Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa wawili tu. Hapi hatuhitaji uchunguzi ni kuanzia KM na watendaji wote sasa wangekuwa Isanga prison!Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.
Ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ACP Salum Hamdun kufanya uchunguzi. Tuhuma mojawapo inayokabili ni malipo ya Milioni 251 yaliyofanyika Machi 31, 2021 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi na waliohusika.
======
Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.
Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.
Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.
Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.
Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.
Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.
Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.
"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.
Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.
Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.
"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.
Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.
Chanzo: Mwananchi
Huyu kama Rais hatamtumbua basi tutegemee utendaji mbovu zaidi. Hapa waziri ni mzembe kupita kiasiWasalaam wanajamii forum!
Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.
Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.
Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.
Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.
Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.
Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
Kipi kilichofanywa na Ummy hadi useme ni kiboko ya mafisadi?Wasalaam wanajamii forum!

Kina nani hao mbona huwataji?Hikubariki na haitakubarika watumishi wa umma ambao wanalipwa mishahara wajilipe posho milioni 400 siku moja!
Huu ni wizi wa mchana kweupe!
Mama yetu mpendwa anza na hawa nyani vinginevyo tutavuna mabua. Usiwahurumie hata kidogo. Kwa kuwa wao hawana huduma na kodi zetu,tengua viuno wote,including waziri wao kama hatachukua jukumu la kujiuzulu mwenyewe.
Anza na wabunge kwanza wana mishahara minono 12M per moon lakini bado wanalipwa 340000 kwa sikuHikubariki na haitakubarika watumishi wa umma ambao wanalipwa mishahara wajilipe posho milioni 400 siku moja!
Huu ni wizi wa mchana kweupe!
Mama yetu mpendwa anza na hawa nyani vinginevyo tutavuna mabua. Usiwahurumie hata kidogo. Kwa kuwa wao hawana huduma na kodi zetu,tengua viuno wote,including waziri wao kama hatachukua jukumu la kujiuzulu mwenyewe.
Mchemba na Masauni.Kina nani hao mbona huwataji?