Mbona unaishi zamani sana.Siasa za Zambia ziko tofauti sana pia sheria yao kuhusu maziko ya marais ni dhaifu. Sheria yao haijatoa madaraka kwa serikali kusimamia mazishi ila familia ndo yenye uamuzi mkubwa. Hili la Lungu sio la kwanza. Hayati Mwanawasa na Keneth Kaunda pia kulitokea mvutano kati ya familia na serikali kwenye maziko. Na kabla ya hapo mwaka 1980 wananchi na familia walikataa serikali kujihusisha kwenye mazishi ya aliyekuwa makamu wa rais hayati Simon Kapwepwe. Rais Kaunda alizomewa msibani na hata jeneza lililotolewa na serikali lilikataliwa. Simon Kapwewe alizikwa bila jeneza.
Askofu Bagonza atumie mfano mwingine na sio huu wa Zambia.