Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Walimu hawaitaki tena CWT, inawakata fedha kila mwezi kupitia mishahara yao kila mwezi maisha yote ya mwalimu.
TSC ifutwe pia iwepo board tu
Board itafanya vipi majukumu ya CWT? Ila hii nchi nawaonea huruma sana akina Lissu kama hizo katiba wanazofundisha majukwaani audience yao ndio nyie!!
 

Chaeo Cha mkuu wa Wilaya hakina hadhi kwa Sasa. Unateuliwa kesho unatumbuliwa, si Bora ubaki kwenye mishe yako binafsi huna stress.
 
Board itafanya vipi majukumu ya CWT? Ila hii nchi nawaonea huruma sana akina Lissu kama hizo katiba wanazofundisha majukwaani audience yao ndio nyie!!
Mkuu watu hawaelewi maana ya chama cha wafanyakazi na chombo cha kitaaluma cha wafanyakazi...hili nalo ni janga la umma
 
Tunapochangia nadhani itapendeza sana kama tukielewa tunachokishauri kwa sababu naona kuna watu tunajiaibisha sana humu. Chama cha Wafanyakazi ni haki ya wafanyakazi ila chombo cha kitaaluma n.k siyo haki ingawa ni muhimu
 
Achana nae huyo mkuu..
 
Ukiteuliwa kwa mpango maalum hasa kwa manufaa ya nchi ama ya kiuchumi au kiusalama ni ngumu sana kukataa, huwezi bishana na tasisi wewe ni nani?
Hakuna cha teuzi kwa Mpango maalum wala maslahi ya taifa. Watu wanakanyagwa ili wazipate ndiyo maslahi taifa hayo? Watu wanateuliwa kwa ajili ya uchawa wao ndiyo maslahi ya taifa na uchumi na usalama huo?
Jaribuni kuwa serious. Yaani mtu aweke rehani ajira na maisha yake ili aje kutumbuliwa baada ya miezi 9kwa fitna za kisiasa?
 
Mnawajengea watu hali ya kutojiamini tu. Kwamba ukipe
Wa uteuzi hiyoo ni hukumu isiyo ma rufaa
Ana kesi ya ubadhirifu ambayo 100% ana hatia. Sasa kama wewe unamshauri ajiamini kukabiliana na uwezekano wa mashtaka hiyo ni juu yako.

Option aliyokuwa nayo ni kuchukua nafasi ya uteuzi kisha ukawepo ugumu kuendesha mashtaka. Kwa uzoefu wa katiba yetu mbovu ulivyo mkuu wa wilaya hakutwi na hatia kirahisi
 
Nimefuatilia huu ni uzi wa pili sasa unaongelea juu ya walimu kukataa uteuzi.

Nijuavyo mimi ni kuwa ukiwa mtumishi wa umma na ukateuliwa basi ajira yako haikomi. Unafanya utaratibu wa kuandika barua kwa mwajiri wako kuwa umeitikia wito wa Rais.

Siku ukitumbuliwa unarudi kwenye ajira yako na mshahara wako wa ukuu wa wilaya haubadiliki.

Ukiona mtu amekataa uteuzi lazima atakuwa na maslahi zaidi na hapo alipo.
 

Unaona kazi ya U-DC ni ya maana sana, na rais kwako ni Mungu, hivyo mtu akichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya inabidi atetemekee nafasi hiyo. Hiyo ni kazi ya majobless, na watu wanaojipendekeza.
 
CWT kunalima kama unabisha chunguza salary slip za walimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…