa nimezaliwa Kigogo kata ya Kinondoni DSM na cheti cha kumaliza elimu ya msingi kinachoonyesha kuwa nimehitimu darasa la saba shule ya msingi misufini, kata ya Kigogo, wilaya ya Kinondoni DSM.
Na kwakuwa shughuli niliyokuwa naenda kuifanya nje ya nchi ilihitaji niwe na umri wa miaka 25 kurudi chini , CHETI CHA KUZALIWA, CHETI CHA ELIMU YA MSINGI NA PASSPORT yenyewe vyote vilionyesha kwamba nimezaliwa mwaka 1993 , japo uhalisia ni kwamba wakati CCM inazaliwa mama yangu alikuwa na ujauzito wa miezi sita.
HIYO NDIYO DAR ES SALAAM ukiwa na pesa unapata kila kitu unachokitaka kwa wakati unaoutaka isipokuwa roho ya binadamu tu!. ,
Hapana ! Kuna watutsi wa TZ wanaoitwa wahangaza au washubi. Kuna watutsi wa Rwanda na watutsi wa Burundi na watutsi wa Uganda nadhani DRC pia wapo!.Nakukumbusha tu passport Sio uraia.
Nyie inabidi mrudi kwenu Rwanda hatuwataki kwetu mmejaa roho mbaya na ndio kiini cha machafuko Easter Africa and Central