Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Walimu hawaitaki tena CWT, inawakata fedha kila mwezi kupitia mishahara yao kila mwezi maisha yote ya mwalimu.
TSC ifutwe pia iwepo board tu
Board itafanya vipi majukumu ya CWT? Ila hii nchi nawaonea huruma sana akina Lissu kama hizo katiba wanazofundisha majukwaani audience yao ndio nyie!!
 
Salaam Wakuu,

Japheth Maganga aliyetuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera akataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya alioteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

Japhet kasema, baada ya Kushauriana na Familia yake, alimuandikia rais Samia kumshukuru kwa kumteua pia na kumuomba atengue uteuzi wake na achaguliwe mtu Mwingine.

Wateule wengine ambao wamekataa uteuzi ni:

Leah Ulaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita na na Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

Wote waliokataa Uteuzi wa Rais Samia ni Viongozi wa juu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Leah Ulaya ni rais wa CWT, Dinah Mathamani ni Makamu wa Rais wa CWT huku Japheth Maganga akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

======

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.

Chanzo: DC mteule ahojiwa na polisi dakika 50, Rais CWT…

Chaeo Cha mkuu wa Wilaya hakina hadhi kwa Sasa. Unateuliwa kesho unatumbuliwa, si Bora ubaki kwenye mishe yako binafsi huna stress.
 
Board itafanya vipi majukumu ya CWT? Ila hii nchi nawaonea huruma sana akina Lissu kama hizo katiba wanazofundisha majukwaani audience yao ndio nyie!!
Mkuu watu hawaelewi maana ya chama cha wafanyakazi na chombo cha kitaaluma cha wafanyakazi...hili nalo ni janga la umma
 
Tunapochangia nadhani itapendeza sana kama tukielewa tunachokishauri kwa sababu naona kuna watu tunajiaibisha sana humu. Chama cha Wafanyakazi ni haki ya wafanyakazi ila chombo cha kitaaluma n.k siyo haki ingawa ni muhimu
 
Mkuu Lusungo, jf was meant to be a home of great minds, lakini all the people are not alike, tuna simple mind, ordinary mind and great minds, kama na wewe ambaye nilikuhesabu ni GT, kama ukinisoma humu unaona nautamani u DC usiku na mchana, then you are very wrong about me!.
Mamlaka ya uteuzi ni moja tuu, mtu anayeutamani uteuzi usiku na mchana, anaweza kuzungumza haya kuhusu mamlaka ya uteuzi?.
Na https://www.jamiiforums.com/threads...030-ndipo-aje-mwanamke.1980867/#post-42540531
Na https://www.jamiiforums.com/threads...-ya-kukoseshwa-tumvumilie-tumpe-muda.1883239/ na
Na https://www.jamiiforums.com/threads...ni-haki-si-uadui-si-chuki-si-kinyume.2043460/
P
Achana nae huyo mkuu..
 
Ukiteuliwa kwa mpango maalum hasa kwa manufaa ya nchi ama ya kiuchumi au kiusalama ni ngumu sana kukataa, huwezi bishana na tasisi wewe ni nani?
Hakuna cha teuzi kwa Mpango maalum wala maslahi ya taifa. Watu wanakanyagwa ili wazipate ndiyo maslahi taifa hayo? Watu wanateuliwa kwa ajili ya uchawa wao ndiyo maslahi ya taifa na uchumi na usalama huo?
Jaribuni kuwa serious. Yaani mtu aweke rehani ajira na maisha yake ili aje kutumbuliwa baada ya miezi 9kwa fitna za kisiasa?
 
Mnawajengea watu hali ya kutojiamini tu. Kwamba ukipe
Wa uteuzi hiyoo ni hukumu isiyo ma rufaa
Ana kesi ya ubadhirifu ambayo 100% ana hatia. Sasa kama wewe unamshauri ajiamini kukabiliana na uwezekano wa mashtaka hiyo ni juu yako.

Option aliyokuwa nayo ni kuchukua nafasi ya uteuzi kisha ukawepo ugumu kuendesha mashtaka. Kwa uzoefu wa katiba yetu mbovu ulivyo mkuu wa wilaya hakutwi na hatia kirahisi
 
Teuzi cha Mpango maalum wala maslahi ya taifa. Watu wanakanyagwa ili wazipate ndiyo maslahi taifa hayo? Watu wanateuliwa kwa ajili ya uchawa wao ndiyo maslahi ya taifa na uchumi na usalama huo?
Jaribuni kuwa serious. Yaani mtu aweke rehani ajira na maisha yake ili aje kutumbuliwa baada ya miezi 9kwa fitna za kisiasa?
Nimefuatilia huu ni uzi wa pili sasa unaongelea juu ya walimu kukataa uteuzi.

Nijuavyo mimi ni kuwa ukiwa mtumishi wa umma na ukateuliwa basi ajira yako haikomi. Unafanya utaratibu wa kuandika barua kwa mwajiri wako kuwa umeitikia wito wa Rais.

Siku ukitumbuliwa unarudi kwenye ajira yako na mshahara wako wa ukuu wa wilaya haubadiliki.

Ukiona mtu amekataa uteuzi lazima atakuwa na maslahi zaidi na hapo alipo.
 
Huyu ana nini pale CWT mpaka angomea Rais wa nchi? Naomba serikali ianzishe ukaguzi maalum, hasa ukizingatia yeye ni Katibu Mkuu, accounting officer ....je Kuna jambo anaficha kwamba akiondoka litabainika? Ana mirija ya wizi?

Nashauri dola imuamshie dude mapema kabisa. Hicho chama akione Kaa la moto. Afukuzwe ualimu tu, anakosa sifa za kushikilia cheo hicho.

Unaona kazi ya U-DC ni ya maana sana, na rais kwako ni Mungu, hivyo mtu akichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya inabidi atetemekee nafasi hiyo. Hiyo ni kazi ya majobless, na watu wanaojipendekeza.
 
UTOVU WA NIDHAMU!

NANI AIJUAYE KESHO!!?

UKUU WA WILAYA NI FURSA YA KUPATA UWANJA WA KUONYESHA LEADERSHIP SKILLS!!!

MSHAHARA MKUBWA NA POSHO KUBWA SIO KILA KITU WAKUU!

CV,CONNECTION AND INTERACTON WITH V.I.PS OF THE STATE MATTERS MOST!

HUWEZI UKAWA MTUMISHI WA UMMA UKAGOMEA UTEUZI TOKA KWA NAMBA MOJA KISA MISHAHARA NA MARUPU RUPU LABDA KAMA ANGEKUWA KWENYE KAMPUNI AU PRIVATE SECTORS!!

WAMEONYESHA ULIMBUKENI NA USHAMBA PIA!
CWT kunalima kama unabisha chunguza salary slip za walimu
 
Back
Top Bottom