Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Haya madudu ndiyo yanayowafanya waandike kwamba sasa hivi wana furaha zamani hawakuwa na furaha.

Lakini sauti ya Majaliwa ina mamlaka ndani yake ndiyo maana wako bize kumfundisha rais Samia kuwa amtoe kwenye uwaziri mkuu kwa sababu eti ni masalia ya JPM!

Kwani SAMIA ni masalia ya nani?
 
Hawa wangekatwa pumbu tu, wasichekewe hata kidogo.

Sasa hivi ni mashambulizi kila upande kama vile machinga wanavyovamia gari la City, kila mtu na kamuhogo kake jamani!
IMG_20210528_061543.jpg
 
Kassimu anaacha kuongelea zilizochotwa na doto james,bashiru,kakonko anatuletea blahblah tu...huyu ndio PM mwenye elimu kma lusinde kibajaji
Tatizo lako umeamini porojo za kigogo ambazo hazina ukweli wowote. Hao akina Doto na Bashiru Kama wangefanya ubadhirifu wangeendelea kuaminiwa kuwa viongozi? Mbona mkurugenzi wa Bandari alisimamishwa kazi kupisha uchunguzi?
 
Kweli hii ni vita tena Vita ngumu sana,
Mama kuwa makini sana, namuomba mungu azidi kukupa nguvu
 
Huyu mzee naye huwa simwelewi hata kidogo ndiyo maana anapambana kupaka nywele rangi aonekane ni kijana maana ndiyo akili yake imeishia hapo kwa vidosho, watu wanapakua mabilioni akina Lugola, Makonda, Sabaya, Mnyeti n.k lakini ndiyo kwanza anacheka nao.

Na wewe hueleweki...

Hawa uliowataja "wanapakua...." au "walipakua fedha ya umma?"

Hebu rekebisha "wakati" hapo. Kwamba, msomaji aelewe iwapo unaongelea wakati huu wa sasa au uliopita...

Kwa sababu as far as it concerned, hawa uliowataja karibu wote hawapo serikalini...
 
Huu ni upuuzi tu, unless mwandishi kakosea. Sina hakika kama ni kazi ya Mkaguzi Mkuu kufanya kazi ya Pre-Audit. My understanding pre-audit inafanyika kabla malipo hayajafanyika. Hii ni kazi ya Mweka Hazina/ Accountant. Lingekuwa ni tukio la mwaka uliopita ambao tayari Mkaguzi ameufanyia kazi, basi ningemuelewa Majaliwa.
Napataga shida kumuelewa huyu bwana.
Si kuna wakaguzi wa ndani ambao kazi yao kubwa ni kufanya pre-audit kabla ya payment yoyote na kuhakikisha utaratibu unafuatwa
 
Haya madudu ndiyo yanayowafanya waandike kwamba sasa hivi wana furaha zamani hawakuwa na furaha.

Lakini sauti ya Majaliwa ina mamlaka ndani yake ndiyo maana wako bize kumfundisha rais Samia kuwa amtoe kwenye uwaziri mkuu kwa sababu eti ni masalia ya JPM ,!!
Kwani SAMIA ni masalia ya nani??
Umewaongelea vizuri sana wapigaji. Wanasema hata Dr Mpango hafai kuwepo kama Makamu wa Rais eti ni mkali sana na nafasi yake anatakiwa kuwepo mtu mpole wa kufanya kazi ya kukata utepe tu.
 
Niliwahi kuleta uzi hapa kwamba wapigaji tumerudi mjini tokea tarehe 18 march 2021 uzi ukafutwa.

JPM alikua kiboko.. yeye ndio alikua sheria.

Ila kwa kutumia sheria zetu hizi huwezi epuka upigaji.

Kwani Approval zipoje huko serikalini, fedha inatokaje bila signature ya katibu mkuu wa wizara husika au waziri?

Mwigulu atwambie kama kweli hakua na taarifa.. au na yeye yumo kwenye mamho haya.
 
Hii habari haijakaa sawa.

Taratibu za fedha zina mtu aliyeomba hiyo fedha, wapo walioidhinisha hayo malipo, ndo na mkaguzi ni mmojawapo, yupo aliyelipwa, aliyetumia nk.

Na kila kitu kipo kwenye mfumo wa fedha.

Mtu muhimu ni aliyeinitiate hayo malipo. Faili la malipo lipo online.
Comedy show!
Aliye initiate nani?? Au ndiyo kina Kurwa!
Auditors ni mbuzi wa kafara tu!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma...
Salum Hamdun ni ACP...!?
 
Back
Top Bottom