Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Siwatetei na ni Jambo jema sana Kuwachukulia Hatua za Kisheria ila ili Watanzania tunaojitambua Kichwani ( Akilini ) tuamini kuwa Serikali ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan haina Double Standards tunaomba iwaunganishe Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ( sasa yupo Wizara ya Viwanda ) Dotto James kwani hawa ndiyo wanawajibika zaidi Kimaamuzi na siyo hawa Wakaguzi ambao Kimsingi naona ni kama mnawaonea tu kwa Gharama za Kuwaogopa akina Mpango na Dotto.
 
Kazi ipo.
 
Pumba tupu, endeleeni kupiga makofi na vigelegele.
 
Usicheke [emoji1787][emoji1787][emoji1787]! Kuna mambo ya ajabu sana katika utumishi wa serikali. Ukiyachunguza kwa makini unaweza kudhani siyo watumishi bali ni wataalam washauri wa serikali.

Posho ndiyo lugha wanayoifahamu!
Inaonyesha walikuwa na njaa sana ,watakuwa ni miongoni mwa waliofurahu kifo cha magu ,yaani nj Kama mbwa wanaosubiri makubwa kwa hali na mali
 
Video: Ndugu zangu Watanzania, taifa letu litajengwa na wenye moyo lakini litaliwa na wenye meno. Nawatakia wikiendi njema

Nawaomba wakati mnapumzika mtafakari yanayojiri kwenye hizi video. Natanguliza samahani kwa kufanya juhudi ya kuzihariri kidogo ili zisichoshe kuzisikiliza.

1.

Your browser is not able to display this video.


2.

Your browser is not able to display this video.


3.

Your browser is not able to display this video.


4.

Your browser is not able to display this video.


5.

Your browser is not able to display this video.


6.

Your browser is not able to display this video.


Sitaongeza neno ila wakati unaangalia hizi video, zitazame kwa makini nyuso za hao wasikilizaji halafu ujiulize kama kuna sababu ya kuhangaika na maisha hapo ulipo.

===

Dar es Salaam. Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.

Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.

Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.

Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.

"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.

Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.

Credit: Mwananchi

Zaidi, soma; Kwa wizi huu, Dkt. Mwigulu Nchemba achia ngazi, jiuzulu
 
Siku tutakapoamua kuachana na kuyachekea matukio kama haya, huo ndio utakaokuwa mwanzo wa nchi yetu kupiga hatua za uhakika na haraka kuelekea kwenye maendeleo halisi ya nchi yetu.

Najaribu tu kukumbuka mfano halisi hapa:

Baadhi ya raia wa China wanapokuja hapa kwa sababu zao mbalimbali, na wengine kwa matembezi ya muda mfupi tu, wanatumia mwanya huo kuona kama wanaweza kutengeneza hela nyingi kwa haraka haraka kwa kutumia mianya wanayoiona hapa kuwaruhusu kufanya hivyo.

Hawa watu wanapokuwa huko kwao hawathubutu kamwe kujihusisha kwenye mambo wanayotufanyia wakiwa hapa. Bila shaka wanao uelewa mzuri sana kinachoweza kuwatokea wakiyafanya hayo wakiwa huko kwao.

Nasi tunahitaji kuzijaribu hizo njia wanazotumia China kuondoa uozo wa aina hii hapa kwetu.

Nayasema haya kwa moyo safi kabisa bila ya kutishwa wala kutetereshwa na kelele nyingi zinazoambatana na kutekeleza adhma hiyo hapa kwetu.
 
Chukueni pesa wajomba mnufaike na familia zenu make hata msipo zichukua hazinisaidii kitu mkizichukua nitakutana nazo kitaa Bora mZichukue mnufaike wengi kuliko kuziacha wanufaike wachache nasema chukueni mpunga ukiwa kitengo piga mpunga WA maana ukisimamishwa KAZI life linaenda kivingine tayari unampunga mbwa haruki
 
Mbona huo upigwaji hujaueleza ?
 
NSSF fao la kujitoa Mmetubebesha aiseeh huko jehanam ikibidi makaa ya Mawe.....
 
Kwa hali yoyote ile hiyo hela ilikuwa inaishia mifukoni mwa watu 3 au wa 5 na ndio maana ukwapuaji ukafanyika na siku za sikukuu. Na ukitaka kuwanasa vizuri wambie wakuonyeshe hizo kazi maalum au mpango kazi uliowafanya wachote hiyo hela, utaona wanaangalia vidole. Wameanza KUMZINGUA MOTHER.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…