Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Vidudu mpaka la saba kama inawezekana msaidie tu mtoto angalau ajue kusema yes, I am hungry asije kufa njaa. Shule iwe ya serikali au private lakini awe vizuri kwenye lugha, ikishindikana mlipe hata ras amfunze maana fainali ni pale anapotakiwa ajieleze kwa kingereza. Mtu ana degree ila ze ze ze ze nyingiiiii. Na ana mi A ya kutosha aliyofaulu kwa kingereza.
 
Wanawalea kimayai mwishowe watoto wanashindwa kucope na maisha halisia wanajisetia standards za kijinga wanajikuta wanajiingiza kwenye tamaa na kuishia kuwa mashoga.

Wazazi usione soo kuwaambia watoto wako uhalisia wa maisha.Hao watoto kama hawataki wajiue pumbavu hakuna kulea ujingaujinga.
 
Sio kweli mzazi asomeshe mtoto mamilioni kuanzia chekechea,msingi,sekondari hadi chuo kikuu bila mkopo wa bodi ya mikopo halafu mwishowe amwache mtoto ahangaike kutafuta elfu 10 kwa siku posho ya uber au bolt au bodaboda

Hiyo pesa aweza tu pewa na mzazi kama pocket money

Wengi wakimaliza kama kazi hamna huendelea kuomba wazazi wao wawalipie wasome Masters hadi Phd ndani ya nchi na nje

Vyuo vingi waulize idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masters na Phd nani anawalipia watakwambia wanajilipia wenyewe na ni walipaji wazuri mno hawasumbui ada

Wazazi hawawaachi bure au kuwaacha waendeshe boda boda au uber au bajaj labda mtoto mwenyewe agome

Wengi sasa hivi wamejazana kwenye digrii za juu wanasoma hatari wakisubiri ajira huko huko huku wanapiga kitabu

Kukitangazwa nafasi za masters na Phd wanazichukua chapchap sababu tayari wanazo mkononi hawahitaji kusomeshwa na mwajiri au mfadhili
 
Hakuna mzazi anapenda mwanae asome katika huu uchafu,ndio maana baadhi wanafanya juu chini wakope wauze mashamba watoto wao wasome sehemu inayoeleweka.
Halafu sio sifa mwanafunzi kusoma mazingira ya ajabu ajabu
 
Unasema nini wewe bure kabisa, embu ongea vitu vyenye akili.Mtaani huku hizo shit masters degrees na bachelor degrees zipo kibao na kuna wengine walienda mpaka kusoma nje ya nchi wamerudi hawana ramani wapo mtaani kula kulala kwa wazazi wao.


Sasa kama 1st degree umesoma imeshindwa kukutoa hiyo masters unasoma ndo itakutoa???😀😀😀😀. Alafu watu wanaoenda kusoma masters huku hata alichosomea degree ya kwanza hajakifanyia kazi huwa nawaona wajinga flani hivi.Maana masters hiyo unayojilipia ungekuwa na job experience ungepata scholarship chap ukasoma kwa scholarship.

Alafu unasomaje masters huna kazi😀😀😀😀hivi vyuo hawawezi kuwaambia ukweli kwasababu wanafanya biashara ila ukija kwenye soko la ajira ndo utaelewa namaanisha nini.
 
Masters watu wanasomea zenye soko kubwa na ndio mabosi wa hao wenye digrii moja Wanakuwa tayari wabajua gap liko wapi wanaenda lijaza kwa kusomea hawarudii kitu kilekiie wamesomea first degree

Wanakuwa wameshafanya utafiti wapi kuna mwanya wa kutoboa kwa level ya masters na Phd sababu wanaenda wakiwa watu wazima sio kama degree ya kwanza walienda wakiwa watoto
 
Walimu wenyewe wa English Medium wamesoma Kayumba. Maneno ya mlevi mmoja

Tutafute hela wakuu, tupeleke watoto shule za mabasi ya njano ambapo wanakula, wanasoma mazingira rafiki na wanajifunza lugha ya kiingereza.
 
Mtoto kama ni nyumbu ni nyumbu tu hata umtoe serengeti umpeleke mbuga za wanyama ulaya atabaki kuwa nyumbu zezeta tu la serengeti
 
kijana wewe inavyoonyesha haupo kwenye ajira.Wewe bado ni DREAMER.KEEP DREAMING, NI RAHA SANA KUOTA ILA GROUND MAMBO NI TAFRANI!!!!

Structure ya kuja kuwa boss haitegemei tu hiyo Elimu kubwa na unavyojitutumua ujue ya kuwa huko makazini watu wapo kila mwaka wanaenda shule tena wenzako wanachungulia fursa iliyopo hapo kitengoni kwao ndo wanaomba kwenda shule.

Sasa wewe wa masters yako ya mchongo utoke uko ilikotoka watu wapo kitengoni miaka na miaka wamekaimu na wanajua kazi wanajua utaratibu wa ofisi alafu wewe kidampa mmoja umeajiriwa na kidegree chako unataka kuja kuwaovertake uliowakuta kijana MIFUMO ITAKUTEMA hutaamini😀😀😀😀huko makazini ni mifumo tu ndo inafanya kazi🤗 na cheo UNAPANDA sio vya kupewa.

Kuwa na masters isiyoendana na 1st degree inaweza kuwa ni upotevu wa muda kwa asilimia kubwa labda kama unasoma for FUN.Tunategemea mtu aliamua kufanya masters ni yule aliyeamua kuwa mbobevu wa eneo ambalo yupo analifanyia kazi.Tofauti na hapo wewe hujui nini unataka unasoma ili mradi tu utambulike unamasters degree,Poor you!!!

Sasa wewe jidanganye kuwa ukishaajiriwa tu unakuwa boss🤗🤗🤗 unapewa kitengo huku hujui kitu.Acheni kudanganyana huko vijiweni mnapoteza muda.

Ukitaka kufanikiwa tafuta mtu awe CAREER ADVICER wako awe anakugaide na huyu mtu utakayemchagua hakikisha ni mtu smart katika hiyo fani yako ili uwe na muelekeo sahihi. Acha na hiyo peer ideology mnajazana ujinga huko mkienda makazini mnaishua kuwa disapointed!!
 
Safi. Ndivyo maisha yalivyo; kila mtu anapambana na jinamizi lake.
 
Mipiango yangu.
1. Shule ya Msingi watoto wasome Government
2. Secondary Watoto wasome private za wakatoliki(Hapa sana sana wakike).
3. Advance - Government
4. Chuo - Government

Kwisha hyo.
 
Mwandiko mzuri mkuu
 
Kusomesha mtoto English Medium Tz na kayumba kwa upande wangu sio kama wanatofautiana. Angalau umpeleke njee.
 
Umefafanua vizuri sana wa Tz bado wako nyuma sana kilicho wa vuruga wengi ni vile shule ya kingereza bila kujali kama mitaala ina fanana, Na mitihani ya Taifa wanafanya kwa pamoja.
 
Hivi vitu vinawasumbua nyinyi wazazi. Mtoto wala habari hana labda mtoto wako lama amashinda njaa. Ila mengine ni mizigo mnajipqchika wazazi wa dotcom
100% Fact
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…