Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Huyu mzee naye huwa simwelewi hata kidogo ndiyo maana anapambana kupaka nywele rangi aonekane ni kijana maana ndiyo akili yake imeishia hapo kwa vidosho, watu wanapakua mabilioni akina Lugola, Makonda, Sabaya, Mnyeti n.k lakini ndiyo kwanza anacheka nao.
Utamuelewa vp na unaanza kumjadili yeye na kutetea majizi? mnataka pesa zirudi mtaani kupitia wizi wa fedha za walipa kodi!
 
Hivi JPM alikutenda nini? Kila siku ni kumpalamikia kama msimbe
Wee ulikuwa ndo mwimbaji mapambio mkuu nini?
Pole yameingia maji, hayamvutii SSH wala wahanga wa ukandamizaji na ukatili wa awamu ya tano .
Yafaa ujitahidi ukatafute kazi nyingine itakusaidia kukutibu roho yako na uweze kuachana na chuki kwa wenye majeraha, wanaoanika ubaya wa Mwendazake.
 
Hii kesi Majaliwa anaangukia pua
Watetezi wa mafisadi mpooo,si ndugu zenu banaaa ndo wapi hizo taasisi wanakula mpunga tu kwa vikao visivyo na tija.
Afu mzunguko wa fedha unarudi siyo!
Ndo fedha mlizokua mnadai zimeadimika mtaani
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.

Ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ACP Salum Hamdun kufanya uchunguzi. Tuhuma mojawapo inayokabili ni malipo ya Milioni 251 yaliyofanyika Machi 31, 2021 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi na waliohusika.

======

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.

Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.

Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.

Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.

"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.

Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.

Chanzo: Mwananchi
Dotto James yuko wapi? Aanze naye
 
Tatizo lako umeamini porojo za kigogo ambazo hazina ukweli wowote. Hao akina Doto na Bashiru Kama wangefanya ubadhirifu wangeendelea kuaminiwa kuwa viongozi? Mbona mkurugenzi wa Bandari alisimamishwa kazi kupisha uchunguzi?
Mbona report ya tume haijasomwa, je wale waliotajwa na CAG kama kingwangwala wamechukuliwa hatua gani? double standard ndiyo inaumiza watu, sheria ni kwa wote si kwa ajili ya watu fulani
 
Waziri mkuu kasimu majaliwa amefanya ziara ya kushitukiza wizarani na kubaini ubadhilifu wa fedha zaidi ya milion 500! Ubadhilifu huo umeanzia march 21 mwaka huu ambapo watumishi wamejilipa posho mbalimbali za kazi ambazo zinauwalakini na hata hivyo posho zimelipwa kwa kutumia majina ya vyeo na sijana la mtu halisi kama alivyotoa maelezo katika vyombo vya habari, kutokana na hili waziri wa fedha mwigulu lameck nchemba tunaomba ulisaidie taifa kuthibiti ubadhilifu huo kwa kuwa rais amekuamini kukaa hapo na katibu wako msisubiri waziri mkuu kufika na kuongelea hayo.
 
Niliwahi kuleta uzi hapa kwamba wapigaji tumerudi mjini tokea tarehe 18 march 2021 uzi ukafutwa.

JPM alikua kiboko.. yeye ndio alikua sheria.

Ila kwa kutumia sheria zetu hizi huwezi epuka upigaji.

Kwani Approval zipoje huko serikalini, fedha inatokaje bila signature ya katibu mkuu wa wizara husika au waziri?

Mwigulu atwambie kama kweli hakua na taarifa.. au na yeye yumo kwenye mamho haya.
Hakuwa kiboko report ya CAG isingekuwa chafu vile
 
Mwigulu hana uwezo huo.
Dr mpango alikua waziri hiyo trh 21 march kwahyo nae anahusika kwan namna moja au nyingine
 
Waziri mkuu kasimu majaliwa amefanya ziara ya kushitukiza wizarani na kubaini ubadhilifu wa fedha zaidi ya milion 500! Ubadhilifu huo umeanzia march 21 mwaka huu ambapo watumishi wamejilipa posho mbalimbali za kazi ambazo zinauwalakini na hata hivyo posho zimelipwa kwa kutumia majina ya vyeo na sijana la mtu halisi kama alivyotoa maelezo katika vyombo vya habari, kutokana na hili waziri wa fedha mwigulu lameck nchemba tunaomba ulisaidie taifa kuthibiti ubadhilifu huo kwa kuwa rais amekuamini kukaa hapo na katibu wako msisubiri waziri mkuu kufika na kuongelea hayo.
Mpaka waziri mkuu agundue yeye alikiwa wapi?
 
Watetezi wa mafisadi mpooo,si ndugu zenu banaaa ndo wapi hizo taasisi wanakula mpunga tu kwa vikao visivyo na tija.
Afu mzunguko wa fedha unarudi siyo!
Ndo fedha mlizokua mnadai zimeadimika mtaani
hueleweki
 
Huyo chawa ana bahati ya uteuzi kweli [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hayo yaliyofukuliwa hapo hazina ni TIP OF AN ICEBERG!!! Kuna uvundo mwingi sana hapo kiasi kwamba wakifuatilia sana , itaonekana kuwa kumteua Dr. Mpango kama makamu wa Rais lilikuwa ni kosa kubwa sana!!!
 
Wasalaam wanajamiiForums!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
Hapo kwa CAG ASSAD NDIO UMEKOSEA UNAJIPIGIA CHEPUO MWENYEWE ACHA USHAMBA
 
Back
Top Bottom