#COVID19 Watendaji na walimu wakuu wanavyoenda kuteseka na fedha za COVID‐19 za IMF

#COVID19 Watendaji na walimu wakuu wanavyoenda kuteseka na fedha za COVID‐19 za IMF

Ml 20 darasa 1 mbona nyingi sana

Upumbavu mtupu na kutupotezea muda bila sababu

Milioni 20 najenga madarasa matano na hela inabaki
mkuu,
madarasa hayo ma5 yatakua navigezo vilivyo tajwa hapo kweli???
 
Wizi wizi wizi mtupu
Bwana wewe hakuna darasa linalojengwa kwa mil 10 usidanganye watu,usifikili darasa ni kibanda Cha kuuzia miwa,emu achana na story za vijiweni tafakari fanya upembuzi yakinifu tena,Watu Kama nyie ndo wale makandarasi mkipewa miradi mnaishia njiani kwakua mlikosea kukadilia GHARAMA mwisho wa siku miradi inakwama na hela za walipakodi mshapewa zote mifukoni imekauka
 
Tofali 500 x 1200 = 600,000, mawe lori 5 x 120,000 = 600,000, nondo 30 x 22,000 = 660,000, bati 40 x 30,000 = 1,200,000, cement 50 x 17,000 = 850,000, mchanga lori 5 x 100,000 = 500,000, misumari 20kgs x 6,000 = 120,000, fundi 1,500,000, mlango 200,000, madirisha 5 x 150,000= 750,000, maji 100,000, kokoto 300,000, vioo na ufundi 300,000, rangi na ufundi 500,000, nauli vifaa 100,000 dharura 1,000,000 jumla 9,280,00 na chenchi inabaki mkuu
Aluminum gani izo za 150,000/=, mkuu
 
Nlipata tenda ya kujenga madarasa 20 kwa 2mln kila darasa nikabidhi likiwa limeisha nimeitema tenda mchana kweupe
 
Tofali 500 x 1200 = 600,000, mawe lori 5 x 120,000 = 600,000, nondo 30 x 22,000 = 660,000, bati 40 x 30,000 = 1,200,000, cement 50 x 17,000 = 850,000, mchanga lori 5 x 100,000 = 500,000, misumari 20kgs x 6,000 = 120,000, fundi 1,500,000, mlango 200,000, madirisha 5 x 150,000= 750,000, maji 100,000, kokoto 300,000, vioo na ufundi 300,000, rangi na ufundi 500,000, nauli vifaa 100,000 dharura 1,000,000 jumla 9,280,00 na chenchi inabaki mkuu
Tofali 500 zinaishia kwenye msingi
 
Mkuu kachukue tenda ya kujenga madarasa Tena Jenga kwa hela yako mwenyewe,Ukimaliza serikali wakayapitisha madarasa hayo uchukue mpunga wote mkuu kwa faida kubwa.
Tatizo mkuu ni rushwa ndani yake, tukienda kiuhalisia 12M inamaliza darasa la kisasa na chenchi inabaki
 
Cement Sina hakika Kama itakuwa mifuko 50
Bati pia Sina hakika Kama zitakuwa 40 Sina hakika kama zinauzwa elfu 30
Tofali vyumba vyetu vidogo huwa vinakula tofali 400 iweje darasa ziwe tofali 500?

Sijaona Gypsum
Madirisha wameambiwa Aluminium
Sijaona tiles
Mifumo ya umeme
Mkuu kuna balance ya 3,720,000 kwenye 12? tumia hiyo kwa vitu vilivyobaki
 
Ninachojua ni kwamba kuna Walimu hata huo Ualimu wenyewe hawaupendi.Hao ni wale wenye One na Two zao ambao baada ya kukosa connection zingine ikabidi waingie huko ili kupoza njaa.Na ni wengi sana huko kwa sasa!
Hapa sijaelewa kaka,baada ya kukosa Connection kwenye ajira au kwenye kozi aipendayo ndiyo akaona asomee ualimu ?
 
Kuna balance ya 3,720,000 ita-cover hayo yote

kwa viwango vinavyo itajika na serikali, io pesa ni ndogo,
ila kwa kujenga jenga tuu, ili kuzuia wanafunzi wasilowe mvua,
io pesa inaweza tosha jenga ilo darasa moja..
 
Nawasalimu sana kwa jina la JMT yetu pendwa!

Baada ya mheshimiwa raisi kuagiza fedha za imf kwenda kwenye elimu na kujenga madarasa ili watoto wa f1 mwakani wasipate tabu ya kusubiri, na tamisemi kazipangia bajeti na kuzigawa, kazi imeanza huku chini (wilayani). Viongozi (wakurugenzi na maafisa elimu) wakiibuka na 'majuhudi' kibao ya kutaka kufanya 'maajabu' ili wawe wa mfano. Bahati mbaya sana, 'majuhudi' yao hayo, yanaenda kuwaangukia na kuwaumiza watendaji na zaidi wakuu wa shule.

Kwa siku chache tu, kuna halmashauri fulani, kwa wakati tofauti, tayari wakuu wa shule wameambiwa (of course kuamrishwa) yafuatayo:

1. Darasa lililolengwa likamilike lakini ni lazima na kitu kingine kitokee (yaani wahakikishe wameanzisha kitu kingine pia k.v boma, ofisi, choo n.k kutoka katika fedha hizo hizo)
2. Madarasa yawekwe marumaru (tiles)
3. Bati ziwekwe za msouth
4. Madirisha ya aluminium
5. Mfumo wa umeme wote ukamilike

Barua za kuwakabidhi fedha hizo zinaandaliwa kwenda kwa wakuu hao kwa majina yao na atakayeshindwa kukamilisha majengo hayo kwa viwango tajwa kazi anayo. Ikumbukwe kuwa fedha zilizotolewa ni m.20 tu kwa chumba kimoja cha darasa. Hapo sidhani kama watendaji na wakuu hawa watakuwa na ujanja mwingine wowote zaidi ya kurudi kwa wanakijiji kuwaambia wajitolee.

AISEE! Kujitolea kipindi hiki ni vigumu kuliko maelezo, siajabu kijiji cha watu 2000 wakajitolea watu 7 tu tena kwa siku mbili tu.

Wakuu wa shule kiukweli kazi wanayo. Huku mitihani ya kitaifa, kule ujenzi uliyoongezewa maagizo. Dah!!!
 
Ahsante, hofu yangu ni kama hayo maagizo yatafuatwa au la!
 
Back
Top Bottom