Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Mkasa wenyewe wa hazina huu hapa:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.

Ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ACP Salum Hamdun kufanya uchunguzi. Tuhuma mojawapo inayokabili ni malipo ya Milioni 251 yaliyofanyika Machi 31, 2021 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi na waliohusika.

======

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.

Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.

Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.

Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.

"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.

Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.

Chanzo: Mwananchi
 
In other words amepiga mkiani badala ya kichwani
 
Hatari sana maana hata sijui nianze kuandika wapi, kweli hivi ni rahisi pesa kutoka namna hii mamilioni watu wanavuta tu na wenye mamlaka wako kimyaa mimi nadhani kuna mengi zaidi ya haya huu mfumo wetu wa malipo hauko sawa kabisa corrupted. Wacha niache hapa naweza kutukana tu mtu analipwa mshahara halafu anajilipa tena ndani ya mshahara sasa huyu contractor au employee.
 
Mkuu sahau kabisa viongozi wa kiafrika kujiuzulu , hungangana mpaka hatua ya mwisho
 
Ukaguzi wa hazina kwa matumizi yaliyofanyika kati ya Januari na Machi umefikia wapi? Vipi; posho wanazolipwa wabunge wa viti maalum wasiokuwa na chama ni halali? "Kweli tunaliwa kimyakimya!"
 
Vijana wa Leo ni waoga Sana, nakubaliana na wewe Kwa mambo yanayoendelea Kwenye wizara ya fedha kwamba, hayakubaliki na mhusika awajibike, Lakini stakubaliana na wewe kumpigia Debe msaafu kurudi tena kazini, wstaafu tuwapongeze Kwa kazi nzuri waliyoifanyia nchi hii Ila sio kurudi ofisini tena, vijana tutafanya kazi gani??
 
pengo la magu linaonekana taratibu
Pengo la magu gani bana hapo walikuwa ndugu zake tupu wangechukua hata bilion we ungejulia wapi ndiyo maana hatukutaka udikteta leo waziri ana ujasiri wa kukemea hayo ni vile tu hujui kuwaza angekuwa huyo Magufuli wako huyo waziri mkuu angeongea kitu kwa hao watoto wa dada ake bosi hapo fedha?
Makonda Paul ni bilionea, Sabaya tu ni bilionea we ungesemea wapi hayo
Acha watu wafanye kazi Magufuli nani bana aende zake
Waza vizuri siyo uwaze upande upande
 
Hii nchi ilimshinda "jiwe", hayo "maji" ya Zanzibar ndiyo yataweza? Maji yenyewe yamelegeaa, sijui, wacha tuone.
 
Hikubariki na haitakubarika watumishi wa umma ambao wanalipwa mishahara wajilipe posho milioni 400 siku moja!

Huu ni wizi wa mchana kweupe!.

Sasa naanza kuelewa kwa nn wale jamaa walitaka kupora urais wa mama. Ni kweli kwamba mwanamke hawezi kuwa rais bora hapa Tanzania? Bado naamini imawezekana. Mama, Mh. Suluhu Rais wangu, mwenye jinsia ya kike. Fanya jambo juu ya waziri huyu mzembe ili wasioamini utendaji wa mwanamke wakuelewe vizuri.
 
Hakuna wa Kujiuzulu hapo wana Uchu wa Madaraka hao
 
Afadhali sasa wakati ule ukiambiwa kazi maalum utahoji na kuuliza za nini kwa sasa watu wanaujasili wa kuhoji na kuandika na sisi tunajua ndo faida ya uhuru wa vyombo vya habari na maoni si ajabu tumeibiwa sana kwa jina la kazi maalumu
 
Nakunaliana kabisa Mwigulu kujiuzulu kama Waziri wa Afya. Umeharibu kwenye paragraph ya pili toka mwisho ulipo mtaja Ummy Mwalimu kuwa awe mbadala kwenye Fedha. Kwenye Afya wanalalamika upotevu wa dawa na MSD kama imekufa ambayo yeye ndiye alikuwa msimamizi kuanzia Novemba 2015 hadi December 2020.

Dr Gwajima ana miezi 5 tu pale Afya.
 
They will always be a difference between a loved leader, and feared and loved leader.

A loved leader: you work and live without consequencies for mission or omission.

A feared leader: you work and live with consequences for mission or omission.
 
Chuki binafsi potea huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…