Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Daaah! kweli wateuliwa wametisha,chama cha kitaaluma lazima kiheshimiwe.
 
Hii ni nzuri sana.

Mtu unateuliwa kwa mbwembwe unaacha shughuki zako baada ya mwaka unatupwa nje ya uteuzi kwa aibu. Hizi nafasi za uteuzi waachiwe majibless na makada tu hazina maana ni kuharibiana maisha kwa kutenguana hivyo hovyo.
Nakusalimia mkuu..🙋‍♂️
 
Hapo wame angalia maslahi huwezi kutoka kwenye mshahara wa m10 na kwenda kwenye mshahara wa m3, kazi za kuteuliwa hazina uhai unaweza kuteuliwa leo kesho ukafukuzwa.hao jamaa wako sahihi kabisa
 
Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

21 September 2023
Uvinza, Kigoma
Tanzania

Uvinza kwa waka moto, mheshimiwa waziri mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa awa mbogo


View: https://m.youtube.com/watch?v=osWgD5N1OuU

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa akiongea akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi CP Thobias Andengenye, mkuu wa wilaya ya Uvinza DC Dina Dina Mathamani, mkurugenzi wa mtendaji wa halmashauri ya Uvinza Bi. Zainab Mbunda na vigogo wengine wa mkoa wa Kigoma, waziri mkuu ahoji uongozi kushidwa kuhakikisha majengo mapya ya hospitali na vifaa tiba kuanza kufanya kazi ya kutoa huduma kwa wananchi.


TOKA MAKTABA:
31 January 2023

RC ANDENGENYE AMUAPISHA MKUU WA WILAYA UVINZA​


Posted On: January 31st, 2023

1695333930431.png

HABARI PICHA: HAFLA YA KUMUAPISHA MKUU WA WILAYA YA UVINZA DINAH MATHAMANI ILIYOFANYIKA JANURI 31, 2023 KATIKA UKUMBI WA KATIBU TAWALA OFISI YA MKUU WA MKOA KIGOMA
Source : https://kigoma.go.tz/new/rc-andengenye-amuapisha-mkuu-wa-wilaya-uvinza-5
 
Hao jamaa kwa kitendo cha kugomea nafasi waliopewa na mh Rais kwenda kumsaidia kutekeleza ilani ni tatizo kubwa sana.
Na chakushangaza maafisa utumishi katika Halmashauri mbalimbali nchini wanawaunga mkono hao majamaa kwa kuisapoti CWT.
Wanaikandamiza CHAKUHAWATA ambayo kimsingi ipo kumsaidia mtumishi kwa ada nafuu za uanachama.
CHAKUHAWATA mwalimu mwanachama huchangia kiasi cha shilingi 5000 kwa mwezi pasi kujali kiwango cha mshahara wake.
CWT mwanachama huchangia kiasi cha shilingi 8000 hadi zaidi ya shilingi 40000 kulingana na kiwango cha mshahara kitu ambacho ni mzigo mkubwa kwa mtumishi.
Ukizingatia kuwa kanuni za ajira na mahusiano kazini zinampa uhuru mwajiriwa kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi lakini kwa walimu imekuwa tofauti.
Kujiunga na CWT imekuwa lazima ukishaajiriwa tu wanakuunga.
Sasa kuna ulazima gani kulazimisha uanachama kwa chama ambacho kinampinga mh Rais kwa kukataa hata teuzi zake jambo ambalo ni dharau kubwa wameonyesha waziwazi viongozi hawa wa CWT kwa kiongozi wa nchi.
Tunawaatarifu maafisa utumishi wapeni uhuru wao wafanyakazi wa kujiunga na chama cha wafanyakazi wanachokitaka wao.
Ahsante.
 
utawala wa mabavu kufifisha vyama vya wanataaluma vilivyokuwa huru mfano Chama cha Waalimu Tanzania- CWT, mawakili wa Tanganyika TLS, madaktari wa Tanganyika MCT ....
 
UTOVU WA NIDHAMU!

NANI AIJUAYE KESHO!!?

UKUU WA WILAYA NI FURSA YA KUPATA UWANJA WA KUONYESHA LEADERSHIP SKILLS!!!

MSHAHARA MKUBWA NA POSHO KUBWA SIO KILA KITU WAKUU!

CV,CONNECTION AND INTERACTON WITH V.I.PS OF THE STATE MATTERS MOST!

HUWEZI UKAWA MTUMISHI WA UMMA UKAGOMEA UTEUZI TOKA KWA NAMBA MOJA KISA MISHAHARA NA MARUPU RUPU LABDA KAMA ANGEKUWA KWENYE KAMPUNI AU PRIVATE SECTORS!!

WAMEONYESHA ULIMBUKENI NA USHAMBA PIA!
Wewe umenena
 
Back
Top Bottom