Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

waziri wa fedha mwigulu lameck nchemba tunaomba ulisaidie taifa kuthibiti ubadhilifu huo kwa kuwa rais amekuamini kukaa hapo na katibu wako msisubiri waziri mkuu kufika na kuongelea hayo.
Kitendo cha PM kwenda pale na kuyabaini hayo madudu ni sababu tosha kabisa kwa Waziri husika kuachia ngazi, ni kashfa kubwa
 
Huyu mzee naye huwa simwelewi hata kidogo ndiyo maana anapambana kupaka nywele rangi aonekane ni kijana maana ndiyo akili yake imeishia hapo kwa vidosho, watu wanapakua mabilioni akina Lugola, Makonda, Sabaya, Mnyeti n.k lakini ndiyo kwanza anacheka nao.
Bado unaendelea kulala au kuamka
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.

Ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ACP Salum Hamdun kufanya uchunguzi. Tuhuma mojawapo inayokabili ni malipo ya Milioni 251 yaliyofanyika Machi 31, 2021 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi na waliohusika.

======

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.

Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.

Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.

Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.

"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.

Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.

Chanzo: Mwananchi
Magufuli alisema mtanikumbuka kwa mazuri na si kwa mabaya huu ni mwanzo tu...makubwa yanakuja.............
 
Katika mambo ambayo nilimshangaa mama,ni kumteua Mwigulu kuwa waziri wa fedha.Hapo nilikata tamaa kabisa na kuona mama hayuko serious.

Wizara ya fedha unataka mtu ambaye yuko committed, asiyekuwa mwamasiasa,mtendaji muadilifu asiyechoka.Si mpenda sifa na utukufu bali mnyenyekevu anayemcha Mungu.Mwigulu hana sifa hizo japo kidogo.

Nakuombea rais wangu Mungu awe nawe kwani najua kazi uliyonayo ni ngumu,ijapo sie tunaiona rahisi.

Kumbuka huyo ni mgombea urais.Atafanya chochote apate pesa ya kuandika maandishi ya kampeni kwenye mawe yote nchi nzima
 
Kiini machoz hakuna lolote hawa wamepangwa wasimame kwa niaba ya pm na bashiru et al ndio walilamba mshiko wakati wa sekeseke la mswiba wa jpm
 
"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.
Naomba ku-paraphrase... "Sisi tulikuwa Mwanza tunalipana Posho na nyinyi hapa ndani mnalipana Posho"

Au Mwanza kulikuwa hakuna Posho ?
 
Magufuli alisema mtanikumbuka kwa mazuri na si kwa mabaya huu ni mwanzo tu...makubwa yanakuja.............
Kwahio unadhani enzi zake kulikuwa hakuna upigaji ? Tofauti ni kwamba enzi zake upigaji mwingine usingesikia ingawa hata sasa angalau tunasikia robo tatu ingawa sio wote..., enzi za mwendazake ungesikia tu ule aliotaka yeye usikie...
 
Hii Wizara kama wameweza kufanya hayo basi wafanyakazi wote wa hii wizara wanatakiwa kuondolewa kabisa serikalini. Dawa ni kuisafisha hiyo wizara. Bila hivyo hakuna kitakachorekebika bila hatua stahiki.
Ni watu wawili tu hapo waziri na katibu mkuu, hao wengine ni kuwaonea
 
Tutamkumbuka JPM..

Waziri wa fedha ivi ni nani?
Una shida wewe
Hizi pesa zimetumika wakati jpm akiwa hai au mara baada ya kufariki..
Mbona wakati wa jpm kila siku alikuwa anatumbua na kusimamisha watumishi
Akili umeipeleka likizo.
Jpm alikuwa mfujaji wa fedha za umma kuliko rais yoyote
 
Haya madudu ndiyo yanayowafanya waandike kwamba sasa hivi wana furaha zamani hawakuwa na furaha.

Lakini sauti ya Majaliwa ina mamlaka ndani yake ndiyo maana wako bize kumfundisha rais Samia kuwa amtoe kwenye uwaziri mkuu kwa sababu eti ni masalia ya JPM!

Kwani SAMIA ni masalia ya nani?
True umesema kweli ndugu,
 
Kama waziri mkuu Kassim Majaliwa alikuwa hajui huu utaratibu basi inabidi ajitafakari sana. Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa watumishi wa serikali kulipana posho kwa kazi nyingi za ofisini kama kuandika taarifa za mwezi na mwaka, kuandika hotuba za bajeti, kuandika taarifa mbalimbali za utendaji kazi zao nk.

Hakuna kazi serikali inayofanywa bila posho na hii imesababisha ugumu kwa viongozi katika kuwasimamia watumishi walio chini yao kama hakuna fedha. Bila posho kazi itafanyika kwa mbinde sana au huyo boss atoe ahadi ya posho pindi fedha itakapopatikana, na ahadi yenyewe iambatane na kuandikwa kwa vocha.

Kwa hiyo hii hatua anayotaka kuichukua waziri mkuu haitafanikiwa kwani posho hizi zilikwisha halalishwa wizara zote na watumishi wanajua kuwa ni haki yao. Vinginevyo asubiri mgomo baridi na ufanisi hafifu kutoka kwa watumishi.
Kweli kabisa. Mishahara midogo isiyokidhi mahitaji hata yale ya muhimu ndiyo tatizo linalosababisha yote hayo. Mtu umekaa miaka ishirini kazini lakini mshahara wenyewe mmmmmh, tena hapo unazo degree zako mbili tayari.
 
Si kuna wakaguzi wa ndani ambao kazi yao kubwa ni kufanya pre-audit kabla ya payment yoyote na kuhakikisha utaratibu unafuatwa
Kawaida hawana nguvu au nao wako kwenye orodha, nakama walikuwa kwenye payroll hapo vocha inatembea kama msg ya whatsap
 
Hii inatisha sana!!!
wakati baadhi ya watumishi wanadai haki zao za malimbikizo ya mishahara tangu mwaka 2018 kumbe kuna watumishi hazina wanajilipa mamilioni kwa wiki mbili!!!
haki za watu wamezikalia, kwa hili Mungu hawezi kuwasamehe.
 
Wasalaam wanajamiiForums!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
Ni kweli Wizara ya Fedha inatakiwa apewe Mchumi mahili ambaye hana ambitions za kisiasa.
 
Back
Top Bottom