Licking Wounds
JF-Expert Member
- Nov 28, 2014
- 4,765
- 6,726
Ccm mnatafuta pa kutokea kwenye kila jambo yaniSiasa za Zambia ziko tofauti sana pia sheria yao kuhusu maziko ya marais ni dhaifu. Sheria yao haijatoa madaraka kwa serikali kusimamia mazishi ila familia ndo yenye uamuzi mkubwa. Hili la Lungu sio la kwanza. Hayati Mwanawasa na Keneth Kaunda pia kulitokea mvutano kati ya familia na serikali kwenye maziko. Na kabla ya hapo mwaka 1980 wananchi na familia walikataa serikali kujihusisha kwenye mazishi ya aliyekuwa makamu wa rais hayati Simon Kapwepwe. Rais Kaunda alizomewa msibani na hata jeneza lililotolewa na serikali lilikataliwa. Simon Kapwewe alizikwa bila jeneza.
Askofu Bagonza atumie mfano mwingine na sio huu wa Zambia.
Kitu kipo wazi kabisa halafu yeye anatafutatafuta visingizoo vya Kapwepwe.Ccm mnatafuta pa kutokea kwenye kila jambo yani
Huenda tunazungumza hadithi tofauti. Mpanda ngazi na mshuka ngazi hawashikani mikono. Lile bandiko lilizungumzia marais wa Zambia na mtoa mada akatutaka tujifunze. Nimetoa maoni kwa kuangalia muktadha huo. Mimi nimezungumzia maraisi kama mwandishi alivyozungumzia maraisi. La kujenga visasi kwa wanasiasa wengine linaweza likawepo ila mada iligusia maraisi.tumeshafika huko. Usijipe na kujiaminisha uongo. Hii list ya waliopotea ndiyo hivyo tunajenga visasi! Unadhani kweli Lisu ana nia kweli ya Uhaini? Mbowe kweli alikuwa na nia ya kutenda ugaidi? Tumeshafika hapo, it is only a matter of time! Chadema wanavyopigwa, kuuawa etc etc unadhani kweli kuna nuru huko mbele?
Nyumbu huwa mnafuata kila kitu atakachosema Bagonza na wanaharakati uchwara wengine.Ccm mnatafuta pa kutokea kwenye kila jambo yani
Sio lazima Bagonza ajue kila kitu. Ajikite kwenye mambo anayojua.Kwamba,hata Kapwepwe angekuwepo ungekuwa umemzidi umri na kuijua sana Zambia aliyoitolea mfano "kijana mdogo" Bagonza,siyo?
Tafuta tusi jipyaUWT acha kupanic
Yeye si mzembemzrmbe ndiyo maana anajua hadi amekukera.Sio lazima Bagonza ajue kila kitu. Ajikite kwenye mambo anayojua.
Aiseee!Hivi ukiwa UCHAWA hata uwezo wa kufikiria mambo ya kawaida unapoteaSiasa za Zambia ziko tofauti sana pia sheria yao kuhusu maziko ya marais ni dhaifu. Sheria yao haijatoa madaraka kwa serikali kusimamia mazishi ila familia ndo yenye uamuzi mkubwa. Hili la Lungu sio la kwanza. Hayati Mwanawasa na Keneth Kaunda pia kulitokea mvutano kati ya familia na serikali kwenye maziko. Na kabla ya hapo mwaka 1980 wananchi na familia walikataa serikali kujihusisha kwenye mazishi ya aliyekuwa makamu wa rais hayati Simon Kapwepwe. Rais Kaunda alizomewa msibani na hata jeneza lililotolewa na serikali lilikataliwa. Simon Kapwewe alizikwa bila jeneza.
Askofu Bagonza atumie mfano mwingine na sio huu wa Zambia.
Kwa anzia Leo na wewe naomba kublock kabisaHUYU MPUUZI NAYE HANAGA LA MAANA ANAJAMBAJAMBA TU HUMU SIJUI KALA MAHARAGE YA WAPI
Nyumbu mmezoea kupelekwa kama mizoga. Kila atakachosema Bagonza kwenue ni sawa tu.Aiseee!Hivi ukiwa UCHAWA hata uwezo wa kufikiria mambo ya kawaida unapotea
Weka pembeni uchawa kama ulivyo weka pembeni ELIMU yako.
Weka pembeni Umalaya wa kisiasa kama ambavyo umeweka pembeni mapenzi Kwa aliyekuwa mume wako
Jitwike kidogo tu akili na fikiria tena
Utawala Bora ni kutenda HAKI kwa yeyote awaye.Hichilema, Uchaguzi Mkuu ni mwaka kesho 2026.
Ameongelea jambo la aibu kwa muktadha ya Kinachoendelea kwenye nchi hiyo kwa Sasa, ulitaka ashuse kitini cha aibu za nyuma kama hizo ulizozitaja? Kwa manufaa Gani katika hoja aliyoitoa?Angetoa ujumbe bila kuhusisha siasa za Zambia asizozijua.
Hata nikikuelewesha hutaelewa kwa sababu umeshaamua kumkabidhi akili zako Bagonza.Ameongelea jambo la aibu kwa muktadha ya Kinachoendelea kwenye nchi hiyo kwa Sasa, ulitaka ashuse kitini cha aibu za nyuma kama hizo ulizozitaja? Kwa manufaa Gani katika hoja aliyoitoa?
Matukio ya Misiba ya Marais wa nchi husika kusababisha mivutano ni ya aibu sio ya aibu? Na je, ni zao la mapungufu kiutendaji wakiwa madarakani? Kama ndio basi huna pointHata nikikuelewesha hutaelewa kwa sababu umeshaamua kumkabidhi akili zako Bagonza.
Huyu Askofu ni kichwa sana, hekima nyingi na busara nyingi pia...Copy and Paste
HILI LA ZAMBIA KAMA SI FUNZO, NI KENGELE. By Bishop Bagonza.
Rais Mstaafu wa sita wa Zambia Edgar Lungu, amefariki tarehe 5/6/2025 akiwa matibabu huko Afrika ya Kusini. Atazikwa Afrika Kusini 25/6/2025 na misa itaongozwa na Askofu Mkuu wa Lusaka Alick Banda.
Wakati huo huo, serikali ya Zambia imefungua kesi ya kuzuia Rais Lungu asizikwe Afrika Kusini. Kesi hiyo itasikilizwa asubuhi saa 2 asubuhi, wakati ibada ya mazishi itaanza saa 4 asubuhi mjini Pretoria.
Rais wa saba, Hekainde Hichilema (HH) ndiye yuko madarakani. Familia ya hayati Lungu imekataa kukubaliana na serikali ya Zambia kuhusu taratibu za mazishi kwa kusema marehemu aliacha wosia kuwa akifa, Rais Hichilema asisogelee wala kuhudhuria mazishi yake.
Alipokuwa madarakani, Rais Lungu alimweka ndani Rais wa sasa mara 15 kwa tuhuma mbalimbali. Naye Rais Hichilema alipomshinda Lungu na kuingia madarakani, amemuweka katika kifungo cha ndani na kumnyima uhuru wa kutembea, kwenda kanisani na hata kugombea katika uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2026.
Yote haya yanatia aibu pande zote. Lakini kwetu Tanzania, haya kama si mafunzo kwetu, basi ni kengele ya kutuamsha tuweke mambo yetu vizuri.
1. Wale tulio madarakani kama mimi tujue ipo siku madaraka haya yataondoka, kwa njia nzuri au mbaya. Kutambua tu kuwa yataondoka, kutufanye kunyenyekea na kutenda wema na haki.
2. Wale wanaotafuta madaraka ni vema kutambua kuwa “mapenzi ya kuposea, siyo ya kuolea na kutunza ndoa”. Ni rahisi kulalamika kuliko kulalamikiwa. Mkiingia madarakani msitumie sheria mbaya zilizoachwa na watangulizi wenu kuwatesa wapinzani wenu wa kisiasa. Unyenyekevu si udhaifu bali unahifadhi nguvu na raslimali.
3. Ukiwa madarakani una uwezo wote wa kukataa ushauri unaopewa. Lakini, huna uwezo wala madaraka ya kukataa madhara ya ukaidi wako wa kukataa ushauri. Machozi yako wakati wa majuto ni kama yale ya samaki. Utazomewa hata na uliowasaidia. Nimeyaona kwa Lungu.
4. Kila aliye madarakani hutoa hotuba nzuri na maelekezo sahihi. Hotuba za Hichilema ni tamu na zinavutia, lakini zinaficha wingi wa kisasi na uchungu. Wasaidizi hawasikilizi hotuba zake; wanakumbuka aliyotendewa. Kiongozi mzuri ni mwenye uwezo wa kudhibiti chawa wake.
5. Familia za viongozi humwangusha kiongozi kabla hajaangushwa na wapinzani wake. Kiongozi anayelaumiwa na familia yake kwa “kutowasaidia”, anaweza kuwa kiongozi bora kuliko “anayebeba” familia nzima. Kiongozi “akiwasahau” ndugu zake, anakuwa amewaepusha na mateso baada ya yeye kuondoka. “Akiwabeba” anaondoka na kuzama nao. Nimeliona kwa Lungu.
6. Madaraka makubwa mikononi mwa mtu mmoja ni hatari kwake, marafiki na adui zake. Kwa kuwa ndugu na marafiki hawana kinga, ni hekima wakijitenga na mwenye madaraka. Kipimo halisi cha maadili ya mwenye madaraka makubwa, ni pale hata maadui na wapinzani wake wanapojiona wako salama mikononi mwake. Yaani adui yako usimwonee wala kumpendelea.
7. Kwa viwango vya siasa za Afrika, maisha mazuri baada ya kustaafu yanaweza kuwa yale ya “hukuharibu kitu na hukutenda la maana”. Kama ulionea, utasutwa. Kama ulitenda mazuri, yataharibiwa ukiona, ufe kwa kihoro. Kila kiongozi anakuja na mambo yake. Kwa hiyo? Sikiliza watu, usisikilize washauri wanaolipwa ili kukushauri. Ukistaafu utaishi na watu, siyo washauri.
Hichilema, Uchaguzi Mkuu ni mwaka kesho 2026.
Mtu anajiita chura kiziwiWatawala wetu ni vipofu na viziwi ndio maana hawaoni wala kusikia ila ndio dalili za mwisho la anguko lao.
HH anapendwa sana na Wazambia, hiyo 2026 asubuhi tu anashinda(sio kwa bao la mkono)Copy and Paste
HILI LA ZAMBIA KAMA SI FUNZO, NI KENGELE. By Bishop Bagonza.
Rais Mstaafu wa sita wa Zambia Edgar Lungu, amefariki tarehe 5/6/2025 akiwa matibabu huko Afrika ya Kusini. Atazikwa Afrika Kusini 25/6/2025 na misa itaongozwa na Askofu Mkuu wa Lusaka Alick Banda.
Wakati huo huo, serikali ya Zambia imefungua kesi ya kuzuia Rais Lungu asizikwe Afrika Kusini. Kesi hiyo itasikilizwa asubuhi saa 2 asubuhi, wakati ibada ya mazishi itaanza saa 4 asubuhi mjini Pretoria.
Rais wa saba, Hekainde Hichilema (HH) ndiye yuko madarakani. Familia ya hayati Lungu imekataa kukubaliana na serikali ya Zambia kuhusu taratibu za mazishi kwa kusema marehemu aliacha wosia kuwa akifa, Rais Hichilema asisogelee wala kuhudhuria mazishi yake.
Alipokuwa madarakani, Rais Lungu alimweka ndani Rais wa sasa mara 15 kwa tuhuma mbalimbali. Naye Rais Hichilema alipomshinda Lungu na kuingia madarakani, amemuweka katika kifungo cha ndani na kumnyima uhuru wa kutembea, kwenda kanisani na hata kugombea katika uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2026.
Yote haya yanatia aibu pande zote. Lakini kwetu Tanzania, haya kama si mafunzo kwetu, basi ni kengele ya kutuamsha tuweke mambo yetu vizuri.
1. Wale tulio madarakani kama mimi tujue ipo siku madaraka haya yataondoka, kwa njia nzuri au mbaya. Kutambua tu kuwa yataondoka, kutufanye kunyenyekea na kutenda wema na haki.
2. Wale wanaotafuta madaraka ni vema kutambua kuwa “mapenzi ya kuposea, siyo ya kuolea na kutunza ndoa”. Ni rahisi kulalamika kuliko kulalamikiwa. Mkiingia madarakani msitumie sheria mbaya zilizoachwa na watangulizi wenu kuwatesa wapinzani wenu wa kisiasa. Unyenyekevu si udhaifu bali unahifadhi nguvu na raslimali.
3. Ukiwa madarakani una uwezo wote wa kukataa ushauri unaopewa. Lakini, huna uwezo wala madaraka ya kukataa madhara ya ukaidi wako wa kukataa ushauri. Machozi yako wakati wa majuto ni kama yale ya samaki. Utazomewa hata na uliowasaidia. Nimeyaona kwa Lungu.
4. Kila aliye madarakani hutoa hotuba nzuri na maelekezo sahihi. Hotuba za Hichilema ni tamu na zinavutia, lakini zinaficha wingi wa kisasi na uchungu. Wasaidizi hawasikilizi hotuba zake; wanakumbuka aliyotendewa. Kiongozi mzuri ni mwenye uwezo wa kudhibiti chawa wake.
5. Familia za viongozi humwangusha kiongozi kabla hajaangushwa na wapinzani wake. Kiongozi anayelaumiwa na familia yake kwa “kutowasaidia”, anaweza kuwa kiongozi bora kuliko “anayebeba” familia nzima. Kiongozi “akiwasahau” ndugu zake, anakuwa amewaepusha na mateso baada ya yeye kuondoka. “Akiwabeba” anaondoka na kuzama nao. Nimeliona kwa Lungu.
6. Madaraka makubwa mikononi mwa mtu mmoja ni hatari kwake, marafiki na adui zake. Kwa kuwa ndugu na marafiki hawana kinga, ni hekima wakijitenga na mwenye madaraka. Kipimo halisi cha maadili ya mwenye madaraka makubwa, ni pale hata maadui na wapinzani wake wanapojiona wako salama mikononi mwake. Yaani adui yako usimwonee wala kumpendelea.
7. Kwa viwango vya siasa za Afrika, maisha bumazuri baada ya kustaafu yanaweza kuwa yale ya “hukuharibu kitu na hukutenda la maana”. Kama ulionea, utasutwa. Kama ulitenda mazuri, yataharibiwa ukiona, ufe kwa kihoro. Kila kiongozi anakuja na mambo yake. Kwa hiyo? Sikiliza watu, usisikilize washauri wanaolipwa ili kukushauri. Ukistaafu utaishi na watu, siyo washauri.
Hichilema, Uchaguzi Mkuu ni mwaka kesho 2026.