Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Hiyo uliyo soma itakuwa Kayumba ya kijijini interior ndani ndani
 
Nafikiri ifike mahala tuache tabia ya kupangia watu hata yale mambo ya kibinafsi!!!!
Mtu asomeshe mtoto wake anapo ona inafaa; Kayumba, English medium, Uganda, Kenya, South Africa, Ulaya nk mbona kote huko watoto wakitanzania wanasoma na wako poa tu?
Kwani amekushikia bunduki? Una pata wapi ujasiri WA kusema amekupangia?


As a matter of fact wewe ndio una mpangia cha kuzungumza.

Acha utoto mkuu
 
Mdogo wangu ,hongera Sana aisee ,vipi nikihitaji uwe unakuja kunipiga msasa wa kiinglishi utakubali ?
Malipo yatakuwepo 🧐
 
So wewe ni tajiri mkuu?

Matajiri wanaongeaga hivyo?


Kama na wewe ni tajiri Basi there is no hope to the future.

Mwenzako ka share story Yake Kwa sababu anataka kuwasaidia na watanzania wenzake wanao poteza pesa zao bure
Nani kamuomba ushauri? Pesa zao zinamhusu nini?

Kuwa na pesa siyo lazima uwe tajiri Chief.

Afungue ofisi wenye shida ya ushauri wake watamfuata huko.
 
Mateso niliyoyapitia kayumba sitaki mwanangu ayapitie kitaeleweka tu.
Wewe Tena " Mideko" . Ukideka tu Kwa Hassan, Juma na Kelvin ada hiyo hapo. Mwenzako Fateema anatafuta hela Yake Kwa jasho ndio maana anaona ni upuuzi kulipa mamilioni shule za EMs wakati hana assets za maana na ana option ya kuwasomesha Kayumba
 
Mkuu maisha magumu kwa mtu moja sio wote mualimu kunywa maji ya dawsco sio poa kabisa au kubeba viazi shuleni kama vitafunwa vya chai ni kujidhalklishwa.
Kuna ndugu yangu mmoja ndio lilikuwa life lake tena shule alikuwa anaenda na baiskeli kabeba viazi vitamu na karanga na chupa ya maji lita 1.5 ...kila siku alikuwa ananiambia maisha sio lele mama..ila sasa hivi maisha yamenyookea kinamna
 
Subiri aende secondari ndio utajua english ni bora.
Kuna jamaa mmoja kwao alikuwa mambo safi... kuanzia chekechea hadi sekondari kasoma EM hadi chuo kaenda ST niniliu... lakini kingereza bado changamoto... kingine mnavyo shadadia kingereza,, kwani kinaongeza nini kwenye uchumi wako zaidi ya kuwa mtumwa tu? Kama kijua jifunze tu lakini usidhani ya kwamba kujua kingereza ni hakika ya mafanikio yako......
 
Wewe Tena " Mideko" . Ukideka tu Kwa Hassan, Juma na Kelvin ada hiyo hapo. Mwenzako Fateema anatafuta hela Yake Kwa jasho ndio maana anaona ni upuuzi kulipa mamilioni shule za EMs wakati hana assets za maana na ana option ya kuwasomesha Kayumba
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Hatari sana
 
100% Fact
 
Sahihi chukua mtoto wa darasa la saba kayumba waongee kiingereza na mtoto wa English medium darasa la pili

Kitoto cha English Medium kitamtoa knock out huyo darasa la saba wa kayumba
Vinaongea kingereza kilichonyooka na vinajiamini.
Mtoto wako wa EM anaenda kuishia UDSM kama wa Kayumba. Wakimaliza hapo wote wanakuwa products za UDSM. Nobody gives a fu.ck where he went in Nursery/Primary school.
 
Ukitaka uishi maisha ya tabu basi ishi ili uwaridhishe jamii.

Kama mpunga upo somesha kwa kina Emmy ,kama hauna somesha Kayumba.
 
Umeongea kinyume chake mkuu. The vice versa is true.

Watoto wa Kayumba ndio WaPo wengi Zaidi mtaani na ndio wana enjoy Zaidi michezo mtaani.

Halafu kusema watoto eti wanaumia kutopanda magari ya njano ni uongo mtupu, ni kwamba hujui saikolojia ya watoto.

Ni wewe mzazi " brainwashed" ndio una umia kuona watoto wa wenzako wanapanda gari la njano kwenda shule na Sio mtoto.


Usikute mtoto wako anawaza kuwa kama Mzize au Kondeboy Hermonize
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…